Mamia kwa maelfu ya mashabiki walijitokezasiku ya Jumatano kumzika mwanamuziki mkongwe wa DRC, Papa Wemba.
Wemba,
aliyezaliwa kwa jina la Jules Shungu Wembadio Pene Kikumba huko Lubefu
enzi za utawala wa Wabelgiji, alianguka na kupoteza maisha wakati
alipokuwa akitumbuiza jukwaani kwenye tamasha nchini Ivory Coast, April
24. Alikuwa na miaka 67.
Mwili wake uliagwa kwa siku tatu kwenye jengo la bunge la nchini hiyo mjini Kinshasa.
Makumi kwa
maelfu pia walikusanyika mtaani mbele ya kanisa la Notre Dame du Congo
Cathedral ambako misa ya mazishi ilifanyika. “Papa Wemba siku zote
amekuwa idol wangu,” alisema JB Mpiana, kiongozi wa kundi la Wenge
Musica.
No comments:
Post a Comment