Familia ya Ankal Muhidin Issa Michuzi
inapenda kutoa shukrani nyingi sana sana kwa ndugu, jamaa,
majirani, marafiki na wafanyakazi wenzie kwa kujitoa kwa hali na mali katika
wakati huu mgumu wa msiba wa mawanae Maggid (pichani) aliyefariki huko Durban, Afrika
Kusini Jumapili ya wiki iliyopita na
kuzikwa katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es salaam juzi Jumamosi.
Ni vigumu mno kumshukuru mtu mmoja
mmoja kutokana na wingi wenu na kwa jinsi kila mmoja wenu alivyojitoa na
kuonesha upendo wa dhati kabla na baada ya mazishi. Tunaweza kujaza kurasa 200
kama hizi na tusiwe tumehitimisha robo tu ya shukrani zetu kwa kila mmoja wenu.
Hivyo tunaomba radhi kwa yoyote ambaye hatutomtaja, kwani wafadhili wetu nyie mko
wengi mno.
Pamoja na hayo shukrani za kipekee ziwaendee Mheshimiwa
Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na
Mama Janeth Magufuli na familia yao yote, Rais Mstaafu wa awamu ya Nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete na
familia yao yote, Rais Mstaafu wa Awamu
ya Pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi na familia yake yote, Rais Mstafu wa awamu ya
Tatu Mzee Benjamin William Mkapa na Mama Anna Mkapa na familia yao yote, Waziri Mkuu Mstaafu Jaji
Joseph Sinde Warioba na Familia yake yote, Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Allan Kijazi, Katibu Mkuu Ikulu Mhe.
Peter Ilomo, Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu Mhe. Ombeni Sefue pamoja na wafanyakazi wenzie wote wa baba
mfiwa kwa kuwa karibu naye katika wakati wote, na kuhakikisha kuwa kila kitu katika msiba huu kinaenda sawasawa. TUNAWAOMBEA
KWA MOLA AWAPE BARAKA ZAKE ZOTE...
Salamu zingine za kipekee ziwaendee
watumishi wote wa Ubalozi wetu Afrika
kusini mjini Pretoria ambao wakiwa chini ya Brigedia Jenerali Kimaryo na Afisa
wa Ubalozi kaka Awesi walisimamia maswala yote ya kuusafirisha mwili kutoka Durban
kuja Dar es salaam. MOLA AWAONGEZEE PALE MTAPOPUNGUKIWA...
Vile vile shukrani za kipeke ziwaendee
Viongozi na wanachama wa Jumuiya ya Watanzania waishio Durban pamoja na Muslim
Burial Society ya hapo hapo Durban ambao walihakikisha mwili wa marehemu
unahifadhiwa, unakafiniwa na unasafirishwa kwa heshima zote. ALLAH AWAJAALIE KATIKA KILA JAMBO...
Kwa Uongozi wa msikiti wa Maamur
uliopo Upanga Dar es salaam pia familia inatoa shukurani za kipekee kwa yote mliotutendea ikiwa ni
pamoja na mwongozo wa kidini katika wakati wote wa msiba na mazishi.
Tutakuwa watovu wa fadhila endapo
kama hatutatoa shukurani za kipekee kwa magrupu ya WhatsApp yote ambayo
baba mfiwa Ankal ni mwanachama.
Shukurani hizi maalum ziwaendee Ma-Admin na wanachama wa Kariakoo Family Group
(KFG), Dar es salaam Old Friends (DOF), Ma Best Group (MBG), Wanahabari, Tasnia ya Habari,
Uongozi, Siasa na Matukio Mix, The New Team, TSJ Alumni, Zama Zile, The Brain
Team, Jazz Fans, The Kop in Tanzania, LFC Bongo, Uswazi Academia, Tanzania
Bloggers Network (TBN), The Legends Family, SID Tanzania Chapter, Mawasiliano,
Team Michuzi, Amani Kwanza Group, Photojournalists TZ, PPAT Members, P Mamas,
RUBY 15, Warembo wa KA, Mambachoz Group, Ndanshau Group, Empress Group kwa
Fundi Mussa na wengi wengine wote katika Social media wakiongozwa na Jamii Forum na VIJIMAMBO BLOG ya Marekani. TUMEHEMEWA
MNO NA KUFARIJIKA SANA KWA MICHANGO YENU
YA HALI NA MALI. WE ARE HUMBLED. MBARIKIWE SANA, SANA, SANA...
Mwisho, lakini sio kwa umuhimu bali kwa nafasi na mpangilio, tunatoa shukrani za kipekee kwa shirikia la ndege la
Emirates kwa kufanikisha usafiri wa mwili wa marehemu, hali kadhalika kampuni
mahiri ya SWISSPORT kwa kusaidia logostics zote katika Uwanja wa ndege wa
Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es salaam.
HATUNA CHA KUWALIPA ZAIDI YA KUTOA
SHUKURANI NA KUSEMA ASANTE SANA NA KUWAOMBEA KWA MOLA KILA MMOJA WENU AWABARIKI
KATIKA SHUGHULI ZENU ZOTE...
Inna Lillahi wa inna ilaihi raji'un
AMIN!
No comments:
Post a Comment