Mkurugenzi
wa Teknolojia ya Habari wa Airtel Tanzania, Frank Filman na Afisa
Uhusiano wa Airtel, Jane Matinde, wakitoa elimu kwa wakazi wa Sinza
Kijiweni jijini Dar es Salaam Aprili 13.2016, kuhusu huduma mpya ya
kifurushi cha Airtel Yatosha kijulikanacho kama “Jipimie Yatosha Yako”
kitakachompatia uhuru mteja kutengeneza na kununua kifurushi
kinachokidhi mahitaji yake.
Afisa
Uhusiano wa Airtel, Jane Matinde (wa pili kulia), na Msaidizi Mtendaji
wa Mkurugenzi Mkuu wa Airtel, Ellen Lupili wakitoa elimu kwa wakazi wa
Sinza Kijiweni jijini Dar es Salaam Aprili 13.2016, kuhusu huduma mpya
ya kifurushi cha Airtel Yatosha kijulikanacho kama “Jipimie Yatosha
Yako” kitakachompatia uhuru mteja kutengeneza na kununua kifurushi
kinachokidhi mahitaji yake.
Afisa
Mauzo wa Airtel Tanzania, Anatory Lelo (kulia), akitoa elimu kwa wakazi
wa Manzese Midizini jijini Dar es Salaam Aprili 13.2016, kuhusu huduma
mpya ya kifurushi cha Airtel Yatosha kijulikanacho kama “Jipimie Yatosha
Yako” kitakachompatia uhuru mteja kutengeneza na kununua kifurushi
kinachokidhi mahitaji yake.
Afisa
Mauzo na Usambazaji wa Airtel Tanzania, Swaliatu Msuya (wa pili
kushoto), akitoa elimu kwa wakazi wa Manzese Midizini jijini Dar es
Salaam Aprili 13.2016, kuhusu huduma mpya ya kifurushi cha Airtel
Yatosha kijulikanacho kama “Jipimie Yatosha Yako” kitakachompatia uhuru
mteja kutengeneza na kununua kifurushi kinachokidhi mahitaji yake.
Afisa
Kitengo cha Manunuzi wa Airtel Tanzania, Alexander Mboya (kushoto), na
Afisa wa Huduma kwa Wateja, Michael Mnyabebe (kulia), wakitoa elimu kwa
wakazi wa Manzese Midizini jijini Dar es Salaam Aprili 13.2016, kuhusu
huduma mpya ya kifurushi cha Airtel Yatosha kijulikanacho kama “Jipimie
Yatosha Yako” kitakachompatia uhuru mteja kutengeneza na kununua
kifurushi kinachokidhi mahitaji yake.
Afisa
wa Huduma kwa Wateja, Michael Mnyabebe (kushoto), akitoa elimu kwa
mkazi wa Manzese Midizini jijini Dar es Salaam Aprili 13.2016, kuhusu
huduma mpya ya kifurushi cha Airtel Yatosha kijulikanacho kama “Jipimie
Yatosha Yako” kitakachompatia uhuru mteja kutengeneza na kununua
kifurushi kinachokidhi mahitaji yake.
Timu
ya Wafanyakazi wa Airtel wakiwa katika picha ya pamoja wakijiandaa
kuingia sokoni katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam Aprili
13.2016, kwa ajili ya kutoa elimu kwa wananchi kuhusu huduma mpya ya
kifurushi cha Airtel Yatosha kijulikanacho kama “Jipimie Yatosha Yako”
kitakachompatia uhuru mteja kutengeneza na kununua kifurushi
kinachokidhi mahitaji yake.
Kushoto
ni Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Bw, Sunil Colaso akiongea na wateja wa
Airtel mkoani Morogoro leo kuhusu huduma mpya ya Jipimie Yatosha yako
iliyozinduliwa mwazoni mwa wiki hii. Airtel ilizindua huduma ya Jipimie
yatosha yako ili kutoa uhuru kwa watumia wa huduma ya vifurushi vya
Airtel Yatosha kutengeneza na kujipia vifurushi kadiri watakavyo. Leo
hii wafanyakazi wa Airtel wote wameingia mtaani na kwend kuwaonyesha
wateja jinsi watakavyofaidi huduma hiyo.
Kufatia
uzinduzi wa huduma mpya ijulikanayo kama Airtel Jipimie Yatosha Yako
kampuni ya simu za mkononi ya Airtel leo imewatembelea wateja wake
katika maeneo mbalimbali jijini Dar es saalam na kuwafikishia huduma hii
mahali pao pa kazi na makazi yao lengo likiwa ni kutoa elimu jinsi gani
ya kujitengenezea vifurushi vinavyokidhi mahitaji yao
Airtel
Jipimie Yatosha Yako "ni moja ya kifurushi cha kibunifu zaidi
kinachompatia mteja uhuru wa kujiunga na Airtel, kuchangua na kupanga
matumizi yake kwa kuunda kifurushi kitakachokidhi mahitaji yake
kiuchumi na kijamii.
Akiongea
kuhusu zoezi hilo Mkurugenzi wa technologia ya habari wa Airtel, Bwana
Frank Filman alisema “ tumeona ni vyema kupeleka huduma hii kwa wateja
wetu na kuwaelekeza ni jinsi gani sasa wanaweza wajitengenezea vifurushi
vya yatosha vinavyokidhi mahitaji yao. Kupitia huduma hii ya Airtel
Jipimie Yatosha Yako sasa tumewawezesha wateja kununua kifurushi cha
muda wa maongezi tu, au kuchanganya kifurushi cha muda wa maongezi na MB
za intaneti au Muda wa Maongezi na SMS lakini pia bado wanaweza kupata
vifurushi vyote yaani muda wa maongezi zaidi, SMS zaidi na MB zaidi
Wakiongea
kwa nyakati tofauti mkazi wa Sinza Kijiweni na Fundi rangi bwana Hamisi
Chande alisema “ hii ni habari njema kwetu wateja kwamba sasa tunaweza
kujitengenezea vifurushi tunavyotaka kwani itatupa fursa ya kupata
zaidi, awali nilikuwa naweza kumnunuali ndugu yangu kufurushi na kupata
hadi huduma ya intaneti wakati sumu yake haina huduma hii sasa kupigia
huduma hii mpya tutafaidika zaidi na pia tutaweza kupanga vyema
vifurushi kulingana na matumizi yetu. Nawapongeza sana Airtel kwa kuja
na huduma hii ya kisasa na kutuletea elimu huku tuliko.”
Kujiunga
na kifurushi cha Yatosha na kufurahia Jipimie Yatosha Yako, wateja
wanatakiwa kupiga namba *149*99# na kuchagua namba 5 ‘Jipimie Yatosha
Yako’ na kutengeneza kifurushi cha chaguo lake.
No comments:
Post a Comment