KAMPUNI
ya Nexgen inayojishughulisha na utetezi wa Haki za watoto hapa nchini
wamewapokea wanafunzi 21 wa shule ya All Saints Anglican ya nchini ya
Australia.
Akizungumza na waandishi wa habari, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni
ya Nexgen, Jacob Kahemele mara baada ya kuwapokea wanafunzi 21, wazazi
wawili na walimu wawili wa shule ya All Saints Anglican ya nchini ya
Australia amesema kuwa wamekuja kwaajili ya kutoa mafunzo mbalimbali
kwaajili ya kumkinga mtoto wa kike ili aweze kuwa salama na kubaki
salama.
Amesema kuwa nchi ya Australia ndio nchini inayoongoza katika
kumlinda mtoto na kuepukana na matatizo mbalimbali yanayomkumba mtoto wa
kike hasa matatizo ya kubakwa kutokana na kesi nyingi kujitokeza hapa
nchini Pia amewaasa viongozi wa nchi waongeze nguvu juu ya kumlinda
mtoto.
Kahemele amesema kuwa viongozi wa siasa waachane kuzungumza vitu
visivyo vya msingi bungeni na adala yake waanze kufikilia juu ya
kumlinda mtoto hasa wa kike ili kuepukana na matatizo mbalimbali
yanayomkumba.
Mkurugenzi
Mtendaji wa kampuni ya Nexgen, Jacob Kahemele akizungumza na waandishi
wa habari mara baada ya wanafunzi wa shule ya All Saints Anglican
kuwasili katika uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es
Salaam. Amesema kuwa wanafunzi hao wamekuja hapa nchini kwaajili ya
kusaidi na kuhamasisha jamii kuzuia na kupambana juu ya usala wa mtoto
katika maisha yake ya utoto.
Mwalimu wa shule ya All Saints Anglican ya nchini Australia, Blendan
Collaghan akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam mala
baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere
jijini Dar es Salaam jana.
Wanafunzi wa Shule ya msingi ya Fountain Gate Academy wakiwapokewa
na kuwafunga skafu za bendera ya Taifa wanafunzi wa shule ya All Saints
Anglican ya nchini ya Australia walipowasili katika uwanja wa ndege wa
Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam jana.
Wanafunzi wa Shule ya msingi ya Fountain Gate Academy wakiwa na
wanafunzi wa shule ya All Saints Anglican ya nchini ya Australia
walipowasili katika uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere jijini
Dar es Salaam jana.
Wanafunzi wa shule ya msingi ya Internation ya Fontain gate
Academy iliyopo Tabata jijini Dar es Salaam wakiwapokea wanafunzi wa
shule ya wanafunzi wa shule ya All Saints Anglican ya nchini ya nchini
Australia katika uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es
Salaam jana .
Wanafunzi wa shule ya All Saints Anglican ya nchini Australia
wakisaidiwa mizigo yao na Wanafunzi wa shule ya msingi ya Internation ya
Fontain gate Academy iliyopo Tabata jijini Dar es Salaam mara baada
yakuwasili katika uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar
es Salaam jana.
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Nexgen, Jacob Kahemele
akifurahiya jambo mara baada ya wanafunzi wa shule ya wanafunzi wa shule
ya All Saints Anglican ya nchini ya nchini Australia waliowasili katika
uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam jana.
Mwanafunzi wa shule ya msingi ya Internation ya Fontain gate
Academy akizungumza na wanafunzi wa shule ya wanafunzi wa shule ya All
Saints Anglican ya nchini ya nchini Australia waliowasili katika uwanja
wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam jana.
Wanafunzi wa shule ya All Saints Anglican ya nchini Australia
wakiwasili katika uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar
es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Nexgen, Jacob Kahemele
akizungumza jambo na walimu wa shule ya All Saints Anglican ya nchini
Australia mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa ndege wa Mwalimu
Julius Nyerere jijini Dar es Salaam jana.
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Nexgen, Jacob Kahemele (Wa pili
kutoka kulia)akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa shule ya All
Saints Anglican ya nchini Australia na Mwanafunzi wa shule ya msingi
ya Internation ya Fontain gate Academy katika uwanja wa ndege wa Mwalimu
Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment