Matukio : Hakuna Mwananchi yeyote wa Nainokanoka, Ngorongoro Atakayehamishwa - Daudi Felix Ntibenda - Wazalendo 25 Blog

Breaking

Glory to Story.


Post Top Ad


26 Jun 2016

Matukio : Hakuna Mwananchi yeyote wa Nainokanoka, Ngorongoro Atakayehamishwa - Daudi Felix Ntibenda


Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Daudi Felix Ntibenda,akizungumza na wananchi wa kata ya Naikanoka(hawapo pichani)Wilayani Ngorongoro, pembeni yake ni Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro,Hashimu Mgandilwa.

Daudi Ntibenda aliwatoa hofu wananchi wa kata hiyo baada yakuenea uvumi wakutaka kuhamishwa kutoka maeneo ya hifadhi ya Ngorongoro.

"Hakuna mwananchi yoyote atakae hamishwa kutoka eneo hili la hifadhi,kwasababu serikali haiwezi kuhamisha watu wake kwani na nyie niwatanzania mnahaki yakuishi hapa,"alisema Ntibenda.

Aliwasisitiza wananchi waendelee kushirikiana na mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro kwasababu na yenyewe ni sehemu ya serikali na imefanya mambo mengi kwa wananchi wanaoishi maeneo ya hifadhi hiyo pamoja na kuwasogezea chakula karibu.

Pia aliwapongeza wananchi wa kata ya Naikanoka kwakuitunza  vizuri hifadhi ya Ngorongoro bila kuingiza mifugo yao katika bonde la hifadhi ya Ngorongoro(Creater),nakuwaomba waendelee hivyohivyo kwasababu bonde hilo ni moja ya vivutio vya utalii vya mkoa wa Arusha.

 
Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro, Hashimu Mgandilwa,akizungumza na wananchi wa kata ya Naikanoka wilayani Ngorongoro(hawapo pichani),alipofanya zaira katika kata hiyo akiambatana na Mkuu wa Mkoa wa Arusha.

Hashimu aliwapiga marufuku matumizi ya pikipiki pasipo na ulazima ili kuepuka madhara ambayo wanaweza kuyapata ikiwemo kukutana na wanyama wakari na wakahatarisha maisha yao.

"Matumizi ya pikipiki yawepo pale inapobidi hasa kubeba wagonjwa wa haraka,lakini nivizuri wananchi wakatumia magari ya kanda,"alisema Mgandilwa.

Aliwasisitiza pia wananchi wa  kata ya Naikanoka wachimbe vyoo ili wajikinge na magonjwa ya mlipuka ikiwepo kipindupindu kwani kwa sasa wanatumia vyoo vya porini(usero).

Aidha aliwahasa wananchi hao kupuuzia baadhi ya wanaharakati na NGO's zilizopo wilayani hapo zinazoleta uchochezo wa mambo mbalimbali ikiwemo uvumi wa wananchi hao kutaka kuhamishwa,alisema wanakuwa hawana nia njema yakuleta maendeleo bali wanataka kujipatia fedha kutoka kwa wafadhiri wao.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Daudi Ntibenda akiwa pamoja na viongozi mbalimbali wa wilaya ya Ngorongoro katika ziara yake ya wilayani humo.

Baadhi wa wananchi wa kata ya Naikanoka waliofika katika mkutano wao na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, katika viwanja vya shule ya Naikanoka.

Post Top Ad