Utalii Wetu : TANAPA yazindua kampeni Kilimanjaro yenye kaulimbiu " Weka Mlima Safi, Tunza mazingira Yakutunze" - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Monday, 25 April 2016

demo-image

Utalii Wetu : TANAPA yazindua kampeni Kilimanjaro yenye kaulimbiu " Weka Mlima Safi, Tunza mazingira Yakutunze"


1+%25282%2529Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Saidi Mecky Sadiki akiongea wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya usafi Mlima Kilimanjaro iliyokuwa na kaulimbiu “ Weka Mlima Safi, Tunza Mazingira Yakutunze” katika lango la Marangu mwishoni mwa wiki. Wengine pichani ni Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA Allan Kijazi (kati) na Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Kilimanjaro Betrita Loibooki.
6+%25281%2529Wakurugenzi kutoka TANAPA wakifuatilia uzinduzi wa Kampeni ya usafi Mlima Kilimanjaro. Kutoka kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Uhifadhi Mtango Mtahiko, Mkurugenzi Utumishi na Utawala Bi. Witness Shoo, Mkurugenzi wa Mipango Dk. Ezekiel Dembe, Mkurugenzi wa Fedha Nassoro Mndeme na nyuma yake Mkurugenzi wa Utalii na Masoko Ibrahim Mussa.
7+%25281%2529Wanafunzi kutoka Chuo cha Taaluma ya Wanyamapori Pasiansi Mwanza nao walishiriki katika kampeni ya usafi Mlima Kilimanjaro.
2+%25281%2529Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Kilimanjaro Betrita Loibooki akiongea wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Usafi Mlima Kilimanjaro.
10+%25281%2529
Baadhi ya wadau walioshiriki kampeni ya usafi Mlima Kilimanjaro
3+%25281%2529Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Saidi Mecky Sadiki akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa TANAPA pamoja na wadau kutoka Kampuni mbalimbali za mawakala wa utalii kutoka Kilimanjaro na Arusha wanaoshiriki Kampeni maalum ya usafi Mlima Kilimanjaro.
9+%25281%2529Idadi kubwa ya wadau wa sekta ya utalii walishirikiana vema na TANAPA kusafisha Mlima Kilimanjaro.
8+%25281%2529Wageni waalikwa wakivaa ‘gloves’ kabla ya kuanza zoezi la usafi.
4+%25281%2529Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Saidi Mecky Sadiki akiokota uchafu wa taka ngumu wakati wa kampeni ya usafi Mlima Kilimanjaro.
5+%25281%2529Meneja Mawasiliano wa TANAPA Pascal Shelutete akiokota uchafu wa taka ngumu wakati wa kampeni ya usafi Mlima Kilimanjaro.
11
Mazingira safi yataendelea kuufanya Mlima Kilimanjaro kutiririsha maji kwa wingi zaidi.

Na Dixon Busagaga wa Kanda ya Kaskazini.

No comments:

Post a Comment

Contact Form

Name

Email *

Message *

Tuwasiliane

Name

Email *

Message *