NAIBU
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi
Andrea Kigwangalla, ametembelea Hospitali ya Taifa ya Kifua Kikuu
Kibong'oto eneo la Sanya Juu Wilani Siha Mkoani Kilimanjaro.
Dkt.
Kigwangalla katika Hospitali hiyo, alipata kitembelea maeneo mbalimbali
ikiwemo wodi za wagonjwa wa Kifua Kikuu (TB) ya kawaida na ile kali
ambapo pia aliweza kutembelea eneo la kituo cha utafiti cha magonjwa
hayo pamoja na Maabara.
Kihistoria
Hospitali hiyo ya Kibong’oto ilifunguliwa rasmi 29 Oktoba mwaka 1952 na
Lady Twining, baada ya miaka saba ya vita ya pili ya dunia chiniya
utawala wa Muingereza na imekuwa ikitoa huduma hiyo ya magonjwa ya
kuambukiza hususani Kifua Kikuu.
Kwa
upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali hiyo, Daktari Bingwa wa
Magonjwa ya Kuambukiza, Dkt Riziki Kisonga amemwelezea Naibu Waziri
changamoto mbalimbali ikiwemo suala la nyumba za watumishi na mambo
mengine ikiwemo suala la bajeti ya vifaa tiba.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Andrea Kigwangalla akitia saini kitabu cha wageni katika Hospitali ya Taifa ya Kifua Kikuu Kibong'oto ilipo Mkoani Kilimanjaro wakati wa ziara yake 10 Aprili 2016. Anayeshuhudia ni Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali hiyo, Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Kuambukiza, Dkt Riziki Kisonga
Msafara huo ukirejea katika maeneo mengine wakati wa ukaguzi na Naibu Waziri wa Afya Dk.Kigwangalla.
Pichani
wote waliovaa 'mask' maalum ni kwa ajili ya kuzuia maambukizi ya
vijidudu vya ugonjwa wa Kifua Kikuu (TB) hasa kwa upande huo wa wagonjwa
maalum wa TB sugu.ambao wapo upande maalum. Hivyo kuvaa kifaa hicho
kinasaidia kupunguza hali ya maambukizo wakati wa kufika eneo hilo kama
sheria na taratibu zilizowekwa kitaalam na uongozi wa Hospitali hiyo.
No comments:
Post a Comment