Matukio : Mhe. Samia Suluhu afungua mkutano wa uwasilishaji fedha kwa kaya maskini Afrika na kukabidhi hundi za madawati - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


16 May 2016

Matukio : Mhe. Samia Suluhu afungua mkutano wa uwasilishaji fedha kwa kaya maskini Afrika na kukabidhi hundi za madawati


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Wajumbe wa Mkutano wa kwanza wa Mifuko ya Maendeleo ya Jamii TASAF kuhusu mpango wa Uhawilishaji wa Fedha na kunusuru kaya Masikini kwa Nchi Jumuiya za Afrika uliofunguliwa leo Mei 16, 2016 katika Hoteli ya Ngurudoto Mjini Arusha.
 Washiriki wa Mkutano wa kwanza wa Mifuko ya Maendeleo ya Jamii TASAF kuhusu mpango wa Uhawilishaji wa Fedha na kunusuru kaya masikini kwa Nchi Jumuiya ya Afrika wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, alipokua akifungua mkutano leo Mei 16, 2016 katika Hoteli ya Ngurudoto Mjini Arusha.    
 Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejiment ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angela Kairuki kabla ya kufungua Mkutano wa kwanza wa Mifuko ya Maendeleo ya Jamii TASAF kuhusu mpango wa Uhawilishaji wa Fedha na kunusuru kaya masikini kwa Nchi Jumuiya ya Afrika wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, alipokua akifungua mkutano leo Mei 16, 2016 katika Hoteli ya Ngurudoto Mjini Arusha.                                                 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Mkurugenzi wa Benki ya Dunia anaeshughulikia Nchi za Tanzania, Burundi, Malawi na Somalia Bibi. Bella Bird walipokutana katika ukumbi wa Mikutano wa Ngurudoto Mjini Arusha leo Mei 16, 2016, ambapo Makamu wa Rais alifungua mkutano wa kwanza wa TASAF kuhusu Uhawilishaji wa Fedha na kunusuru kaya masikini kwa Nchi Jumuiya ya Afrika.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akikabidhi Hundi kwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongela  kwa ajili ya kukabiliana na uhaba wa Madawati. Jumla ya Madawati Elfu 16.5 yenye thamani ya Tshs. 1 Bilioni moja zilikabidhiwa kwa Wakuu wa Mikoa inayozunguka Mbuga ya Hifadhi ya Taifa kwa ajili ya kukabiliana na tatizo la Madawati kwenye Shule zote zilizomo katika Wilaya za Mikoa hiyo. Makabidhiano hayo yamefanyika leo Mei 16,2016 katika ukumbi wa Ngurudoto mjini Arusha. Katikati waziri wa Maliasili Utalii Profesa Jumanne Magembe (Picha na OMR)     
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akikabidhi Hundi kwa Mkuu wa Mkoa wa Songwe Mhe. Chiku Galawa kwa ajili ya kukabiliana na uhaba wa Madawati. Jumla ya  Madawati Elfu 16.5 yenye thamani ya Tshs. 1 Bilioni moja zilikabidhiwa kwa Wakuu wa Mikoa inayozunguka Mbuga ya Hifadhi ya Taifa kwa ajili yakukabiliana na tatizo la Madawati kwenye Shule zote zilizomo katika Wilaya za Mikoa hiyo. Makabidhiano hayo yamefanyika leo Mei 16,2016 katika ukumbi wa Ngurudoto mjini Arusha. Katikati ni waziri wa Maliasili Utalii Profesa Jumanne Magembe.
Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amefungua Mkutano wa nchi za Afrika zinazotekeleza Mpango wa Uhawilishaji Fedha kwa kusisitiza kuwa serikali ya Tanzania inatambua umuhimu wa kushirikisha wadau katika mapambano dhidi ya umaskini barani Afrika.

Mheshimiwa Samia amesema licha ya juhudi kubwa kufanywa na mataifa mbalimbali barani Afrika dhidi ya umaskini, tatizo hilo limeendelea kuwakabili wananchi hivyo kuweko kila sababu ya kubuni mbinu thabiti za kutokomeza adui huyo wa ustawi wa wananchi.Amesema kuanzishwa kwa mipango ya uhawilishaji fedha ambayo imeanza kutekelezwa na nchi mbalimbali barani Afrika katika miaka ya karibuni kutasaidia kwa kiwango kikubwa jitihada za kutokomeza umaskini.

Ameto mfano wa Tanzania kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii -TASAF - ambao umepata mafanikio makubwa katika kipindi kifupi tangu kuanza utekelezaji wa Mpango wa Uhawilishaji fedha ambapo hadi sasa zaidi ya kaya maskini Milioni Moja na Laki Moja zimeandikishwa na kuanza kupata ruzuku ya fedha kwa ajili ya kuboresha maisha na mkazo ukiwekwa katika sekta ya elimu, afya na lishe huku kaya husika zikijengewa uwezo wa kukuza shughuli za kiuchumi ili hatimaye ziweze kujitegemea.

Mapema waziri wa nchi ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora mheshimiwa Angellah Kairuki amesema mafanikio makubwa yamepatikana katika utekelezaji wa shughuli za Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF katika utambuzi, uandikishaji na utoaji wa Ruzuku kwa wakati kwa kaya za walengwa nchini kote, na kuwa changamoto chache zilizojitokeza zinafanyiwa kazi ili kuboresha zaidi Mpango huo.

Mkutano huo unaoshirikisha nchi 17 na mashirika mbalimbali ya kimataifa umeitishwa nchini Tanzania kufuatia mafanikio yaliyopatikana katika utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya maskini -PSSN- ambapo pia washiriki hao watapata fursa ya kutembelea kaya za walengwa ili kuona namna wanavyonufaika na huduma za mpango huo.

Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akifungua Mkutano wa Nchi za Afrika Zinazotekeleza Mipango ya Uhawilishaji Fedha katika Hotel ya Ngurdoto, Arusha, Tanzania.
Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya utumishi wa Umma na Utawala Bora Mheshimiwa Angella Kairuki akitoa hotuba ya kumkaribisha Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan kufungua mkutano wa Nchi za Afrika Zinazotekeleza Mipango ya Uhawilishaji Fedha katika Hotel ya Ngurdoto nje kidogo ya jiji la Arusha.
Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia (Tanzania, Kenya Uganda na Burundi) Ms Bella Bird akitoa hotuba katika Mkutano wa Nchi za Afrika Zinazotekeleza Mipango ya Uhawilishaji Fedha katika Hotel ya Ngurdoto nje kidogo ya jiji la Arusha.
Mwenyekiti wa kamati ya uongozi taifa ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF Dr. Florens Turuka akitoa maelezo ya kabla ya ufunguzi wa mkutano wa Nchi za Afrika Zinazotekeleza Mipango ya Uhawilishaji Fedha katika Hotel ya Ngurdoto nje kidogo ya jiji la Arusha.
Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bwana Ladislaus Mwamanga akitoa neno la shukrani baada ya Makamu wa Rais Mhe.Samia Suluhu Hassan kufungua Mkutano wa Nchi za Afrika Zinazotekeleza Mipango ya Uhawilishaji Fedha .
 Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia  (Tanzania, Kenya Uganda na  Burundi) Ms Bella Bird akitoa hotuba katika Mkutano wa Nchi za Afrika Zinazotekeleza Mipango ya Uhawilishaji Fedha katika Hotel ya Ngurdoto nje kidogo ya jiji la Arusha.
 Mwenyekiti wa kamati ya uongozi taifa ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF Dr. Florens Turuka akitoa maelezo ya kabla ya ufunguzi wa mkutano wa Nchi za Afrika Zinazotekeleza Mipango ya Uhawilishaji Fedha katika Hotel ya Ngurdoto nje kidogo ya jiji la Arusha.
 Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bwana  Ladislaus Mwamanga akitoa neno la shukrani baada ya Makamu wa Rais Mhe.Samia Suluhu Hassan kufungua  Mkutano wa Nchi za Afrika Zinazotekeleza Mipango ya Uhawilishaji Fedha .
 Naibu Mwakilishi Mkazi wa UNICEF nchini Tanzania Bwana  Paul Edwards  akihutubia washiriki wa Mkutano wa Nchi za Afrika Zinazotekeleza Mipango ya Uhawilishaji Fedha .
 Baadhi ya washiriki wa Mkutano wa Nchi za Afrika Zinazotekeleza Mipango ya Uhawilishaji Fedha kutoka nchi 17 barani Afrika wakisikiliza hotuba ya ufunguzi  iliyotolewa na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan(hayupo pichani)



 Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF bwana Ladislaus Mwamanga akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari juu ya utekelezaji wa Mpango wa kunusuru Kaya maskini unaotekelezwa na serikali kupitia TASAF .
 Baadhi ya Washiriki wa mkutano wa Nchi za Afrika Zinazotekeleza Mipango ya Uhawilishaji wakiwa katika picha ya pamoja na Mkamu wa Rais Samia Suluhu Hassan(aliyeketi katikati)

 
 Baadhi ya Washiriki wa mkutano wa Nchi za Afrika Zinazotekeleza Mipango ya Uhawilishaji wakiwa katika picha ya pamoja na Mkamu wa Rais Samia Suluhu Hassan(aliyeketi katikati)

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad