Shindano
la Mama Shujaa wa Chakula msimu wa tano limeingia katika hatua ya pili
ya kupokea fomu na kuwachuja wakina mama waliotuma maombi ya ushiriki
wao baada ya hatua ya mwanzo ya kugawa fomu hizo kufanyika katika
uzinduzi wa shindano hilo mkoani Mtwara mapema mwaka huu.
Fomu
hizo zimepokelewa leo katika kituo cha mazoezi cha Azura jijini Dar
ambapo timu ya majaji kumi kutoka taasisi mbalimbali walizipitia fomu
hizo katika zoezi litakalochukua takribani wiki nzima hadi kukamilika
kwake.
Kwa
mujibu wa Afisa Miradi kutoka shirika la kimataifa la Oxfam, Kefah
John, alisema kuwa takribani washiriki 3,000 wametuma maombi yao kupitia
fomu hizo ambapo katika hatua ya kwanza watapatikana washiriki 28 ambao
watachujwa na kubakia washiriki 18 watakaopiga kambi mkoani Monduli,
Arusha na hatimaye kumpata mshindi mmoja.
Wakizungumza
na waandishi wa habari, msanii Jacob Stephen JB na mtangazaji wa EFM,
Dina Marios ambao ni mabalozi wa shindano hilo, waliwahamasisha wakina
mama watumie shindano hilo litakalorushwa laivu kupitia kituo cha
televisheni ya ITV ili kujifunza njia mbalimbali za kuboresha uzalishaji
wao ili kukuza kipato cha familia.
Meneja
Utetezi wa Shirika la kimataifa la OXFAM, Eluka Kibona akizungumza neno
la utangulizi wakati wa hafla ya maamuzi ya Fomu za Mama Shujaa wa
Chakula shindano linaloendeshwa na Shirika la Kimataifa la OXFAM kwa
mwaka 2016.
Afisa
Miradi kutoka Shirika la kimataifa la OXFAM Kefah Mbogela akizungumzia
juu ya Shindano la Mama Shujaa wa Chakula, Umiliki wa Ardhi na
Changamoto za ardhi na mitaji ili kujiendeleza.
Katikati
ni aliyekuwa mshiriki wa Shindano la Mama Shujaa wa chakula 2014, Ester
Kulwa akiwahamasisha wakina mama kushiriki katika Shindano la Mama
Shujaa linaloendeshwa na Shirika la Mataifa la OXFAM.
Mwigizaji
Maarufu wa Bongo Movie, Jacob Stephen Jb ambaye pia ni Balozi wa
chakula na kampeni ya Grow iliyo chini ya Shirika la kimataifa la OXFAM
(wa kwanza kulia) akizungumzia jinsi shindano la Mama shujaa wa Chakula
lilivyoweza kuwasaidia akina mama.
Balozi
wa chakula na kampeni ya Grow iliyo chini ya Shirika la kimataifa la
OXFAM, Dina Marios ambaye pia ni mtangazaji wa E-FM Radio akisisiza
akinamama warejee mikoani kulima
Balozi
wa chakula na kampeni ya Grow iliyo chini ya Shirika la kimataifa la
OXFAM ambaye pia ni Fashion Blogger, Shamim Mwasha akiwahamasisha
akinamama kujikita zaidi katika kilimo kwa kuwa kinalipa.
Baadhi
ya waandishi wa habari pamoja na wageni wengine wakiwa katika hafla
hiyo ya maamuzi ya Fomu za Mama Shujaa wa Chakula shindano
linaloendeshwa na Shirika la Kimataifa la OXFAM kwa mwaka 2016.
Zoezi
la kupitia fomu elfu tatu (3,000) za Mama Shujaa wa Chakula shindano
linaloendeshwa na Shirika la Kimataifa la OXFAM kwa mwaka 2016
likiendelea.
Majaji
wakipitisha maamuzi kwa fomu za washiriki wa shindano la mama shujaa wa
chakula msimu wa tano, 2016 zoezi litakalochukua wiki nzima ili
kuwapata washiriki.
No comments:
Post a Comment