Jumla
ya watoto 120 wanatarajiwa kufanyiwa upasuaji katika hospitali ya
Bugando jijini Mwanza, kufuatia tatizo la kichwa kikubwa walilozaliwa
nalo chini ya udhamini wa taasisi ya GSM ambayo imedhamini zoezi hilo
litakalofanyika katika mikoa mitano ikiwa ni awamu ya kwanza kati ya nne
zinazotarajiwa kufanyika tanzania nzima.
Akiongea
na waandishi wa habari katika uzinduzi wa zoezi hilo linalojumuisha
madaktari Bingwa 10 kutoka Taasisi ya mifupa na Upasuaji MOI, Mkurugenzi
Mkuu wa Hospitali ya Bugando, Profesa Kien Mteta aliishukuru taasisi ya
GSM kwa kuamua kulichukua tatizo hilo ambalo ameliita kuwa ni kubwa
ukilinganisha na jinsi linavyochukuliwa na jamii ya watanzania.
Dk
Kien aliwaambia wanahabari kwamba jumla ya watoto 2000 huzaliwa na
vichwa vikubwa katika kanda ya Ziwa peke yake, na mtaalamu wa kuhudumia
wagonjwa wa namna hii ni mmoja tu ambapo pia kwa Tanzania nzima,
wataalamu wa upasuaji wa watoto wenye vichwa vikubwa wako tisa tu.
Cha
kusikitisha ni kwamba kati ya hao, ni wachache sana hurudi kwa ajili ya
matibabu bali wengi wao hufariki kwa kufichwa ndani na wazazi wao aidha
kwa imani za kishirikina ama kushindwa kwa wazazi kumudu gharama za
matibabu.
Mkuu
wa Hospitali ya Bugando, Profesa Kien Mteta (kulia) akiongea na
wanahabari huku akisikilizwa kwa umakini na Mkurugenzi wa taasisi ya
Mifupa na upasuaji Dk Othman Kiloloma (katikati) pamoja na Afisa kutoka
GSM, Halfan Kiwamba.
Mtaalamu
wa upasuaji wa ubongo na mishipa ya Fahamu, Dk Gerald Mayaya akitoa
ufafanuzi kwa wanahabari kuhusiana na kambi ya upasuaji wa watoto wenye
vichwa vikubwa katika Hospitali ya Bugando.
Meneja
Mkuu wa taasisi ya GSM, Shannon Kiwamba (katikati) akiongea na
wanahabari kuhusiana na sera yao mpya ya kusaidia watanzania katika
masuala ya elimu na Afya, kulia kwake ni Mkuu wa Hospitali ya Bingando,
Prof Kien Mtena na kushoto kwake ni Mkuu wa mawasiliano wa Taasisi ya
GSM, Halfan Kiwamba.
Mkuu
wa kitenngo cha Upasuaji na Mifupa ambaye ndio mratibu wa kambi ya tiba
ya watoto wenye vichwa vikubwa na migongo wazi akifafanua jambo kwa
wanahabari(hawapo pichani).
Baadhi ya wahudumu wanaoshiriki kambi ya watoto wenye vichwa vikubwa wakisikiliza viongozi wao wakati wakiongea na wanahabari.
Wanahabari kazini.
Picha ya pamoja ya wawezeshaji wa zoezi la kambi ya upasuaji wa watoto wenye vichwa vikubwa na migongo wazi.
Mkuu wa Hospitali ya Bingando, Prof Kien Mtena (kulia) katika picha ya pamoja na mwanahabari wa Jembe Fm Mwanza G. Sengo.
Taarifa kwa umma kupitia mabango ya Hospitali ya Rufaa Bugando.
No comments:
Post a Comment