Mshindi
wa Airtel Trace Music Stars Tanzania 2016, Melisa John, akiimba mara
baada ya kutangazwa mshindi katika fainali za shindano la Airtel Trace
Music Stars zilizofanyika katika ukumbi wa Julius Nyerere Jijini Dar es
salaam. Melisa amejishindia shilingi milioni 50 pamoja na kupata tiketi
ya kuiwakilisha Tanzania katika michuano ya Airtel Trace Music Stars
Afrika. Mshindi wa pili wa mashindano hayo ni Nandi Charles na Watatu
ni Salim Mlindila
Katibu
Mtendaji wa Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) Godfrey Mungereza (kulia)
akikabidhi mfano wa hundi ya shilingi milioni 50 kwa mshindi wa Airtel
Music Stars Tanzania 2016, Melisa John, mara baada ya kuibuka mshindi
wa shindano hilo. Melisa amejishindia shilingi milion50 pamoja na kupata
tiketi ya kuiwakilisha Tanzania katika michuano ya Airtel Trace Music
Stars Afrika.
Mshindi
wa Airtel Trace Music Stars Afrika, Nalimi Mayunga akitumbuiza wakati
wa fainali za shindano la Airtel Trace Music Stars Tanzania
lililofanyika katika ukumbi wa JNICC jijini Dar es salaama, wakati wa
fainali hizo, Mayunga pia alizindua wimbo wake wa video aliomshirikisha
mwimbaji wa Marekani Akon ujulikanao kama “ Please don’t go away”
Mshindi
wa Airtel Trace Music Stars Afrika, Nalimi Mayunga akitumbuiza wakati
wa fainali za shindano la Airtel Trace Music Stars Tanzania
lililofanyika katika ukumbi wa JNICC jijini Dar es salaama, wakati wa
fainali hizo, Mayunga pia alizindua wimbo wake wa video aliomshirikisha
mwimbaji wa Marekani Akon ujulikanao kama “ Please don’t go away”
Meneja
Rasilimali watu wa Airtel , Bi Gabriel Kaisi (kulia) akimkabithi Nandi
Charles mfano wa hundi ya shilingi milioni 5 mara baada ya kuibuka
mshindi wa pili wa shindano la Airtel Trace Music Stars Tanzania, katika
shindano hilo Melisa John aliibuka kuwa mshindi wa kwanza
mshindi
wa Airtel Music Stars Tanzania 2016, Melisa John, akiongea mara baada
ya kutangazwa mshindi na kukabithiwa mfano wa hundi ya shilingi
miliioni 50. Kulia ni mama yake Melisa John,na kushoto nao MC wa fainali
hizo.
mshindi
wa Airtel Music Stars Tanzania 2016, Melisa John akipongezwa na mama
yake baada ya kuibuka mshindi nakupata kitita cha shilingi milioni 50
Majaji wa shindano la Airtel Trace Music Stars Tanzania, Luciano Gadie Tsere(kushoto) na Tony Joett wakifatilia kwa makini washiriki wanavyoimba ili kupata mshindi wa shindano hilo kwa Tanzania
Mshindi wa tatu wa shindano la Airtel Trace Music Stars Tanzania Salim Mlindila akipokea mfano wa hundi ya shilingi milioni 2 kutoka kwa Meneja wa kampuni ya Tabasamu, Lucy Ngongoseke
Baadhi
wa waalikwa waliojitokeza kushuhudia shindano la Airtel Trace music
Stars wakiwa katika picha wakati wa koktaili kabla ya shindano hilo
kuanza
Washiriki
walioingia katika tano bora ya shindano la Airtel Trace Music Stars
wakiimba wimbo wa pamoja wakati wa finali za shindano hilo lililofanyika
ukumbi wa JINCC jijini Dar es Saalam.
Wageni
waalikwa mbalimbali wakifatilia na kuwashangilia washiriki wa shindano
la Airtel Trace Music Stars wakiwa Jukwaani huku wakirekodikumbukumbu
mbalimbali kupitia simu zao za mkononi
Wageni
waalikwa mbalimbali wakifatilia na kuwashangilia washiriki wa shindano
la Airtel Trace Music Stars wakiwa Jukwaani huku wakirekodikumbukumbu
mbalimbali kupitia simu zao za mkononi.
Mashindano
ya Airtel Trace Music Stars ya taifa yamefikia mwisho ambapo Melisa
John alitangazwa kuwa mshindi wakati wa fainalii za shindano hilo
lililowashirikisha washiriki watano bora na kufanyika katika ukumbi wa
Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Saalam.
Baada
ya kuimba kwa umahiri mkubwa wimbo wa mwanamuziki wakimarekani Mica
Paris ujulikanao kama “My One Temptation” Melisa aliweza kuwaaminisha
majaji kwamba hakika yeye anastahili kuwa mshindi wa Airtel Trace Music
Stars msimu wa 2.
Melisa amejishindia shilingi milion 50 huku mshindi wa pili Nandi Charles akijishindia shilingi milioni 5 na mshindi wa tatu Salim Mlindila akiondoka na shilingi milioni 2.
Kufatia
ushindi huo Melisa sasa amepata tiketi ya kuiwakilisha Tanzania katika
mashindano ya Airtel Trace Music Stars Afrika yatakayoshirikisha
washiriki kutoka nchi 9 zikiwemo Niger,
DR Congo, Gabon, Kenya, Madagascar, Malawi, Nigeria, Ghana and Zambia
yanayotegemea kufanyaka tarehe 11 Juni 2016 , Lagos nchini Nigeria.
Mshindi
wa Airtel Trace Music Afrika atapata nafasi ya kupata mafunzo ya
muziki na kurekodi video na mwanamuziki nguli na mtunzi wa nyimbo Keri
Hilson , Atlanta nchini Marekani.
“Nimefurahi
sana kuibuka mshindi leo, pamoja na ushindi huu mashindano yalikuwa ni
ya ushindani kwani kila mshiriki alikuwa na uwezo wa kuimba na mzuri kwa
namna tofauti. Nashukuru Mungu kwa kunifikisha hapa na nawashukuru
Airtel kwa kutuandalia jukwaa hili ambapo leo limenifanya niweze kuishi
ndoto zangu. Napenda sana kuimba na napenda sana mziki naamini huu ni
mwanzo mzuri wa safari yangu ya kuwa mwanamuziki nyota” alisema Mshindi
wa Airtel Trace Music Stars 2016 Melisa John.
Kwa
upande wake Afisa Uhusiano wa Airtel, Jane Matinde alisema “ Airtel
inajivunia kuwa sehemu ya kuinua maisha ya vijana wengi, tunaamini
kupitia program zetu za kuwawezesha vijana tutagusa maisha ya vijana
wengi na kuwawezesha kuzifikia ndoto zao. Tumefurahia mashindano ya
mwaka huu yamekuwa na mvuto zaidi na tunampongeza Melisa kwakuibuka kuwa
mshindi. Tunamtakia afanye vyema katika michuano ya Afrika nchini
Nigeria.”
Katika
fainali hizo Mshindi wa Airtel Trace Music Stars Afrika, Nalimi Mayunga
alitoa burdani ya nyimbo yake ya “ Nice Couple”na kuweza kuzindua kibao
chake na video yake ijulikanayo kama “ Please don’t go away” e
inayomshirikisha mwanamuziki nguli kutoka marekani, Akon
No comments:
Post a Comment