Kituo
cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC kimemtunuku mfanyakazi wake Hussein
Baitira tuzo ya ubunifu baada ya mfanyakazi huyo kugundua mbinu ya kurekebisha viyoyozi zaidi ya
10 vya Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius
Nyerere ambavyo vilikuwa havifanyikazi.
Mkurugenzi Mwendeshaji wa
AICC, ndugu Elishilia Kaaya amemkabidhi Hussein hundi yenye thamani ya shilingi
3,800,000/-
ikiwa ni motisha kwa mfanyakazi huyo kutokana juhudi alizozionesha nakulipunguzia shirika gharama ambayo Shirika lingeingia kwa kukodisha mtaalamu kutoka nje ya nchi kuja kurekebisha viyoyozi hivyo.
Akiongea wakati wakukabidhi hundi hivyo,
ndugu Kaaya
alieleza kuwa tuzo hiyo imetolewa kwa mujibu wa utaratibu wa Shirika wa kumzawadia mfanyakazi ambaye ameonesha ubunifu wa hali ya juu katika kuliletea shirika maendeleo.
“Napenda kukupongeza kwa kuonesha ubunifu wa hali ya juu katika kazi yako na tuzo hii iwe kichocheo cha
kuongeza ubunifu zaidi kwako wewe pamoja na wafanyakazi wengine wote wa AICC”,
alisisitiza.
Mkurugenzi wa Miliki na Miradi,
ndugu Victor Kamagenge amesema kwamba kama viyoyozi hivyo visingeendelea kushindwa kufanyakazi shirika lingelazimika kuingia gharama ya kununua viyoyozi vipya na kubadilisha mfumo wa umeme.
Akizungumza baada ya kukabidhiwa hundi hiyo,
Hussein alisema kuwa majuma kadhaa kugundua tatizo la viyoyozi hivyo na kupata ufumbuzi
wake.
Alieleza kuwa viyoyozi vya
JNICC
ni aina ya mfumo wa teknolojia ya Hisense lakini mfumo huo haupo kwasasa na hivyo kulazimika kuingia katika mtandaokutafuta teknolojia nyingine kama
Hitachi nakutumia kitabumtando cha maelekezo (internet manual)
kugundua tatizo na kupata ufumbuzi wake.
No comments:
Post a Comment