Matukio : Mhe. Said Meck Sadick afanya ziara ya utambulisho wilaya ya Hai, Kilimanjaro. - Wazalendo 25 Blog

Breaking

Glory to Story.


Post Top Ad


27 Apr 2016

Matukio : Mhe. Said Meck Sadick afanya ziara ya utambulisho wilaya ya Hai, Kilimanjaro.


Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ,Said Mecky Sadickyakitia saini katika kitabu cha wageni alipotembelea ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Hai hii leo.
Mkuu mpya wa wilaya Hai , Gelasius Byakanwa (kushoto) akimuelekeza jambo Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Said Mecky Sadick alipotembelea ofisini kwake mapema hii leo.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ,Said Mecky Sadick akizungumza na watendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Hai.
Mkuu mpya wa wilaya ya Hai,Gelasius Byakanwa akitoa taarifa ya wilaya hiyo kwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ,Said Mecky Sadick alipotembelea ofisini kwake mapema hii leo.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Hai ,Said Mderu akiandaa taarifa kwa ajili ya kukabidhi kwa mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ,Said Mecky Sadick.
Mkuu wa Polisi wilaya ya Hai ,OCD Pancras Mdimi akifuatilia taarifa ya wilaya iliyokuwa ikitolewa kwa mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Said Mecky Sadick akisoma ubao wenye majina ya wakuu wa wilaya waliowahi kufanya kazi katika wilaya hiyo .
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ,Said Mecky Sadick akiongozana na Mkuu mpya wa wilaya ya Hai,Gelasius Byakanwa wakati wakitoka katika ofisi ya mkuu huyo wa wilaya.

Na Dixon Busagaga wa Globua ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

Post Top Ad