Mtakwimu
kutoka Makao Makuu ya Shirika la Afya Duniani (WHO) Geneva,Switzarland
Doris MA FAT (Kulia) akigawa machapisho yenye mwongozo kuhusu namna ya
kujaza taarifa mbalimbali zinazosababisha vifo wakati wa mafunzo ya siku
2 ya wataalam wa Afya kutoka nchi zipatazo 14 za Bara la Afrika leo
jijini Dar es salaam.
Mtaalam
na Mkufunzi wa masuala ya Afya kutoka Makao Makuu ya Shirika la Afya
Duniani (WHO) Geneva - Switzarland, Olau Poppe akitoa mafunzo kwa Timu
ya wataalam wa Afya kutoka nchi zipatazo 14 za Bara la Afrika kuhusu
mfumo wa taarifa unaotumika kutambua sababu za kifo cha mgonjwa kwa
lengo kuwajengea uwezo watalaam kuhusu ujazaji wa taarifa kuhusu sababu ya kifo cha mgonjwa pindi wanapojaza cheti cha kifo (Death Certificate).Washiriki wa Mafunzo hayo ya Siku mbili watakua na jukumu la kutoa mafunzo kwa wataalam wengine kwenye nchi wanazotoka kuhusu mfumo huo.
Mtaalam
na Mkufunzi wa masuala ya Afya kutoka Makao Makuu ya Shirika la Afya
Duniani (WHO) Geneva, Olau Poppe akifuatilia majadiliano ya washiriki wa
mafunzo ya siku 2 ya wataalam wa Afya kutoka nchi zipatazo 14 za Bara
la Afrika kuhusu mfumo unaotumika kutambua sababu ya kifo cha mgonjwa
utakaowasaidia watalaam hao kujaza taarifa sahihi kwenye cheti cha
kifo.
Baadhi ya Washiriki wa mafunzo
kwa Timu ya wataalam wa Afya kutoka Tanzania, Zambia na Cameroon
wakifuatilia miongozo mbalimbali iliyokuwa inatolewa na watalaam kutoka
Makao Makuu ya Shirika la Afya Duniani (WHO) wakati wa Mafunzo kuhusu mfumo wa taarifa unaotumika kutambua sababu za kifo cha mgonjwa kuwawezesha watalaam hao kujaza taarifa sahihi juu ya sababu ya kifo cha mgonjwa leo jijini Dar es salaam.
Sehemu ya Washiriki wa mafunzo
kwa Timu ya wataalam wa Afya kutoka Tanzania na Malawi wakifuatilia
miongozo mbalimbali iliyokuwa inatolewa na watalaam kutoka Makao Makuu
ya Shirika la Afya Duniani (WHO) wakati wa Mafunzo kuhusu mfumo wa taarifa unaotumika kutambua sababu za kifo cha mgonjwa kuwawezesha watalaam hao kujaza taarifa sahihi juu ya sababu ya mwisho ya kifo cha mgonjwa leo jijini Dar es salaam. Picha/Aron Msigwa.
No comments:
Post a Comment