Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amosi Makala (Katikati)akizungumza na viongozi wa benki kuu ya Tanzania (BOT)tawi la Mbeya,kulia Mkurugenzi wa benki kuu ya Tanzania (BOT)tawi la Mbeya Jovent Rushaka na Meneja Utawala na fedha Bakali Ally kushoto katika mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa mikutano benki kuu ya Tanzania (BOT)tawi la Mbeya ,June 28 -2016. |
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amosi Makalla akizungumza na viongozi na wafanyakazi wa benki kuu ya Tanzania (BOT)tawi la Mbeya mara baada ya kufanya ziara katika kwa engo la kujitabulisha . |
Baadhi ya viongozi wa benki hiyo wakimsikiliza kwa makini Mkuu huyo wa Mkoa wa Mbeya Amosi Makalla mara baada ya kufanya ziara katika benki hiyo June 28 mwaka huu. |
Baadhi ya viongozi wa benki hiyo wakiwa makini katika mkutano huo. |
Mgeni rasmi katika picha ya Pamoja na viongozi na wafanyakazi wa benki hiyo. |
Na EmanuelMadafa, JamiiMojablogu Mbeya
SERIKALI MKOANI Mbeya imeitaka benki kuu ya Tanzania (BOT)tawi la Mbeya kufanya
utatifi juu ya kuwepo kwa ununuzi wa mazao kwa wakulima mapema kabla ya
kuanza kukomaa hususani mazao ya ndinzi hasa katika halmsahuri ya
wilaya ya Rungwe Mkoani humo.
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amosi Makalla wakati akizungumza na wafanyakazi
wa benki Kuu Tanzania (BOT)tawi la Mbeya mara baada ya kufanya ziara
katika benki hiyo yenye lengo la kujitambulisha.
Amesema kwa muda mrefu sasa wakulima
wa mkoa huo wamekuwa wakinyonywa na baadhi ya wafanyabiashara ambao
wamekuwa wakinunua mazao mapema yakiwa shambani na kupangia bei ya chini
ambayo haiendani na bei hali ya sokoni .
Amesema nivema benki hiyo ikajaribu kulifanyia utatiti suala hilo ili kuona kama mfumo huo unaweza kuleta tija kwa mkulima kwani benki hiyo inanafasi nzuri ya kuisaidia serikali katika uchocheaji wa ukuaji wa uchumi.
Amesema
lengo la serikali ni kuwalinda wananchi wake sanjali na kuwaondolea
umaskini hivyo lazima ifanyike kila aina ya jitihada katika kufanikisha
suala hilo.
Wakati huo huo Mkuu huyo wa Mkoa wa mbeya Amosi Makalla ameipongeza benki hiyo kwa kuweka jitihada za makusudi katika kudhibiti mfumuko wa bei nchini.
Amesema
kama mfumuko wa bei utashindwa kudhibitiwa tafsiri halisi ya kukua kwa
uchumi haitakuwa na maana yeyote kwa mwananchi wa kawaida hivyo lazima
benki hiyo ikaongeza jitihada zaidi katika kudhibiti hali hiyo.
Kwa upande Mkurugenzi wa benki kuu ya Tanzania( BOT)tawi la Mbeya Ndugu Juvent Rushaka amesema benki hiyo iko tayari kufanya utafiti suala lolote la kiuchumi.
Aidha Mkurugenzi huyo ameelezea changamoto mbalimbali ambazo tawi hilo linakutana nazo likiwemo suala la kutopata takwimu mbalimbali kwa usahihi na kwa wakati.
Amesema
changamoto nyingine ni miundombinu ya kiusalama ya majanga ya moto kwa
kipindi kirefu sasa kwa ukosefu wa maji katika bomba la kuzimia moto
hali ambayo ni hatarishi endapo litatokea janga la moto katika twi hilo.
No comments:
Post a Comment