Mfuko wa Maendeleo ya jamii –TASAF-umeanza mkakati maalumu utakaowezesha jamii ya Wahadzabe walioko katika mikoa ya Arusha,Manyara na Singida kuandikishwa katika Mpango wa Kunusuru Kaya maskini unaotekelezwa na mfuko huo nchini kote.
Wakizungumza
wakati wa ziara ya kukagua utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya
maskini unavyotekelezwa katika wilaya ya Karatu mkoani Arusha,viongozi
wa TASAF walioambatana na wadau wa maendeleo walioongozwa na Mkurugenzi
Mkazi wa Benki ya Dunia nchi za Tanzania Bi.Bella Bird,na baadhi ya
maafisa wa benki hiyo kutoka Marekani ,baadhi ya wahadzabe waliomba
kuorodheshwa katika Mpango huo ili waweze kunufaika na huduma zitolewazo
kupitia utaratibu wa kuhawilisha fedha.
“
baadhi ya wananchi wenzetu wameandikishwa kwenye mpango huku wengi wetu
hatujapata fursa hiyo na tumeanza kuona namna wanavyonufaika na huduma
za mpango huo’’ alisisitiza mmoja wa wahadzabe katika kijiji cha
Endamaghan umbali wa kilometa 70 kutoka makao makuu ya wilaya ya Karatu
mkoani Arusha.
Akizungumza
baada ya kutembelea makazi ya wahadzabe Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya
Dunia Bi. Bella Bird amepongeza jitihada zinazochukuliwa na Serikali
kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF- kwa kuweza kuwafikia wananchi
ambao wanakabiliwa na umaskini nchini kote.
‘’Benki
ya Dunia inatambua na kuunga mkono jitihada za serikali ya Tanzania
katika kukabili tatizo la umaskini miongoni mwa wananchi wake,umuhimu
mkubwa pia unapaswa kuwekwa katika kunusuru jamii za watu walioko katika
mazingira magumu wakiwemo wahadzabe” alisisitiza Bi. Bird.
Kwa
upande wake,Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Maendeleo ya
Jamii-TASAF-Bwana Ladsilaus Mwamanga alisema zoezi la kutambua na
kuziandikisha kaya maskini katika jamii ya Wahadzabe lilifanyika. Hata
hivyo alisema zoezi hilo liliathiriwa kwa kiwango kikubwa na mfumo wa
maisha ya jamii hiyo wa kuhamahama kutafuta chakula kwa kuwinda wanyama
na kuokota matunda na asali.
“Hatukuweza
kuwaandikisha wote ingawa kimsingi wanastahili kuingizwa kwenye
Mpango,hii ilitokana na kuhamahama kwa wananchi hao kujitafutia chakula
hususani matunda, asali na mizizi” alisisitiza Bwana mwamanga.
Hata
Mkurugenzi Mtendaji huyo wa TASAF ameahidi kuwa kazi ya kuziandikisha
kaya za walengwa katika jamii hiyo ya wahadzabe na nyingine zenye maisha
ya kuhamahama itafanyika upya na kwa haraka ili waweze kuziingiza
kwenye Mpango wa Kunusuru na Kaya Maskini unaotia mkazo katika kuboresha
maisha ya walengwa hususani kupitia sekta za elimu, afya,lishe na
kukuza kipato kwa kaya za walengwa.
Zifuatazo ni picha za ziara ya viongozi wa TASAF na Wadau wa Maendeleo katika maeneo ya wahadzabe,wilayani Karatu Mkoani Arusha.
Mkurugenzi
Mtendaji wa TASAF,Bw. Ladislaus Mwamanga (aliyevaa Kaunda suti)
akiwasikiliza baadhi ya wananwake wa jamii ya Wahadzabe katika kijiji
cha Endaghan wilayani Karatu mkoani Arusha wakati wa ziara ya wadau wa
maendeleo na TASAF kuona utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini .
Baadhi
ya Wananchi kutoka jamii ya Wahadzabe wakisikiliza hotuba ya Mkurugenzi
Mkazi wa Benki ya Dunia Bi. Bella Bird ( hayupo pichani) alipotembelea
kijiji cha Endamaghan kuona utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya
Maskini kupitia TASAF.
Mmoja
wa wananchi kutoka jamii ya Wahadzabe akieleza jambo kwa viongozi wa
TASAF na Benki ya Dunia waliotembelea kijiji cha Endamaghan wilayani
Karatu mkoani Arusha kukagua utekelezaji wa Mpango wa kunusuru kaya
maskini. Wananchi hao wameomba kuingizwa kwenye Mpango huo ambao
umeorodhesha baadhi yao kutokana na tabia yao ya kuhamahama na hivyo
kuwa vigumu kuwapata.
Mkurugenzi
Mkazi wa Benki ya dunia Bi. Bella Bird (watatu kushoto waliochuchumaa)
akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wakazi wa kijiji cha
Endamaghan ambao ni wahadzabe ambao wameomba kuingizwa kwenye mpango wa
kunusuru kaya .
Wananchi
jamii ya Wahadzabe wakiwa mbele ya nyumba yao katika eneo la Endamaghan
wilaya ya Karatu mkoani Arusha. TASAF inakusudia kuiorodhesha jamii
hiyo katika mpango wa kunusuru kaya maskini.
Mkurugenzi
Mkazi wa Benki ya Dunia Bi. Bella Bird akiwahutubia wakazi wa
Endamaghan katika wilaya ya Karatu mkoani Arusha juu ya utekelezaji wa
Mpango
Mmoja
wa Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini katika kijiji cha
Endamaghan kutoka jamii ya Wahadzabe akipokea fedha za ruzuku kupitia
mpango huo.
Mmoja
wa wananchi jamii ya Wahadzabe katika kijiji cha Endamaghan katika
wilaya ya Karatu mkoani Arusha (aliyevaa bangili) akipokea fedha za
ruzuku kupitia Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unaotekelezwa na TASAF.
Baadhi
ya walengwa wa Mpango wa kunusuru kaya maskini katika kijiji cha
Endamaghan wakiwemo jamii ya Wahadzabe wakisikiliza hotuba ya Mkurugenzi
Mkazi wa Benki ya Dunia Bi. Bella Bird (hayupo pichani) juu ya
utekelezaji wa Mpango huo.
No comments:
Post a Comment