Matukio : Rais Dk. Magufuli Atoa Msaada wa Bajaj Kwa Mlemavu Thomas Kone - Wazalendo 25 Blog

Breaking

Glory to Story.


Post Top Ad


18 Aug 2016

Matukio : Rais Dk. Magufuli Atoa Msaada wa Bajaj Kwa Mlemavu Thomas Kone

 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Dkt Ayoub Rioba akimlaki Bw. Thomas Kone (35) alipofika ofisi za TBC1 Mikocheni jijini Dar es salam kupokea Bajaji mpya ambayo amezawadiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli baada ya kumuona katika tarifa ya habari ya TBC1 akiwa anatafuta msaada wa usafiri ili aweze kujikimu kimaisha na familia yake ya mke na watoto wawili. Rais aliguswa na kijana huyu na kuamua kumsaidia kwani pamoja na ulemavu wake ameendelea kuchapa kazi bila wasiwasi.
 Kaimu Mnikulu ambaye pia ni Naibu Katibu wa Rais Bw. Ngusa Samike akimlaki Bw. Thomas Kone (35) alipofika ofisi za TBC1 Mikocheni jijini Dar es salam kupokea  Bajaj mpya ambayo amezawadiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli. Anayeshuhudia ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Dkt Ayoub Rioba
 Mgeni akisindikizwa ndani kwa heshima zote ili akapokee Bajaji yake 
  Kaimu Mnikulu ambaye pia ni Naibu Katibu wa Rais Bw. Ngusa Samike akiongea na Bw. Thomas Kone (35) ambaye haamini bahati yake  katika  ofisi za TBC1 Mikocheni jijini Dar es salam kabla ya kumkabidhi  Bajaj mpya ambayo amezawadiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli. Anayeshuhudia ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Dkt Ayoub Rioba
 Bw. Thomas Kone (35) akimshukuru  Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Dkt Ayoub Rioba katika  ofisi za TBC1 Mikocheni jijini Dar es salam baada ya kituo hicho kuwezesha apewe   Bajaj mpya ambayo amezawadiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.
Kaimu Mnikulu ambaye pia ni Naibu Katibu wa Rais Bw. Ngusa Samike akimkabidhi funguo na nyaraka Bw. Thomas Kone (35) kwa ajili ya Bajaji mpya ambayo amezawadiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli baada ya kumuona katika tarifa ya habari ya TBC1 akiwa anatafuta msaada wa usafiri ili aweze kujikimu kimaisha na familia yake ya mke na watoto wawili. Rais aliguswa na kijana huyu na kuamua kumsaidia kwani pamoja na ulemavu wake ameendelea kuchapa kazi bila wasiwasi. Anayeshuhudia ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji TAnzania (TBC) Dkt Ayoub Rioba ambaye mwanahabari wake Mbozi Katala ndiye aliyemtangaza bwana Kone. Hafla hii fupi imafanyika makao makuu ya TBC 1 Mikocheni jijini Dar es salaam leo Agosti 18, 2016
  Bw. Thomas Kone (35) akimshukuru Kaimu Mnikulu ambaye pia ni Naibu Katibu wa Rais Bw. Ngusa Samike bada ya kuipokea   Bajaj mpya ambayo amezawadiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.
  Kaimu Mnikulu ambaye pia ni Naibu Katibu wa Rais Bw. Ngusa Samike na  Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Dkt Ayoub Rioba na watumishi wa kituo hicho wakimwangalia Bw. Thomas Kone (35) akipanda  Bajaji yake mpya ambayo amezawadiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
 Kaimu Mnyikulu ambaye pia ni Naibu Katibu wa Rais Bw. Ngusa Samike na  Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Dkt Ayoub Rioba wakimshuhudia   Bw. Thomas Kone (35)  ndani ya Bajaji yake mpya ambayo amezawadiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
  Kaimu Mnyikulu ambaye pia ni Naibu Katibu wa Rais Bw. Ngusa Samike na  Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Dkt Ayoub Rioba wakiwa na Bw. Thomas Kone (35)  katika Bajaji yake mpya ambayo amezawadiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
 Kaimu Mnikulu ambaye pia ni Naibu Katibu wa Rais Bw. Ngusa Samike akitoa salamu za Rais ambaye aliguswa na kijana huyu na kuamua kumsaidia kwani pamoja na ulemavu wake ameendelea kuchapa kazi bila wasiwasi. Anayeshuhudia ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Dkt Ayoub Rioba ambaye mwanahabari wake Mbozi Katala ndiye aliyemtangaza bwana Kone. Hafla hii fupi imafanyika makao makuu ya TBC 1 Mikocheni jijini Dar es salaam leo Agosti 18, 2016
   Kaimu Mnikulu ambaye pia ni Naibu Katibu wa Rais Bw. Ngusa Samike na  Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Dkt Ayoub Rioba na watumishi wa kituo hicho wakiwakatika picha ya pamoja na Bw. Thomas Kone (35) baada ya kukabidhiwa Bajaji yake mpya ambayo amezawadiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
 Bw. Thomas Kone (35) akimpongeza manahabari wa TBC1  Bw. Mbozi Katala kwa kufanya kazi nzuri kiasi cha kumfanya  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amzawadie Bajaji hiyo  kwani pamoja na ulemavu wake ameendelea kuchapa kazi bila wasiwasi.
  Kaimu Mnikulu ambaye pia ni Naibu Katibu wa Rais Bw. Ngusa Samike akishuhudiwa na  Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Dkt Ayoub Rioba na watumishi wa kituo hicho akimpongeza mwanahabari  Bw. Mbozi Katala aliyeripoti changamoto ya Bw. Thomas Kone (35) kiasi cha kumfanya  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amzawadie Bajaji hiyo  kwani pamoja na ulemavu wake ameendelea kuchapa kazi bila wasiwasi.  PICHA NA IKULU.

Post Top Ad