Kutoka
kulia ni Dk. Zaitun Bokhary na Dk. Yona Ringo wa Hospitali ya Taifa ya
Muhimbili (MNH) wakimfanyia upasuaji mtoto mwenye tatizo kwenye mfumo
wa hewa na chakula LEO kwa kushirikiana na Profesa Saber M. Waheeb
(kushoto) na wenzake kutoka Misri.
Kutoka
kulia ni Dk. Yona Ringo na Dk. Zaitun Bokhary wa Muhimbili wakiendelea
na upasuaji kwa kushirikiana na wataalamu kutoka Misri.
Profesa
Saber M. Waheeb (katikati) akijadiliana jambo na Dk. Zaitun Bokhary
kabla ya kuanza kwa shughuli ya upasuaji kwa watoto wanane LEO. Kutoka
kushoto ni Mwambata wa Jeshi la Wananchi Tanzania, Kanali Salum Haji
Othman nchini Misri na nchi zote za Mashariki ya kati na Dk Yona Ringo
wakifuatilia mazungumzo hayo leo.
Grace
Joel akiwa na watoto wake pacha, Eliudi Joel (katikati) na Elikana
Joel wakisubiri kufanyiwa upasuaji wad njia ya mkono. Awali watoto hao
kutoka Mbeya walizaliwa wakiwa wameungana na baadaye walifanyiwa
upasuaji na kutenganishwa.
Kutoka
kushoto ni Eliudi Joel na Elikana Joel wakiwa katika Hospitali ya Taifa
ya Muhimbili (MNH) wakisubiri kufanyiwa upasuaji leo.
Profesa Dk. Saber M. Waheeb akifanya utafiti mdogo kwa mtoto ambaye amelazwa kwenye Jengo la watoto katika hospitali hiyo.
Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Profesa
Lawrence Museru (kushoto) akimkaribisha Profesa Saber M. Waheeb katika
hospitali hiyo leo.
Profesa
Lawrence Museru (kulia) akizungumza na madaktari na wataalamu wa kada
nyingine leo katika hospitali hiyo kabla ya kuanza kwa shughuli ya
upasuaji.
Kutoka
kushoto ni Mwambata wa Jeshi la Wananchi Tanzania, Kanali Salum Haji
Othman nchini Misri na nchi za Mashariki ya kati akizungumza jambo na
Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Upasuaji, Dk. Julieth Magandi leo wa
hospitali hiyo.
Picha na John Stephen, Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH)
Na John Stephen.
HOSPITALI
ya Taifa ya Muhimbili (MNH) LEO imeanza upasuaji kwa watoto wanane na
wenye matatizo ya njia ya mkojo na mfumo wa hewa na chakula ili kuwa
sawa na watu wengine ambao hawana matatizo hayo.
Madaktari
wa hospitali hiyo wanafanya upasuaji huo kwa kushirikiana na madaktari
kutoka Misri ambao wamewasili leo wakitokea Misri kwa ajili ya kushiriki
shughuli hiyo.
Madaktari
wa Muhimbili ni Dk. Zaitun Bokhary, Dk. Yona Ringo Madaktari, Dk.
Herman Wella, Dk. Victor Ngolta, Dk Mwajabu Mbaga, Dk. Joachim Angela,
Dk. Hashim Lituli na Dk. Gertrud Mollel wakati madaktari na wataalamu
wa kada nyingine kutoka Misri ni Mahamed Malak, Saber Waheeb, Amr Alaa,
Tamer Ghoneim, Ragia Mohamed Awad, Sherouk Saad Ayoub, Hazem Ahmed.
Wataalamu
hao wametembelea watoto waliolazwa kwenye Jengo la Watoto na
kujadiliana na madaktari wa hospitali hiyo jinsi watakavyotoa huduma za
upasuaji kwa watoto hao.
Kwa
mujibu wa Dk Julieth Magandi, watoto wengine sita watafanyiwa upasuaji
huo kesho. Dk Magandi amesema Leo madaktari hao wameanza kwa mtoto
mwenye tatizo la mfumo wa chakula na hewa na kwamba watoto pacha wawili
waliungana na kutenganishwa kutoka Mbeya nao watafanyiwa upasuaji wa
kuweka sawa mfumo wa njia ya mkojo.
Baadhi
ya watoto wanaofanyiwa upasuaji ni; Nasra Rashidi, Hughes Khalid, Fahad
Selemani, Elikana Joel, Eliudi Joel, Hasna Hamis Kalemea, Ibrahim Haji
na Sofia Ramadhani.
No comments:
Post a Comment