Matukio : Waajiri walalamikia rushwa kukwamisha Biashara - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Thursday, 4 February 2016

demo-image

Matukio : Waajiri walalamikia rushwa kukwamisha Biashara


IMG_8068
 Mkurugenzi wa chama cha waajiri Tanzania (ATE) Agrey Mlimka  akifafanua jambo katika mkutano wa siku moja wa kujadili changamoto mbalimbali zinazo wakabili waajiri mkutano uliowashirikisha  waajiri kutoka katika sekta mbalimbali uliofanyika ndani ya hotel ya Kibo palace jijini Arusha
IMG_8070


IMG_8076


IMG_8077


IMG_8060
 wanachama wa chama cha waajiri pamoja na wasio wanachama wa  wakiwa wanajadili  kwa makini changamoto ambazo zinawakabili waajiri na jinsi ya kuzitatua .
IMG_8059
Na Woinde Shizza,Arusha
Chama cha Waajiri nchini kimelalamikia vitendo vya rushwa kuwa vikwazo katika biashara hivyo wameiomba serikali kukemea vitendo vya rushwa pamoja na urasimu ili kuboresha mazingira mazuri ya biashara za kitaifa na kimataifa.

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mkuu wa  Chama cha Waajiri (ATE),Aggrey Mlimuka  akizungumza katika Mkutano Mkuu wa Waajiri amesema kuwa serikali inapaswa kujenga mazingira bora kwa waajiri wanaotoa nafasi za  ajira ili kujenga uchumi endelevu wa nchi 


Mkurugenzi huyo ameiomba serikali iondoe vikwazo kwa waajiri wanaoajiri wataalamu kutoka nje kutokana na kukosekana kwa wataalamu hao nchini pamoja na kupunguza tozo kubwa za mafunzo ya wafanyakazi ambayo ni asilimia 5%.

Kwa upande wake Afisa Mwajiri wa Kampuni ya Utalii amesema kuwa kwa muda mrefu wamekua wakipata adha kubwa wakati wa kuajiri watu kutoka nje ya nchi suala ambalo serikali inatambua kuwa baadhi ya taaluma hazipatikani nchini hivyo kulazimika kuchukua wataalamu kutoka nje.

No comments:

Post a Comment

Tuwasiliane

Name

Email *

Message *

Contact Form

Name

Email *

Message *