Mnadhimu
Mkuu mstaafu wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Luteni Jenerali
Samuel Ndomba (kwenye gari kushoto) na Mkuu wa Vikosi vya Kulinda Amani
Umoja wa Mataifa, Luteni Jenerali mstaafu, Paul Ignas Meela wakitoa
heshima katika hafla ya kuagwa iliyofanyika Viwanja vya Twalipo Mgulani
Dar es Salaam leo mchana. Maofisa Majenerali 16 waliostaafu Utumishi
Jeshini waliagwa.
Brigedia
Jenerali mstaafu, Msangi (kulia mbele), akikagua gwaride maalumu
waliloandaliwa maofisa hao wastafu wakati wakiagwa rasmi baada ya
kumaliza utumishi wao jeshini.
Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), mstaafu Meja Jenerali, Raphael Muhuga, akikagua gwaride hilo.
Wanafamilia wa wastaafu hao wakiwa kwenye hafla hiyo ya kuagwa jamaa zao.
Ukaguaji gwaride rasmi ukiendelea.
Maofisa hao wastaafu wakiwa jukwaa kuu.
Hapa maofisa hao wakiwa wamesimama wakati gwaride likipita jukwaa kuu na kutoa heshima.
Mkuu wa Majeshi, Jenerali, Davis Mwamunyange (kushoto), akisalimiana na kumpongeza Mkuu wa Vikosi vya Kulinda Amani Umoja wa Mataifa, Luteni Jenerali mstaafu, Paul Ignas Meela katika hafla hiyo.
Askari wa JWTZ wakifuatia matukio mbalimbali kwenye
hafla hiyo.
Gwaride likipita mbele ya jukwaa kuu kutoa heshima.
Wapiga picha wa magazeti wakiwa kazini kuchukua matukio mbalimbali.
Taswira ya jukwaa kuu katika hafla hiyo.
Wastaafu hao wakiwa katika picha ya pamoja na mkuu wa majeshi.
Mkuu
wa majeshi, Davis Mwamunyange (katikati), akiwa katika picha ya pamoja
na wakuu wa majeshi wastaafu. Kushoto Robert Mboma na George Waitara
(kulia).
Mkuu wa majeshi akiwa katika picha ya pamoja na familia ya Mnadhimu Mkuu wa JWTZ, Luteni Jenerali, Samuel Ndomba.
Hapa ni furaha tupu kwa kustaafu utumishi ndani ya jeshi.
Askari wa JWTZ wakiwa imara wakati wa kuwaaga maofisa hao.
Hapa ni saluti wakati wakiwaaga wapiganaji wenzao.
Na Dotto Mwaibale
JESHI
la Wananchi Tanzania (JWTZ), limewaaga Mameja generali, Luteni na
Brigedia Generali 16, akiwemo, aliyekuwa Msaidizi wa Mkuu wa Majeshi ya
Ulinzi na Usalama, Luteni Generali Samwel Ndomba.
Tukio
la kuwaaga majenerali hao ambao wamestaafu utumisho wao jeshini
limefanyika jijini Dar es Salaam leo katika viwanja Twalipo Mgulani saa
tatu hadi saa tatu asubuhi ambapo liliambatana na gwaride maalumu la
vikosi mbalimbali vya Anga, nchini kavu, majini pamoja na Jeshi la
Kujenga Taifa (JKT).
Hafla
hiyo ya kuwaaga Magenerali hao iliongozwa na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi
na Usalama (CDF), Davis Mwamunyange ambapo waaga hao ni wa vyeo
mbalimbali vya Brigedia Generali waliokuwa nane, Meja Jenerali sita na
Luteni wawili na kuhudhuliwa na viongozi mbalimbali na wastaafu wa jeshi
hilo.
Majenerali
hao kila mmoja alipata fursa ya kukagua gwaride kila alipowasili
viwanjani hapo ambapo kati yao ni Luteni Generali walipata heshima ya
pekee na kufanyiwa gwaride lililokuwa tofauti na wengine.
Majenerali
hao ni Mnadhim Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama JWTZ, Luteni
Jenerali Samwel Ndomba ambaye pia aliwahi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Ngara,
Mkuu wa Utumishi katika jeshi hilo na Mkuu wa Mkoa wa Arusha.
Wengine
ni Mkuu wa Tawi la Usalama na Utambuzi jeshini, Luteni Jeneral Paul
Ignas ambaye pia aliwahi kuwa ni Mkuu wa Mjeshi ya kulinda amani Darfur
nchini Sudani.
Kwa
upande wa Mameja Jenerali ambao walipewa heshima na kukagua vikosi
hivyo ni Mkuu wa Jeshi la Nchi kavu, Meja Jenerali Salum Kijuu, Mkuu wa
Utumishi Jeshini, Meja Jenerali Vicent Mlitaba, Mkuu wa Jeshi la Anga,
Meja Jenerali Joseph Kapwani, Mkuu wa Chuo cha Ukamanda na Unadhimu
kilichopo Duruti mkoani Arusha Meja Jenerali Ezekiel Kiunga.
Wengine
ni Mkuu wa Shirika la Mzinga mkoani Morogoro, Meja Jenerali Charles
Mzanila, Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Raphael
Mhunga.
Na
wengine ambao ni Mabrigedia ni Mkuu wa Chuo cha Kijeshi cha Sayansi ya
Tiba Lugalo, Brigedia Jenerali Dk.Luhindi Msangi , Mkuu Tawi la Ukaguzi
jeshini ambaye pia aliwahi kuwa mkaguzi wa majeshi ya SADC, Brigedia
Jenerali Emanuel Maganga.
Wengine
ni Mkuu wa Tawi la Akiba, Brigedia Jenerali Agustino Gailanga ambaye
pia aliwahi kuwa mpambe wa Rais mstaafu, Benjamin Mkapa, Mratibu wa
Miradi ya Maendeleo Jeshini, Brigedia Jenerali Mrisho Abdallah , Mkuu wa
Kikosi cha Ndege cha usafirishaji, Brigedia Jenerali Ezra Ndimugwango.
Na
wengine ni Kamanda wa Brigedi ya Tembo mkoani Songea, Brigedia Jenerali
John Chacha, Mkurugenzi wa Mahusiano ya Kimataifa jeshini, Brigedia
Jenerali Martini Mwankanye na Mkuu wa Shule ya 'Eflantria' mkoani
Arusha, Brigedia Harodi Mzirai.
Akizungumza
mara baada ya hafla hiyo Luteni Jenerali mstaafu Ndumba alifurahia
hatua hiyoa na kubainisha kuwa kwa sasa wanaenda kuanza maisha mapya.
(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com.
No comments:
Post a Comment