Mkurugenzi
Mkuu wa Baraza la uwezeshaji wa wananchi kiuchumi (NEEC), Bang'i Issa
akizungumza wakati wa kufungua masomo ya vijana walioshinda kurishiriki
shindano la Ajira yangu Business plan Competition jjini Dar es Salaam
leo.
Mkufunzi
mkuu wa maswala ya ujasiliamali, Tobias Swai akiwapongeza washindi 50
wa shindano la Ajira Yangu Business Plan Compitition jijini Dar es
Salaam leo.
Mwakirishi
kutoka shirika la kazi (ILO), Geras Shirove akizungumza na washindi wa
shindano la Ajira yangu jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi
ya washiriki wa shindano la Ajira yangu waliohudhulia katika shindano
hilo wakiwa kwenye mkutano leo jijini Dar es Salaam.
Na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.
WASHIRIKI
wa shindano la kibiashara la Ajira yangu Business plan Competition
wameaswa kutumia vyema fursa waliyoipata ya kupata mafunzo kwani
yanaweza kubadili mitazamo yao ya kimaisha hususani katika masuala ya
kujiajiri badala ya kuwa na fikra za kuajiliwa.
Hayo
yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la uwezeshaji wa wananchi
kiuchumi (NEEC), Bang'i Issa wakati akizungumza na washirikibwa shindano
la Ajira yangu Business plan Competition jiji Daf es Salaam leo.
Amesema kuwa watumie fursa hiyo kwani wao ni washindi wa awamu ya kwanza
na kuwa kwenye 50 bora kati ya 831. Ni ushindi mmojawapo.
Bang'i amesema kuwa wazingatie mafunzo watakayoyapata ili wachaguliwe kwe 20 bora na 10 bora.
Pia
amewaasa washiriki wa shindando hilo kuwatumia vizuri wakufunzi pamoja
na mkufunzi mkufunzi mkuu vizuri ili baadae wafanye umakini vizuri
katika kuboresha mà andiko yao na kuyawasilisha kwaajili ya mchunjo.
Nae
mwakilishi kutoka ILO, Geras Shirove amesema kuwa amewapongeza
washiriki 50 wa kiendelea kushindania shindano hilo kwani washiriki wa
shindano hilo walikua 831.
No comments:
Post a Comment