Elimu : Ufaulu Wapanda kwa shule za msingi , Mufindi - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


7 Jan 2017

Elimu : Ufaulu Wapanda kwa shule za msingi , Mufindi



 

Na Ofisa habari Mufindi
Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi imeendelea kustawi katika sekta ya elimu ambapo tathimini ya matokeo ya darasa la saba ya Halmshauri hiyo yanaonesha kupanda kutoka asilimia 80.39 mwaka 2015 hadi asilimia 84.90% mapema mwaka jana, ikiwa ni sawa na ongezeko la asilimia 4.51.


Akisoma taarifa wakati wa kikao cha thimini ambacho huwakutanisha wakuu wa shule zote za msingi na maaofisa elimu kata, Ofisa elimu taaluma wa Halmshauri ya Wilaya ya Mufindi MRIAMU NGALA amebainisha, kuwa tathimini ya ufaulu huo umejumuisha shule 143, watahiniwa elfu 05 mianne 38 ambapo wavulana ni elfu 02 miatatu 84 na wasichana ni elfu 03 na 54 huku wanafunzi waliofaulu na kuchaguliwa kuendelea na elimu ya Sekondari wakiwa ni elfu 4 miasita 17 sawa na asilimia 84.9.


Akisoma taarifa hiyo Bi. NGALA ameainisha masomo ambayo wanafunzi wamefanya vizuri zaidi kuwa ni pamoja na somo la Kiswahili ambalo ufaulu wake ni asilimia 90. 51, Sayansi 90.13, Maarifa 87.88, Hisabati 56.34 huku somo la Kingereza likishika nafasi ya tano kwa asilimia 27.20.


Aidha, afisa elimu huyo mwenye dhamana ya taaluma, ametaja baadhi ya malengo ambayo walijiwekea na ndiyo yaliyochangia kufikia mafanikio hayo kuwa ni pamoja na kufaulisha kwa asilimia 95, ufuatiliaji wa utendaji kazi, uwepo wa kambi za masomo, udhibiti wa utoro wa Wanafunzi na Waalimu, ukamilishaji wa mada kwa wakati na uwepo wa mazoezi ya kujipima. Idara ya elimu msingi ya Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi imeweka uratibu wa kufanya tathimini ya kina kwa kila mwaka mara baada ya kutoka kwa matokeo ya mitihani ya darasa la saba ili kuangazia mafanikio ya ufaulu kwa kila shule, kubainisha changamoto na kuziwekea mikakati ya kuzikabili huku tathimini hiyo ikienda sanjari na kutunuku zawadi na vyeti kwa wakuu wa shule na maofisa elimu kata walifaulisha wanafunzi wengi zaidi hivyo kupandisha wastani wa ufaulu wa halmashauri.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad