Matukio : Waziri, Prof. Maghembe awasimamisha kazi wafanyakazi wa 4 - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


25 Mar 2016

Matukio : Waziri, Prof. Maghembe awasimamisha kazi wafanyakazi wa 4


  Waziri wa Maliasili na Utalii Prof. Jumanne Maghembe (kulia) akizungumza katika Mkutano na Waandishi wa Habari kuhusu kumsimamisha kazi Mtendaji Mkuu na Wakurugenzi  watatu wa  Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) katika ukumbi wa Ngorongoro Makao Makuu wa Wizara hiyo Mpingo House Jijini Dar es Salaam leo .  Kushoto  ni Naibu Waziri wa Wizara ya Maliasili na Utalii Eng. Ramo Makani.
 Baadhi ya Waandishi wa habari Waliohudhuria Mkutano huo wa Waziri wa Maliasili na Utalii Prof. Jumanne Maghembe katika ukumbi wa Ngorongoro Makao Makuu wa Wizara hiyo Mpingo House Jijini Dar es Salaam leo.


Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof.Jumanne Mghembe amemsimamisha kazi  Mtendaji  Mkuu  wa Wakala wa Huduma za Misitu nchini, (TFS)    Bw. Juma Mgoo pamoja na Wakurugenzi wawili  wa wakala  hiyo ili kupisha  uchunguzi kutokana na  ukusanyaji usioridhisha wa mapato yatokanayo na mazao ya misitu.

Prof. Maghembe ametaja  majina ya Wakurugenzi hao aliowasimamisha kazi  kuwa  ni  Mkurugenzi Rasilimali Misitu, Bw.  Zawadi Mbwambo  pamoja   na Kaimu   Mkurugenzi  wa Mipango na Matumizi endelevu  ya Misitu, Bw. Nurdin Chamuya

Wengine  waliosimamishwa  kazi ni wakuu wa Kanda za Wakala wa Huduma za Misitu  nchi nzima   ambao  ni Bw.  Hubert Haule wa Kanda ya Kusini,  Bw.  Bakari Rashidi wa kanda ya Mashariki,                Bw. Shabani Mwinyi Juma wa kanda ya kati ,  Emanuel Minja wa kanda ya Magharibi pamoja na  Bw. Bruno wa nyanda za juu kusini

Akizungumza leo na Waandishi wa Habari Makao Makuu ya Wizara hiyo jijini  Dar es Salaam, Prof. Maghembe amesema hatua hiyo imekuja  baada ya  kubaini shehena kubwa za magogo   aina ya mninga  katika Mkoa wa  Rukwa wilayani Kalambo  yakiwa  yamekatwa na kuwekwa ndani ya makontena kule kule   ndani ya msitu  pamoja na kutengenezewa nyaraka  feki zinazoonesha magogo hayo yanatoka nchini  Zambia    tayari  kwa  kusafirishwa kupelekwa nchini  China lakini hata hivyo  baada ya kubaini wizi huo hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa na Wakala ya Huduma za Misitu Tanzania ( TFS).

Amesema kuwa baada ya kubaini hivyo usiku wa jana aliweza kupata taarifa kuwa  shehena ya Magogo hayo yenye  thamani  ya shilingi milioni 500  yaliyotakiwa  kupelekwa Makao makuu ya Wilaya ya Kalambo   yamemwagiwa petrol  na yamechomwa moto

Aliongeza kuwa  kumekuwa na ubadhilifu unaofanywa na Maofisa wa ukusanyaji wa maduhuri  ya Serikali yanayotokana na rasilimali za misitu katika Mikoa na Wilaya kwa kutowasilishwa katika mfuko Mkuu wa Serikali.

Kwa upande mwingine , Prof Maghembe amesema kuwa  pesa zitokanazo na makusanyo hayo zimekuwa hazipelekwi  benki kwa wakati na hata zikipelekwa benki  zimekuwa zikipelekwa pungufu na muda mwingine pesa hizo zimekuwa hazipelekwi kabisa.

Wakati huo huo, Waziri Maghembe  amemsimamisha kazi  Mkurugenzi Msaidizi wa  Idara ya Wanyamapori wa Matumizi Endelevu,   Dkt. Charles Mulokozi  kwa kosa la kukaidi agizo la kusaini vibali  vya kusafirisha Wanyamapori nje ya nchi.

Hatua hiyo imekuja  baada  ya jana  nyani 61 kukamatwa katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro na kubaini kuwa Idara ya Wanyamapori  ndio iliyotoa vibali vya kusafirisha nyani hao na vibali hivyo vikiwa vimetiwa saini na Mkurugenzi huyo.
Ameongeza kuwa ndege ya kutoka Ulaya Kusini  iliyotakiwa kusafirisha nyani hao imeshikiliwa pamoja na rubani wake kwa mahojiano zaidi.


Prof ,Maghembe amesema  kutokana taarifa alizozipata kuwa jumla ya  nyani 450 ndio waliokuwa wanawindwa kwa ajili ya  kusafirishwa kupelekwa nje.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad