Bw. Jeyapaulraj, akipokea nyaraka kwa niaba ya Abu Dhabi Indian School, mshindi wa shule na kituo cha kikundi cha watoto yatima.
Bibi Atija, akipokea nyara kwa niaba ya Mkuu wa Umoja wa Wanawake, mshindi wa kikundi cha wazee.
Wafanyakazi
wa Shirika la Ndege Etihad, Wahudumu wa watoto, marubani, Ali Al
Shamsi, Makamu Rais wa mikakati akiwa na watoto wenye Autism.
CHINI ya
ulezi wake Mtukufu, Sheikha Shamsa bint Hamdan Bin Mohamed Al Nahyan,
Mheshimiwa Mwenyekiti wa kituo cha Autism mjini Abu Dhabi, Shirika la
ndege la Etihad limeendesha hafla hiyo ya kuchangisha fedha kwa sababu
maalum kupitia matembezi.
Zaidi ya washiriki 5,200 wa kila umri walikusanyika katika bustani za Al Mushrif Central Mjini Abu Dhabi siku ya Ijumaa Machi 18 kushiriki katika tukio la matembezi ya dakika 30.
Fedha
zote zilizotolewa katika tukio zitakwenda katika ujenzi wa jengo jipya
litalokuwa kituo kipya cha utabibu mjini Abu Dhabi kwa ajili ya
waathirika wa ugonjwa wa Autism, pamoja na ukarabati wa shule nchini
India.
Mtukufu
Sheikha Shamsa Bint Hamdan Bin Mohamed Al Nahyan alitoa pongezi kwenda
shirika la ndege la Etihad kwa ajili ya maandalizi ya tukio hilo, ambayo
inaonyesha dhaira ya kampuni kuendelea kusaidia kuleta maendeleo ya
kijamii na uboreshaji endelevu katika jamii zinazo wazunguka.
Tukio
hilo pia lilihudhuriwa na Mtukufu Sheikh Thiyab Bin Khalifa Bin Hamdan
Al Nahyan, Eugenia Davis, Baraza la Umoja wa Mataifa ya Amerika, Kanali
Abdulrahman Al Swaidi, Wizara ya Mambo ya Ndani, Shayma Nawaf Fawwaz,
Afisa Mtendaji Mkuu wa GOSSIP, Mheshimiwa Mariem Al Rumaithi, Mjumbe wa
Bodi ya Shirika la matunzo ya kibinadamu na Mahitaji Maalum la Zayed ,
na Dk. Khawla Salem Rashed Al Saaedi, mwakilishi wa Rais wa Wanawake na
Health Alliance International.
Khaled
Al Mehairbi, Makamu wa Rais wa uendeshaji wa uwanja wa ndege wa Abu
Dhabi na Mwenyekiti wa Michezo na kamati za kijamii katika shirika la
ndege Etihad, alisema: "Shirika la ndege Etihad lina nia ya kutoa huduma
bora kwa watoto wenye ugonjwa wa akili ili kuboresha ubora wa maisha
yao.
"Hii
ni sehemu ya ahadi yetu kuendelea kuleta maendeleo kwa jamii yetu ya
ndani na kuboresha afya ya umma na kuongeza ufahamu wa autism.”
"Matembezi
haya ya faraja kwa mara nyingine tena imewaleta kwa pamoja jamii ya Abu
Dhabi, na tuna matumaini kuwa na uwezo wa kuongeza ufahamu na fedha
muhimu kwa kusaidia watu wenye mahitaji – hapa nyumbani pamoja na
kimataifa”
Matebezi
hayo yalikuwa wazi kushiriki kwa watu wa miaka yote, baada ya usajili
washiriki walipokea kipima spidi pamoha na fulana iliyobeba nembo ya
tukio hilo.
Bibi Athba Ali, meneja manunuzi wa shirika la ndege la Etihad na
mama wa watoto wawili, alisema: "Mimi nina furaha na fahari kuwa sehemu
ya tukio hili la “Tembea kwa Hisani" tukio hilo. Nina furaha kuona
kwamba tukio limefanikiwa katika kuleta kila mtu pamoja ili kusaidia
kufanikisha tukio hili. Tulifurahia tukio hili la matembezi na tayari
tunatazamia tukio la mwaka ujao.”
Burudani
kutoka “Bollywood” ilikuwepo kuwapa washiriki motisha na burudani huku
shirika la ndege la Etihad waliandaa shughuli mbali mbali kwa ajili ya
wanafamilia wote ikiwa ni pamoja na mazoezi ya kurusha ndege chini ya
nahodha wa ndege pamoja na warsha ya mapishi ya ndani ya ndege chini ya
mpishi mkuu. Wahudumu wa watoto walikuwepo kusaidia kusimamia na kuchangamsha watoto.
Wakati
wa mchezo wa 'Jaribu na ushinde', waliohudhuria walikuwa na nafasi ya
kushinda idadi kubwa ya zawadi ikiwa ni pamoja na tiketi daraja la
uchumi kutoka shirika la ndege la Etihad, Bidhaa zisizolipiwa ushuru za
bure, Uanachama wa mwaka mmoja kwa famila nzima wa Kituo cha kimataifa
cha mapumziko na michezo cha Al Forsan, malazi ya wikiendi nzima katika
hoteli ya nyota 5, Vocha ya watu wawili ya mlo wa usiku, zawadi kutoka
kwa Apparel Group na mengi zaidi.
Wadhamini
wa tukio la mwaka huu walikuwa: Wizara ya Mambo ya Ndani, Jamii ya
Autism Emirates, Abu Dhabi Media Company, Emirates Red Crescent, Baraza
la elimu la Abu Dhabi, Braza la michezo la Abu
Dhabi, Kampuni ya maji ya Al Ain, Bustani ya Mushrif, Shirika la Zayed,
Verde, Austin Reed, Glossip Milano, Muungano wa wanawake wa Hindi,
Gossip Café na Desserts, Canon Mashariki ya Kati, wa Kituo cha kimataifa
cha mapumziko na michezo cha Al Forsan, Hospitali ya LLH, Nyumba ya
sanaa ya kisasa Etihad, Kampuni ya uchapishaji ya United, Silkor,
Primavera Medical Rehabilitation LLC, Crowne Plaza na Staybridge Suites
Abu Dhabi Yas Island, Holiday Inn Abu Dhabi, Rosewood Abu Dhabi, Hoteli
ya Royal Rose, Landmark Gulf Group, Kituo cha marekani cha vipaji
maalum, Kituo cha tiba ya meno cha Boston na Mercure Al Ain Grand Jebel
Hafeet.
No comments:
Post a Comment