Maxence M. Melo wa Jamii Forum akiwa katika picha na Mtendaji mkuu wa Csema , Kiiga Joel. Maxence M. Melo wa Jamii Forum akiwa katika picha na Mtendaji mkuu wa Csema , Kiiga Joel Mmoja ya watoto wakiwa katika michezo.
JAMII
imetakiwa kubadilika kwa kuacha kufanya ukatili wa watoto ili kuweza
kuwa na watoto kwa kujitambua. Hayo ameyasema leo Mkugenzi Mtendaji wa
Taasisi isiyo ya Kiserikali C-SEMA, Kiiya Joel, wakati wa maadhimisho ya
siku mtoto wa Afrika iliyofanyika katika viwanja vya Jakaya Kikwete,
amesema kesi nyingi za watoto kutelekezwa ambazo zimekuwa zikifikia
kituomn hicho kupitia huduma ya simu mkononi. Kiiya amesema watoto
wanatelekezwa na kufanya watoto kuishi mitaani na kuhitaji msaada wa
kujikimu hali ambayo inafanya watoto kukosa haki ikiwemo kukosa elimu.
Amesema
kuwa katika utoaji wa huduma ya simu C-SEMA imejipanga kuboresha huduma
visiwani Zanzibar ili kuhakikisha vitendo viovu vya watoto vinapatiwa
taarifa. "Tumepata fedha ambazo C sema itaboresha huduma kupiga ya simu
kwa ajili ya kupata matukio ambayo yanakandamiza watoto visiwani
Zanzibar ", amesema Kiiya. Kiiya amewataka watanzania kutoa ushirikiano
kwa kupiga simu ya bure 116 na kutoa taarifa za matukio ya ukatili dhidi
ya watoto ili yaweze kutatuliwa mara moja.
Watoto katika picha ya Pamoja .
Amesema
kuwa kituo cha huduma ya simu kwa mtoto kimekuwa hakipokei simu nyingi
kutokana na kwamba huduma hiyo haijafahamika maeneo mengi ambapo kwa
mwezi hupokea simu 30 kiwango ambacho ni kidogo kulingana na ukubwa wa
tatizo. "Naomba watanzania wote popote pale walipo kupiga simu ya bure
116 pale wanaposikia taarifa za kuwepo kwa matukio ya ukatili dhidi ya
watoto ili yaweze kufanyiwa kazi," amesema Amesema kuwa toka kituo hicho
kianze Juni 16, mwaka 2013 wamekuwa wakipokea simu za matukio ya watoto
kupewa ujauzito, matunzo ya watoto baada ya kutekelezwa, ulawiti na
ubakaji.
Aliongeza
kuwa wameamua kuadhimisha siku hiyo kwa kukutanisha watoto kutoka
maeneo mbalimbali ikiwa pia ni sehemu ya kuanzishwa kwa huduma hiyo.
Amesema C-Sema inataka kuona huduma za watoto nchini zinalenga maslahi
ya mtoto na ndio maana kwa kushirikiana na serikali C-Sema imekuwa
ikikusanya maoni ya watoto nchi nzima kupitia Huduma ya Simu kwa Mtoto
(116), Barua za Maoni ya Watoto, na gazeti la Sema kwa ajili ya watoto.
Watoto katika michezo mbalimbali.
Amesema
maoni haya hutumiwa na viongozi wa Manispaa katika kuongeza bajeti ya
watoto ili kuboresha huduma za watoto kwa kupiga simu hiyo ya bure. Siku
ya Mtoto wa Afrika uadhimishwa kila mwaka ifikapo Juni 16 na kwa hapa
nchini kauli mbiu ya mwaka huu ni 'ubakaji na ulawiti kwa mtoto
vinaepukika chukua hatua.
Watoto wakiangalia mpira. Baadhi ya watoto wakiwa uwanjani. Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
No comments:
Post a Comment