Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye. akiwa katika mkao
wa kusafisha kichwa unaojulikana kwa lugha ya Yoga "KAPALABHATI". Faifa
za mkao huu ni pamoja na kusafisha njia za kupumulia na kuponya kukohoa,
kutibu mafua, pumu na maambukizi kwa njiaya kupumua. Hali kadhalika
unaufanya mwili kuchangamka na kuipa sura nuru na ujana na pia
kustawisha mfumo wa neva na kuboresha mfumo wa kusaga chakula. Wazi
Nape, ambaye alifuatana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, aliongoza
mamia ya wakazi wa jiji katika kuadhimisha Siku ya YogaDuniani kwenye
ufukwe wa Coco Juni 19, 2016. (PICHA NA K-VIS MEDIA/KHALFAN SAID)
Mkao wa kusafisha kichwa (Kapalabhati)
Mkao wa kufikiri kwa uzingativu au kama ujulinavyo "Dhyana"
Mkao
unaosaidia mwili kuwa imara au kama unavyojulikana "Tadasana". Kutoka
kushoto ni Wazir Nape, Balozi wa India nchini Tanzania, Sandeep Arya na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul makonda.
Umbo lapembe tatu au Trikonasana
Mkao
wa radi, ujulikanao kwa lugha ya Yoga, Vajrasana, hii inachukuliwa kama
mkao wa Tahajudi, wakati mtu anafanya mazoezi kwa ajili ya tahajudi,
anatakiwa kufumba macho mwisho wa mazoezi
Yoga
ikiendelea, kutoka kulia kwenda kushoto, ni aliyekuwa Balozi wa
Tanzania nchini Uingereza, Peter Kalaghe, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,
Paul Makonda, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape
Nnauye, Balozi wa India nchiniTanzania Sandeep Arya, na Balozi Mbelwa Kairuki
Mkao wa Kapalabhati, mkao wa kusafisha kichwa
Kupoza mwili kwa kudhibiti pumzi, kwa lugha ya Yoga "Sitali Pranayama"
Mkao wa mwili mfu kwa lugha ya Yoga, Savasana, mkao huu unasaidia kupunguza kila aina ya misukosuko na kutuliza mwili na akili.
Mkao
wa Nzige, au kwa lugha ya Yoga "Salabhasana" mkao huu unasaidia kwenye
matatizo ya viungo na maumivu ya chini ya mgongo, hulainisha misuli ya
mapaja, na hips na kwenye maeneo ya figo. Pia hupunguza mafuta kwenye
mapaja na makalio, ni mazoezi mazuri katika kupunguza uzito ikiwa ni
pamoja na kusaidia viungo vya tumbo kusaga chakula
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Benki M, Allan Msalilwa (Mbele), akiwa miongoni
mwa wananchi waliojitokeza kwenye mazoeziya Yoga Coco Beach. Benki M ndio mfadhili
mkuu wa mazoezi hayo
Waziri Nape katika mkao wa "Tadasana", unaosaidia mwili kuwa imara au
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda katika mkao wa "Tadasana", unaosaidia mwili kuwa imara au
Mkao
wa Mti, au kwa jina la Yoga "Vrikshasana" mkao huu unaboresha ufanisi
wa misuli na mishipa ya fahamu, pia huimarisha mwili, ustahamilifu na
umakini, unaboresha misuli ya miguu na tishu zinazounganisha viungo.
Ma MCs katika mkao wa Bhadrasana (Muafaka/Mzuri)
Mkao
wa Sungura, kwalugha ya Yoga, "Sasankasana", mkao huu unasaidia
kupunguza msongo wa mawazo, hasira na mengineyo, unafungua viungo vya
uzazi, unasaidia kupata choo, na kutuliza maumizu ya mgongo
Mkao
wa Pumzi Nyuki au kwa lugha ya Yoga, "Bhramari Pranayam", mkao huu una
faida ya kupunguza msongo wa mawazo, na unasaidia kutoa wasiwasi, hofu,
hasira na kuleta utulivu wa akili. Faida ya kutoa mlio kama wa Nyuki
inasaidia kutuliza akili na mfumo wa neva, lakini pia ni mkao mzuri kwa
kuleta utulivu kwa ujumla na kuepusha madhara ya msongo wa mawazo
No comments:
Post a Comment