Na Ally Daud.
Idadi ya vifo kwa watoto wachanga na wakina mama vinazidi kupungua kutoka
siku hadi siku katika kufikia malengo ya milenia .
Akizungumza hayo katika hafla fupi ya kuzindua maonesho ya picha Mwakilishi
wa Katibu Mkuu Wizara ya Afya , maendeleo ya Jamii , Jinsia na Watoto ,
Mkurugenzi wa Tiba Dkt. Margaret Mbando amesema kuwa Tanzania imepiga
hatua katika kufikia malengo ya milenia kwa kupunguza Idadi ya vifo kwa watoto
wachanga na wakina mama.
“Tumefanikiwa kupunguza Idadi ya vifo kwa watoto wachanga na wakina mama
ili kufikia malengo ya milenia kwa upande wa afya kupitia mfumo wa kujiunga na
bima ya afya kwa jamii” alisema Dkt. Mbando.
Mbali na hayo Dkt Mbando amesema kuwa amewakaribisha wananchi wote
hususani wakazi wa Dar es salaam kuudhuria maonesho hayo yaliyofunguliwa leo
yenye kauli mbiu ya “Huduma Bora kwa Afya Bora”yatayofikia kilele mpaka Juni
10 mwaka huu ili kupata ujumbe zaidi kupitia picha yanayofanyika Makumbusho
ya Taifa jijini.
Aidha ameipongeza Serikali ya Ujerumani kupitia ubalozi wake kwa kushirikiana
vizuri na Serikali ya Tanzania na kukubaliana kupata msaada wa Euro milioni 47
kwa muda wa miaka mitatu ijayo katika kuinua sekta ya Afya.
Kwa upande wa balozi wa Ujerumani Mhe. Egon Kochanke amesema kuwa
mchango wa Serikali ya ujerumani kwa sekta ya afya Tanzania utaendelea kuwa
sehemu ya mpango wa ushirikiano wa nchi mbili ili kuinua sekta hiyo nchini.
Balozi wa Ujerumani Mhe. Egon Kochanke kulia akikata utepe kuashilia kuanza rasmi kwa
maonesho ya picha yanayofanyika Makumbusho ya Taifa mpaka Juni 10 mwaka huu jijini Dar
es salaam na wa kwanza kushoto ni Mwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara ya Afya , maendeleo ya
Jamii , Jinsia na Watoto , Mkurugenzi wa Tiba Dkt. Margaret Mbando.
Balozi
wa Ujerumani Mhe. Egon Kochanke akiongea na waandishi wa habari na
Wadau wa Mpango wa Tanzania na Ujerumani kusaidia Afya (TGPSH) hawapo
pichani wakati wa ufunguzi wa maonesho ya picha yanayofanyika Makumbusho
ya Taifa mpaka Juni 10 mwaka huu jijini Dar es salaam.
Mwakilishi
wa Katibu Mkuu Wizara ya Afya , maendeleo ya Jamii , Jinsia na Watoto ,
Mkurugenzi wa Tiba Dkt. Margaret Mbando akiongea na waandishi wa habari
na Wadau wa Mpango wa Tanzania na Ujerumani kusaidia Afya (TGPSH)
hawapo pichani wakati wa ufunguzi wa maonesho ya picha yanayofanyika
Makumbusho ya Taifa mpaka Juni 10 mwaka huu jijini Dar es salaam.
Mshauri wa ufundi kutoka Mpango wa Tanzania na Ujerumani kusaidia Afya (TGPSH) Dkt.
Baltazar Ngoli wa kwanza kulia akitoa maelekezo ya picha kwa Balozi wa Ujerumani Mhe.
Egon Kochanke wa pili kulia pamoja na Mwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara ya Afya ,
maendeleo ya Jamii , Jinsia na Watoto , Mkurugenzi wa Tiba Dkt. Margaret Mbando wa tatu
kulia wakati wa ufunguzi wa maonesho ya picha yanayofanyika Makumbusho ya Taifa jijini
Dar es salaam.
Wadau mbalimbali wa Mpango wa Tanzania na Ujerumani kusaidia Afya (TGPSH) wakifuatilia
kwa makini maelezo ya Mwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara ya Afya , maendeleo ya Jamii ,
Jinsia na Watoto , Mkurugenzi wa Tiba Dkt. Margaret Mbando hayupo pichani wakati wa
ufunguzi wa maonesho ya picha yanayofanyika Makumbusho ya Taifa mpaka Juni 10 mwaka
huu jijini Dar es salaam.
No comments:
Post a Comment