Michezo : Taswira mbalimbali ya mtanange wa Simba na Yanga uliopigwa uwanja wa Taifa ,Jijini Dar - Wazalendo 25 Blog

Breaking

Glory to Story.


Post Top Ad


22 Feb 2016

Michezo : Taswira mbalimbali ya mtanange wa Simba na Yanga uliopigwa uwanja wa Taifa ,Jijini Dar

 Mbunge wa Jimbo la Kilolo mkoani Iringa, Mhe. Venance Mwamoto akifuatilia mchezo kati ya Yanga Afrika na Simba SC uliofanyika katika Uwanja wa Taifa leo jijini Dar es Salaam. Hadi dakika 90 zinayoyoma Simba SC ililala kwa mabao 2 : 0.
 Mashabiki wa Timu ya Yanga Afrika  wakifuatilia mchezo kati yao na Simba SC uliofanyika katika Uwanja wa Taifa leo jijini Dar es Salaam.Hadi dakika 90 zinayoyoma Simba SC ililala kwa mabao 2 : 0. Picha na: Frank Shija,WHUSM
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akisalimiana na mashabiki wa mpira wa miguu wakati wa mchezo wa watani wa jadi kati ya Yanga Afrika na Simba Sports Club katika Uwanja wa Taifa  jijini Dar es Salaam.
 Mashabiki wa Timu ya Simba SC wakifuatilia mchezo kati yao na Yanga Afrika uliofanyika katika Uwanja wa Taifa leo jijini Dar es Salaam. Hadi dakika 90 zinayoyoma Simba SC ililala kwa mabao 2 : 0.
  Mabeki wa Timu ya Simba wakiokoa mpira wa hatari katika lango lao wakati wa mechi dhidi ya Yanga iliyochezwa katika Uwanja wa Taifa  jijini Dar es Salaam.Mechi hiyo imeisha kwa wenyeji Yanga Afrika kuibuka kidedea kwa mabao 2:0.
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akisalimiana na Naibu Waziri wake Mhe. Annastazia James Wambura walipokutana katika mchezo wa watani wa jadi kati ya Yanga Afrika na Simba Sports Club katika Uwanja wa Taifa leo jijini Dar es Salaam.Katikati ni Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akisalimiana na Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba (kushoto)walipokutana katika mchezo wa watani wa jadi kati ya Yanga Afrika na Simba Sports Club katika Uwanja wa Taifa  jijini Dar es Salaam.
Mchezaji wa Timu ya Simba Kona kuelekea katika lango la watani wao Yanga wakati wa mechi ya Ligi Kuu iliyochezwa katika Uwanja wa Taifa leo jijini Dar es Salaam.Mechi hiyo imeisha kwa wenyeji Yanga Afrika kuibuka kidedea kwa mabao 2:0.
Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba akishangilia mara baada ya Donald Ngoma kuiandikia Yanga bao la kwanza mnamo Dakika ya 38 ya mchezo uliofanyika katika Uwanja wa Taifa  jijini Dar es Salaam. Hadi dakika 90 zinayoyoma Simba SC ililala kwa mabao 2 : 0.

Post Top Ad