Na Eleuteri Mangi-MAELEZO
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa amemuagiza
Kaimu Meneja Msaidizi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) Nelson Mlali
kufanya uhakiki wa kampuni zinazotoa huduma mbalimbali bandarini ili
kuboresha utendaji kazi na kuepuka mgongano wa maslahi binafsi minongoni
wa watumishi wa bandari.
Profesa
Mbarawa alitoa kauli hiyo baada ya kufanya ziara ya kushtukiza jana
jioni(29/03/2016) kwenye ofisi za Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) eneo
la kupakulia mafuta yanayoingia nchini (KOJ) Kurasini.
“Mtafanyaje
kazi na mtu ambaye ni mfanyakazi na huku kampuni yake inatoa huduma
bandarini, hamuoni kutakuwa na mgongano wa kimaslahi binafsi,” alihoji
Profesa Mbarawa.
Aidha,
Prof. Mbarawa amemtaka Kaimu Meneja Msaidizi Mlali azingatie umiliki wa
makampuni kulingana na taarifa za Wakala wa Usajili wa Biashara na
Kampuni nchini (BRELA) katika zoezi la kuhakiki kampuni hizo.
Akiwa
eneo la (KOJ) Kurasini, Prof. Mbarawa amewataka wafanyakazi wa TPA
wabadilike na kufanya kazi kwa juhudi na maarifa badala ya kufanya kazi
kwa mazoea ili kuboresha kuongeza ufanisi na kuliongezea taifa mapato
kwa manufaa ya wananchi.
Prof.
Mbarawa amewaagiza pia Mamlaka ya Bandari wanaponunua vipuri na vifaa
mbalimbali vinavyohitajika bandarini hapo wazingatie vipimo sahihi
kulingana na vifaa vinavyohitajika kuendeshea mitambo mbalimbali ili
kulipunguzia taifa gharama zisizohitajika.
Mamlaka ya Bandari nchini ina bandari mbalimbali zilizopo katika ukanda wa bahari ya Hindi na maziwa yaliyopo nchini.
Ukanda
wa Bahari ya Hindi una bandari ya kuu za Dar es salaam, Tanga na Mtwara
pamoja na Bandari ndogo zilizopo Lindi, Kilwa Masoko, Mafia, Bagamoyo,
Pangani na Kwale.
Bandari
nyingine ziliozo katika maziwa mbalimbali nchini ni pamoja na Ziwa
Victoria lenye bandari ya Mwanza, Bukoba, Kemondo, Musoma na Nansio,
Ziwa Tanganyika likihusisha bandari ya Kigoma na Kasanga wakati Ziwa
Nyasa kuna bandari ya Itungi, Manda, Liuli na Mbaba Bay.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akiongea na baadhi ya wafanyakazi wa
TPA eneo la kupakulia mafuta yanayoingia nchini (KOJ) Kurasini leo
jijini Dar es salaam. Wa kwanza kulia Mhandisi anayefanya kazi eneo la
KOJ Jabiri Muyones.
Kapteni Abdulla Mwingamno (kulia)
akimuonesha Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame
Mbarawa (kushoto) baadhi ya vifaa vya kituo cha kupakulia mafuta
yanayoingia nchini (KOJ) Kurasini leo jijini Dar es salaam.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akiongozana na Mhandisi anayefanya kazi
eneo la KOJ Jabiri Muyones alipotembelea TPA eneo la kupakulia mafuta
yanayoingia nchini (KOJ) Kurasini leo jijini Dar es salaam.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akikagua baadhi vipuri eneo la
kupakulia mafuta yanayoingia nchini (KOJ) Kurasini leo jijini Dar es
salaam.
Eneo la kupakulia mafuta yanayoingia nchini (KOJ) Kurasini jiji Dar es salaam.(Picha na Eleuteri Mangi-MAELEZO)
No comments:
Post a Comment