Matukio : Naibu waziri , Hamad Masauni ziarani mkoani Kigoma - Wazalendo 25 Blog

Breaking

Glory to Story.


Post Top Ad


30 Mar 2016

Matukio : Naibu waziri , Hamad Masauni ziarani mkoani Kigoma

Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati), akisalimiana na wafanyakazi wa Mashirika mbalimbali ya Kitaifa na Kimataifa yanayohudumia wakimbizi katika Kambi ya muda ya NMC, iliyoko mkoani Kigoma, kushoto ni Mratibu wa Wakimbizi Mkoani Kigoma, Tonny Samwel Laiser.Naibu Waziri yupo mkoani Kigoma kwa ziara ya kikazi.
Msimamizi wa Kambi ya muda ya NMC, Jordan Emmanuel (wa kwanza kushoto), akimuonyesha Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, jinsi mfumo wa jiko la kupikia chakula kambini hapo unavyofanya kazi.Naibu Waziri yupo mkoani Kigoma kwa ziara ya kikazi.
Sehemu ya vitanda vipya vikiwa katika moja ya mabweni ya Kambi ya muda ya wakimbizi ya NMC , tayari kwa kufungwa na kuanza kutumika na wakimbizi wanaohifadhiwa kambini hapo.
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati), akizungumza na Mkuu wa Wilaya ya Kakonko, mkoani Kigoma, Peter Toima Kiroya (wa kwanza kushoto), wakati walipotembelea iliyokua kambi ya Karago iliyotumika kuhifadhi wakimbizi.Kulia ni Mkuu wa Kambi ya Wakimbizi Mtendeli, Innocent Mwaka.Naibu Waziri yuko mkoani Kigoma kwa ziara ya kikazi.
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto), akifafanua jambo kwa Mkuu wa Shirika la Kuhudumia Wakimbizi Duniani Ofisi ndogo ya Kibondo, Dost Yousafzai(kushoto), wakati alipotembelea iliyokuwa kambi ya Wakimbizi ya Karago,Wilayani Kibondo mkoani Kigoma.
Mkuu wa Shirika la Kuhudumia Wakimbizi Duniani Ofisi ndogo ya Kibondo,Dost Yousafzai (kushoto), akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(kulia), wakati ya ziara ya Naibu Waziri kutembelea ilipokuwepo kambi ya wakimbizi ya Karago, wilayani Kibondo. Naibu Waziri yuko mkoani Kigoma kwa ziara ya kikazi.
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na wakimbizi wa Burundi (hawapo pichani) wanaoishi katika kambi ya Mtendeli, iliyoko wilayani Kakonko mkoani Kigoma.Naibu Waziri yuko Mkoani Kigoma kwa ziara ya kikazi.(Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)

Post Top Ad