Mkuu
wa Idara ya Ujirani Mwema katika Hifadhi ya Taifa ya Mlima ya
Mahale,Mhifadhi Romanus Mkonda akizungumza juu ya ujenzi wa madaraja
ulioanza katika barabara ya kuelekea katika hifadhi hiyo.
Wanahabari
wakimsilikiliza Mhandisi kutoka kampuni ya ujenzi ya Lilangela
inayojenga daraja la Lagosa katika barabara ya Buhingu wilayani Uvinza
,Marango Ngose alipokuwa akizungumzia juu ya ujenzi huo unaofadhiliwa na
Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA).
Kibao kinachoonesha taarifa mbalimbali juu ya ujenzi wa daraja hilo.
Baadhi ya mafundi wakijaribu kuchimba udongo katika eneo la mto Lagosa ambako daraja hilo linajengwa.
Baadhi ya malighafi zinazotumika kwa ajili ya ujenzi wa daraja hilo zikiwa eneo la ujenzi.
Kukamilika
kwa ujenzi wa daraja hili kuta tatua changamoto ya wananchi katka
vijiji hivyo kuvuka kwenda upande mwingine ambako kwa sasa wamekuwa
wakilazimika kuvuka katikati ya mto huku wakiwa wamebeba vyombo vyao vya
usafiri na hata mifugo imekua ikipita katika mto huo.
Ari
kadharika kina mama na watoto kwa sasa wamekua wakilazimika kwenda
kupata huduma ya maji upande wa pili wa mto huo na kwamba wanalazimika
pia kupita ndani ya mto huo ili kuvuka kwenda katika makazi yao.
Meneja
Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Pascal Shelutete
akiwa ameongozana na wanahabari wakitoka katika eneo kunako jengwa
daraja hilo.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii aliyeko Kigoma.
SHIRIKA la Hifadhi za Taifa (TANAPA) limetoa Sh. Milioni 584 kwa ajili ya ujenzi wa madaraja mawili ikiwa ni njia
moja
ya kutatua changamoto ya miundombinu ya barabara katika vijiji
vinavyopakana na Hifadhi ya Taifa Milima ya Mahale vilivyopo wilaya ya
Uvinza mkoani Kigoma.
Baadhi
ya wananchi wanaoishi katika vijiji vya Lukoma na Igalula wanakabiliwa
na changamoto ya barabara jambo linalowafanya washindwe kufanya
shughuli zao za kimaendeleo.
Akizungumza
na waandishi wa habari waliotembelea vijiji hivyo vilivyoko mwambao mwa
zimwa Tanganyika ,Mkuu wa idara ya ujirani mwema ,Mhifadhi Romanus
Mkonda aliyataja madaraja hayo kuwa Lagosa na Lukoma.
“Daraja la Lagosa linatumia Sh. Milioni 296 wakati lile la Lukoma litatumia Sh. Milioni 288,” alisema.
Alisema
lengo la TANAPA ni kusaidia jitihada za serikali za
kuimarisha mawasiliano ya barabara katika ukanda huo kwa ajili ya
kuwawezesha wananchi kiuchumi.
“Iwapo
barabara hiyo itapitika itarahisisha usafiri na usafirishaji kwa
wananchi wa ukanda huu na pia Hifadhi yetu itaweza kupata watalii
wengi kwa sababu usafiri uliopo sasa hivi ni wa maji na Ndege pekee,”
alisema.
Hata
hivyo, alisema iwapo miundombinu hiyo ya barabara itakamilika itaepusha
gharama kubwa ambazo Hifadhi inaingia kwa ajili ya kwenda mjini kununua
vitu mbalimbali vya hifadhini.
Aliongeza
kuwa barabara hiyo itawasaidia wananchi hao kupata huduma mbalimbali
zinazopatikana nje ya eneo lao ikiwa ni pamoja na kusafirisha mazao na
kuyapeleka masoko ya nje.
“Kwa
mfano tunapotaka kwenda mjini tunatumia Boti ambalo linatumia Lita 1000
za petroli kwenda na kurudi na oil lita 40...hivyo iwapo barabara
zitakamilika gharama hizi zitapungua,” alisema.
Pia, alisema barabara hizo zikikamilika utalii utaongezeka na kuliongezea taifa pato.
Aliongeza
kuwa kwa mwaka wa fedha 2016/17, TANAPA imetenga Sh. Milioni 500 kwa
ajili ya kujenga madaraja ya Nkonkwa na Igalula yaliyopo vijijini hapo.
Naye
mwenyekiti wa kijiji cha Igalula, Mussa Matililo alisema iwapo madaraja
hao yatakamilika itawarahisishia wananchi wa maeneo hayo katika
shughuli zao za kilimo.
“Pia,
itarahisisha mawasiliano ya kijiji kimoja kwenda kijiji kingine kwa
sababu kwa sasa mawasiliano yamekuwa magumu kutokana nah ii mito
miwili,” alisema.
No comments:
Post a Comment