Mwanzilishi wa Taasisi ya Wanaume Men at Work Bw. Maxwell Stansalaus akizungumza na Wanaume jana jijini Arusha katika mkutano Mkuu wa Wanaume uliofanyika jana na kuhudhuriwa na zaidi ya wanaume 700 ambao lengo lake ni kuwakumbusha wanaume wajibu walionao kwa familia,jamii na taifa.
Mhamasishaji wa Masuala ya kijamii Samuel Sasali akizungumza na mamia ya wanaume waliokusanyika katika Mutano wa wanaume ulioandaliwa na taasisi ya wanaume ya Man at work.
Mkuu wa Chuo cha Arusha Journalism and Training Cetre ( AJTC) Bw. Joseph Mayagila akihojiwa na Vyombo vya habari (hawapo pichani) alivyoungana na mamia ya wanaume waliokusanyika katika Mkutano wa wanaume ulioandaliwa na taasisi ya wanaume ya Men at work.Picha na Ferdinand Shayo
Mhamasishaji wa Masuala ya kijamii Samuel Sasali akizungumza na mamia ya wanaume waliokusanyika katika Mutano wa wanaume ulioandaliwa na taasisi ya wanaume ya Man at work.Picha na Ferdinand Shayo
Wanamuziki wa bendi wakitumbuiza katika Mkutano wa wanaume ulioandaliwa na taasisi ya wanaume ya Men at work.
Na Ferdinand Shayo wa Wazalendo 25 Blog ,Arusha.
Taasisi
isiyo ya kiserikali ya Wanaume Kazini
maarufu kama Men at Work imelaani vikali vitendo vya ushoga vinavyoshusha hadhi
na thamani ya wanaume hivyo wameitaka serikali kupiga vite vitendo hivyo
ambavyo ni kunyume cha Maadili ya Tanzania na Afrika kwa Ujumla.
Muasisi wa
Taasisi hiyo yenye makao yake jijini
Arusha Maxwell Stanslaus amesema kuwa Wanaume kazini wanapinga vikali
vitendo vya ushoga kwa zaidi ya Asilimia 100% na kuwataka wanaojihusisha na
vitendo hivyo kuacha Mara moja.
Maxwell
alisema hayo jana katika mkutano Mkuu wa Wanaume kazini uliofanyika jijini hapa
huku akisema kuwa taasisi hiyo imelenga kuhimiza wanaume kote nchini kutimiza
wajibu wao na kutenda majukumu yao kama wanaume katinga ngazi ya familia,jamii
na taifa ili kuchochea maendeleo.
“Kwa sasa
tunaona nidhamu ya serikali imerudi kutokana na Mwanaume mmoja tu Rais John
Pombe Magufuli kuamua kutimiza wajibu yake hivyo Basi Wanaume zaidi ya Milioni walioko Tanzania wakiamua kutimiza majukumu
yao na wajibu Tanzania itanyooka” Alisema Maxwell
Moja kati ya
Wanaume waliohudhuria ni Joseph Mayagila alisema kuwa matatizo ya ushoga
yanatokana na baadhi ya wanaume kujisahau na kujaribu kuwa wanawake ,jukwaa
hili la wanaume ni muhimu kuwakumbusha wanaume juu ya uanaume wao na kutimiza
yale yanayowapasa kama wanaume.
Dokta
Emmanuel Buganga ameeleza kuwa vuguvugu
la wanawake kudai haki zao linatokana na baadhi ya wanaume kutotimiza wajibu
wao kama wanaume wameacha majukumu yao ya kutunza familia zao na kuwa walezi na
walinzi wa familia .
Mhamasishaji
wa Masuala ya kijamii Samuel Sasali amesema kuwa wanaume wengi wamejisahau sana
katika masuala ya malezi ya familia kwani usimpolea mtoto katika njia impasayo
atakuja kukuaibisha ukubwani.
No comments:
Post a Comment