Kaimu
Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Utamaduni katika Wizara ya Habari
Utamaduni Sanaa na Michezo, Bibi. Lily Beleko akiwahutubia wageni
waalikwa wakiwemo Mapadre, Masista pamoja na Viongozi mbalimbali wakati
wa Uzinduzi wa Kamusi ya Ukristo uliofanyika Baraza Katoliki la Maaskofu
Tanzania (TEC) Kurasini Jijini Dar es Salaam 17 Agosti, 2016.
Katibu
Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) Padre Ubadius
Kidavuri akiwahutubia wageni waalikwa wakiwemo Mapadre, Masista pamoja
na Viongozi mbalimbali wakati wa Uzinduzi wa Kamusi ya Ukristo
uliofanyika Baraza Katoliki la Maaskofu Tanzania (TEC) Kurasini Jijini
Dar es Salaam 17 Agosti, 2016.
Mwandishi
wa Kamusi ya Ukristo, Padre Jorad Nyenyembe akiwahutubia wageni
waalikwa wakiwemo Mapadre, Masista pamoja na Viongozi mbalimbali wakati
wa Uzinduzi wa Kamusi ya Ukristo uliofanyika Baraza Katoliki la Maaskofu
Tanzania (TEC) Kurasini Jijini Dar es Salaam 17 Agosti, 2016.
Katibu
Mtendaji Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) Dkt. Selemani Sewangi
akiwahutubia wageni waalikwa wakiwemo Mapadre, Masista pamoja na
Viongozi mbalimbali wakati wa Uzinduzi wa Kamusi ya Ukristo uliofanyika
Baraza Katoliki la Maaskofu Tanzania (TEC) Kurasini Jijini Dar es Salaam
17 Agosti, 2016.
Mkurugenzi
Mkuu wa Kampuni ya Uchapishaji Vitabu ya Mkuki na Nyoka, Bw. Walter
Bugoya akiwahutubia wageni waalikwa wakiwemo Mapadre, Masista pamoja na
Viongozi mbalimbali wakati wa Uzinduzi wa Kamusi ya Ukristo uliofanyika
Baraza Katoliki la Maaskofu Tanzania (TEC) Kurasini Jijini Dar es Salaam
17 Agosti, 2016.
Baadhi
ya wageni waalikwa katika Hafla ya Uzinduzi wa Kamusi ya Ukristo
wakifuatilia uwasilishwaji wa hotuba mbalimbali toka kwa Viongozi na
Mgeni rasmi wa hafla hiyo 17 Agosti, 2016 Jijini Dar es Salaam.
(Picha/Habari na Benedict Liwenga-WHUSM).
Serikali
imempongeza Mwandishi wa Kamusi ya Ukristo Padre Jordan Nyenyembe
pamoja na wadau wengine waliohusika katika kufanikisha uandishi wa
Kamusi hiyo.
Pongezi
hizo zimetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Kaimu Mkurugenzi Idara ya
Maendeleo ya Utamaduni katika Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na
Michezo, Bibi. Lily Beleko ambaye alimwakilisha mgeni rasmi Mhe. Waziri
Nape Nnauye wakati wa Hafla ya Uzinduzi wa Kamusi hiyo.
Akisoma
hotuba kwa niaba ya Mhe. Waziri Nape Nnauye, Bibi. Beleko amesema
kwamba Padre Jordan Nyenyembe anapongezwa kwa uandishi wa Kamusi hiyo
kwani kunaonyesha juhudi za kukuza na kuitangaza lugha ya Kiswahili.
Alisema
kwamba uandishi wa Kamusi ni kazi ngumu na endapo maneno ndani ya
Kamusi hayatafsiriwi sawa sawa basi kuna uwezekano wa kusababisha chuki,
ghasia na hata mapigano na hasa maneno yanayohusiana na masuala ya
imani ya dini Fulani.
“Ni
matumaini yangu kwamba, Kamusi hii itahamasisha na kurahisisha uelewa wa
vitabu na maandiko mbalimbali kwa usahihi na ufasaha kwa jamii na
kuleta upendo, utulivu na amani”, alisema Beleko.
Aliongeza
kuwa Wamisionari wa mwanzo wa imani ya kikristo walisaidia katika
usahihishaji na uenezaji wa lugha ya Kiswahili kupitia vitabu na nyaraka
mbalimbali, aidha walishiriki katika kuandika sarufi za Kiswahili,
kamusi za kiswahili na kutafsiri Biblia kutoka lugha moja kwenda lugha
nyingine hali ambayo ilisaidia kukuza dini ya Ukristo na kukuza lugha
ya Kiswahili.
“Lugha
yetu ya Kiswahili kila kukicha inazidi kukua na kupitia Kamusi hii
tunaamini kwamba wasomaji wataongeza maarifa na ufasaha na kudumisha
umoja, amani na uzalendo”, alisema Beleko.
Kwa
upande wake Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC)
Padre Ubadius Kidavuri ambaye aliliwakilisha Baraza hilo alieleza
kwamba, ushirikiano kati ya serikali na taasisi za kidhni ni jhambo
mhimu katika kusukuma maendeleo ya taifa.
“Katika
Kanisa la Katoliki Tanzania linaunga mmkono jitihada zote za Wasomi na
Wataalam wote wanaowezesha ujuzi na maarifa mbalimbali kidini na hata
kielimu kuwafikia Wananchi katika kukabiliana na changamoto, hivyo
nachukua nafasi kwa niaba ya Baraza, kumshukuru na kumpongeza Padre
Jordan kwa jitigada zake za kubuni na kufanya kazi hii njema kwa
Watanzania”, alisema Padre Ubadius.
Naye
Mwandishi wa Kamusi hiyo, Padre Jordan Nyenyembe alisema kwamba Kamusi
hiyo inakamilisha kazi iliyoanza mwaka 2004 kama Makala katika Gazeti la
Kiongozi iliyoitwa ‘Kiswahili cha Mwanakanisa’.
Alisema
kwamba, wasomaji watakaokuwa wanaitumia Kamusi hiyo wawe huru
kumshirikisha kwa kutoa maoni yao mbalimbali ili aweze kuboresha katika
matoleo yajayo.
“Mtakaoisoma Kamusi hii msisite kutoa maoni yenu ambayo yataniwezesha kuboresha katika matoleo yajayo”, alisema Padre Jordan.
Naye
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Uchapishaji Vitabu ya Mkuki na Nyoka, Bw.
Walter Bugoya alieleza kwamba, kuandaa kamusi kama hiyo kunahitaji mtu
kufahamu masuala mengi ambayo anatarajia kuyaandika, hivyo anakuwa na
kazi kubwa ambayo inahitaji umakini, kutafuta maana sahihi ya maneno.
“Pia
katikia suala la uhalili Mwandishi anahitaji kusaidiwa na Wahariri ili
kazi yake iwe rahisi kwa wasomaji kwa kupata maana sahihi ya maneno
ndani ya kitabu husika”, alisema Bw. Bugoya.
Kwa
upande wake Katibu Mtendaji Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) Dkt.
Selemani Sewangi alisema kuwa, suala la lugha kwenye Makanisa ni muhimu
sana kwani litasaidia kukuza uelewa wa mafundisho ya imani ya dini hiyo,
hivyo amepongeza kazi ya uandishi wa Kamusi hiyo.
No comments:
Post a Comment