Katibu
Mtendaji wa Mfuko Kichocheo wa Kilimo Nyanda za Juu Kusini (SAGCOT
CTF), John Kyaruzi (kulia), akizungumza na wafugaji wakati wa ufunguzi
wa semina ya siku tano ya kilimo ufugaji wa kibiashara (FAAB)
iliyoandaliwa na SAGCOT CTF, Kiwanda cha Maziwa Njombe kwa kushirikiana
na Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo na Biashara, (UNCTAD)
yenye lengo la kuwafanya wafugaji hao kufuga kibiashara. Semina hiyo
ilifanyika mkoani Njombe jana. Kulia kwake ni Mwenyekiti wa Kamati ya
Uwekezaji ya mfuko huo, Dr Rosebud Kurwijila na Mkurugenzi wa Hamashauri
ya Mji wa Njombe, Iluminata Mwenda.
Mwenyekiti
wa Kamati ya Uwekezaji ya Mfuko Kichocheo wa Kilimo Nyanda za Juu
Kusini (SAGCOT CTF), Dk. Rosebud Kurwijila (kushoto), akifungua semina
ya siku tano ya Kilimo Ufugaji Biashara (FAAB) iliyoandaliwa na SAGCOT
CTF, Kiwanda cha Maziwa Njombe kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa
Mataifa la Maendeleo na Biashara, (UNCTAD) yenye lengo la kuwafanya
wafugaji hao kufuga kibiashara. Semina hiyo ilifanyika mkoani Njombe
jana. Kulia ni Katibu Mtendaji wa SAGCOT CTF, John Kyaruzi.
Mratibu
wa Biashara wa Mfuko Kichocheo wa Kilimo Nyanda za Juu Kusini (SAGCOT
CTF), Abdala Msambachi akitoa elimu kwa wafugaji wa ng’ombe wa maziwa
mkoani Njombe jana ili kufanya ufugaji wa wa kisasa utakaoinua uchumi
wakati wa semina ya siku tano ya Kilimo Ufugaji Biashara (FAAB)
iliyoandaliwa na SAGCOT CTF, Kiwanda cha Maziwa Njombe kwa
kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo na Biashara,
(UNCTAD).
Mkurugenzi
wa Halmashauri ya Mji wa Njombe, Iluminata Mwenda (kushoto),
akizungumza na wafugaji wa halmashauri yake waliohudhuria semina ya
siku tano kuhusu Kilimo Ufugaji Biashara (FAAB) iliyoandaliwa na Mfuko
Kichocheo wa Kilimo Nyanda za Juu Kusini (SAGCOT CTF), Kiwanda cha
Maziwa Njombe kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la
Maendeleo na Biashara, (UNCTAD). Kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Kamati
ya Uwekezaji ya SAGCOT CTF, Dk. Rosebud Kurwijila na Katibu Mtendaji wa
mfuko, John Kyaruzi.
Baadhi ya wafugaji wakifanya wakijadiliana wakati wa semina ya wafugaji
inayolenga kuwainua kiuchumi wafugaji wa ng’ombe wa maziwa mkoani
Njombe iliyoandaliwa na Mfuko wa SAGCOT CTF.
Na Mwandishi wetu Njombe
WAFUGAJI
wa ng’ombe mkoani Njombe wamepewa changamoto kufanya ufugaji kilimo
kibiashara ili kuongeza uzalishaji na ubora wa maziwa utakaoweza kuinua
kipato chao imeelezwa mkoani humo jana.
Wito
huo umetolewa na Mwenyekiti wa Kamati ya Uwekezaji ya Mfuko Kichocheo wa
Kilimo Nyanda za Juu Kusini (SAGCOT CTF), Dr Rosebud Kurwijila, wakati
akizungumza na baadhi ya wafugaji wa mkoa huo kwenye semina ya siku tano
ya Kilimo Ufugaji Biashara (FAAB) iliyoandaliwa na SAGCOT CTF kwa
kushirikiana na Kiwanda cha Maziwa Njombe pamoja na Shirika la Umoja wa
Mataifa la Maendeleo na Biashara, (UNCTAD ikiwa na lengo la kuinua
kipato kutokana na ufugaji wa ng’ombe wa maziwa kibiashara.
Alisema
hii ni semina ya nne kutolewa nchini Tanzania kwa uratibu wa Mfuko wa
SAGCOT CTF na UNCTAD mara ya kwanza ikiwa ni mkoani Tanga 2015 mafunzo
yakitolewa kwa awamu tatu yakiwa na madhumuni ya kuwafanya wafugaji
wakulima wanaondokana na kilimo cha kujikimu.
“Mfuko
Kichocheo wa SAGCOT CTF unatoa ufadhili kwa wafugaji hao kupitia
kiwanda cha kusindika maziwa cha Njombe ambapo mfuko ulifanya utafiti wa
kujua nini mfugaji anahitaji kuinuka kiuchumi,” alisema.
Akizungumza
wakati wa ufunguzi wa semina hiyo, Katibu Mtendaji wa Mfuko Kichocheo
wa SAGCOT CTF, John Kyaruzi amesema kuwa sasa ni wakati wa wafugaji
kutajirika kutokana na ufugaji na ndio maana ufadhili wa elimu hiyo
utasaidia wafugaji kufuga kibiashara ambapo mahitaji makubwa ni kupata
ng’ombe mwenye uwezo wa kutoa maziwa kwa wingi.
“Wafugaji
wengi wapo vizuri katika hatua ya kulisha mifugo yao lakini
wanachokikosa ni elimu ya uchaguzi wa ng’ombe wazuri wa maziwa na hivyo
Mfuko Kichocheo wa SAGCOT CTF hautatoa mkopo wa pesa pekee kwa wakulima
bali kuwawezesha kutoka na kile mfugaji atakacho,” alisema.
Katibu
Mtendaji huyo wa SAGCOT CTF aliongeza kuwa elimu hiyo ni muhimu kwani
itasaidia wakulima wafugaji kutambua kuwa kilimo ni biashara huku pia
wakipewa mbinu ya kupunguza gharama katika ufugaji wa ngo’mbe wa maziwa
kibiashara na kwa matumizi yao hivyo kukuza uchumi wa mkulima mmoja
mmoja, jamii na pia kujenga afya zao kutokana na kutumia maziwa bora.
Naye
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Njombe, Iluminata Mwenda alisema
kuwa wafugaji hao watumie vizuri fursa hiyo kwa kuwa wanaletewa elimu ya
kuwa na uchumi mzuri na kuwa wafugaji wakifanya vizuri halmashauri nayo
itaongeza kipato chake kwa kuwa na kiwanda cha maziwa kinachozalisha
kwa wingi.
Nao
baadhi ya wafugaji wameishukuru SAGCOT CTF, UNCTAD pamoja na washirika
wengine waliofanikisha semina hiyo kwani kupitia mafunzo hayo wanaweza
kuwa ufugaji wenye tija kwa ajili ya kuinua kipato na kuboresha afya
zao.
Mfuko
wa SAGCOT CTF ulianzishwa Mei 2011 chini ya sheria ya wadhamini ya Mwaka
2002 chini ya Mpango Shirikishi wa Uchumi nchini (PPP), kuchochea
maendeleo katika sekta ya kilimo nchini. Katika kufikia malengo mfuko
ulitafuta wabia muhimu kufikia azma hiyo hivyo Shirika la UNCTAD ni
mshirika wake katika kutoa utaalamu elekezi. (technical assistance).
No comments:
Post a Comment