Maisha Yetu : Kijiji cha Olbili kilichopo wilayani Simanjiro chakabiliwa na njaa - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633


PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0676 643 633

Wednesday, 13 April 2016

Maisha Yetu : Kijiji cha Olbili kilichopo wilayani Simanjiro chakabiliwa na njaa

 Wananchi wa Kijiji cha Olbili kilichopo kitongoji cha Tilili,kata ya Shambarai wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara wakibeba mabango kupinga kunyang`anywa ardhi ya waliyokua wakiitumia kwa kilimo na kubadilishwa kuwa ya malisho ya mifugo,kijiji hicho  kinakabiliwa na tatizo la ukosefu chakula cha miongoni  mwa familia nyingi hali inayochangia kuzorota kwa hali ya lishe na shughuli za kijamii pamoja na za kiuchumi.




Wananchi wa Kijiji cha Olbili kilichopo kitongoji cha Tilili,kata ya Shambarai wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara wakibeba mabango kupinga kunyang`anywa ardhi ya waliyokua wakiitumia kwa kilimo na kubadilishwa kuwa ya malisho ya mifugo,kijiji hicho  kinakabiliwa na tatizo la ukosefu chakula cha miongoni  mwa familia nyingi hali inayochangia kuzorota kwa hali ya lishe na shughuli za kijamii pamoja na za kiuchumi.Picha na Ferdinand Shayo



Na Ferdinand Shayo wa Wazalendo 25 Blog ,Simanjiro.

Kijiji cha Olbili kilichopo kitongoji cha Tilili,kata ya Shambarai wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara kinakabiliwa na tatizo la ukosefu chakula cha miongoni  mwa familia nyingi hali inayochangia kuzorota kwa hali ya lishe na shughuli za kijamii pamoja na za kiuchumi.

Wananchi wa kijiji hicho Zuhura Salim na Anna Lazaro  wamesema kuwa uhaba huo wa chakula unatokana na kunyang`anywa  maeneo waliyokua wanatumia kwa kilimo na kutumika kama ardhi ya malisho.

Wananchi hao waliandamana na mabango yao kuzunguka eneo la shamba hilo wameiomba serikali kupitia wizara ya ardhi na wizara ya kilimo kuingilia kati mgogoro huo baina yao na wafugaji wanaogombea eneo hilo ambalo kwa zaidi ya miaka  24 tangu mwaka 1992 hadi mwaka 2013 ambapo walizuiwa kutumia maeneo hayo ambayo  walikua  wakiyatumia kwa shughuli za kilimo cha kujikimu .

Eliud Jackson ni Mwanakijiji wa Olbili amesema kuwa licha ya kunyimwa maeneo ya kulima pia mwaka huu hawakupata chakula cha msaada kama kata nyingine zilizopata mgao huo hivyo kuteseka na njaa  wao na watoto wao ,wamemuomba Rais Magufuli kutazama suala hilo na kulipatia ufumbuzi.


Mwenyekiti wa Kitongoji cha Tilili Kingi Lomayani Laizer amesema kuwa baada ya kuzuiliwa kulima na Mtendaji wa Kata na Diwani aliyekua madarakani walifika katika ngazi za wilaya bila mafanikio hivyo wanamuomba Mkuu wa Mkoa wa Manyara afike kutatua mgogoro huo ili kuwanusuru na baa la njaa.

“Nimefuatilia suala hili kwa Mwenyekiti,Mtendaji wa kata na Diwani aliyemaliza muda wake bila mafanikio kwani wao ndio walitoa zuio la kutuzuia kulima katika maeneo haya ,inaonekana jambo hili linashikiliwa na wafugaji wenye fedha wanatumia fedha zao kuwanyanyasa wakulima” Alisema Laizer

Aliiomba serikali kupitia wizara ya kilimo,ardhi kufika katika kijiji hicho na kutatua kero hiyo ya muda mrefu kwani wamekua wakishindwa kuendesha familia zao kutokana na kutegemea kilimo kama shughuli ya kuwapatia chakula na kipato.

No comments:

Post a Comment