Mke
wa Rais Mama Janeth Magufuli akiweka saini katika kitabu cha wageni
mara baada ya kuwasili katika Kituo cha Makazi ya Wazee na Watu Walemavu
cha Nunge,
Kigamboni,
jijini Dar es salaam alikotembelea na kusikiliza mahitaji yao pamoja na
kutoa msaada wa mchele kilo 3000, Unga kilo 3000 na Maharage Kilo 1200
ikiwa msaada wake kwa wazee na walemavu hao.
Mke
wa Rais Mama Janeth Magufuli akisikiliza taarifa kutoka kwa Bw. Ojuku
Mgedzi, Mkuu wa Kituo cha Makazi ya Wazee na Watu Walemavu cha Nunge,
Kigamboni,
jijini Dar es salaam alikotembelea na kusikiliza mahitaji yao pamoja na
kutoa msaada wa mchele kilo 3000, Unga kilo 3000 na Maharage Kilo 1200
ikiwa msaada wake kwa wazee na walemavu hao.
Mke
wa Rais Mama Janeth Magufuli akipokea taarifa kutoka kwa Bw. Ojuku
Mgedzi, Mkuu wa Kituo cha Makazi ya Wazee na Watu Walemavu cha Nunge,
Kigamboni,
jijini Dar es salaam alikotembelea na kusikiliza mahitaji yao pamoja na
kutoa msaada wa mchele kilo 3000, Unga kilo 3000 na Maharage Kilo 1200
ikiwa msaada wake kwa wazee na walemavu hao.
Mke
wa Rais Mama Janeth Magufuli akikabidhiwa taarifa Bw. Ojuku Mgedzi,
Mkuu wa Kituo cha Makazi ya Wazee na Watu Walemavu cha Nunge,
Kigamboni,
jijini Dar es salaam alikotembelea na kusikiliza mahitaji yao pamoja na
kutoa msaada wa mchele kilo 3000, Unga kilo 3000 na Maharage Kilo 1200
ikiwa msaada wake kwa wazee na walemavu hao.
Mke
wa Rais Mama Janeth Magufuli akioneshwa maeneo mbalimbali na Bw. Ojuku
Mgedzi, Mkuu wa Kituo cha Makazi ya Wazee na Watu Walemavu cha Nunge,
Kigamboni,
jijini Dar es salaam alikotembelea na kusikiliza mahitaji yao pamoja na
kutoa msaada wa mchele kilo 3000, Unga kilo 3000 na Maharage Kilo 1200
ikiwa msaada wake kwa wazee na walemavu hao.
Mke
wa Rais Mama Janeth Magufuli akisalimiana na wagonjwa waliofika kupata
huduma katika zahanati ya Kituo cha Makazi ya Wazee na Watu Walemavu cha
Nunge,
Kigamboni,
jijini Dar es salaam alikotembelea na kusikiliza mahitaji yao pamoja na
kutoa msaada wa mchele kilo 3000, Unga kilo 3000 na Maharage Kilo 1200
ikiwa msaada wake kwa wazee na walemavu hao.
Mke
wa Rais Mama Janeth Magufuli akitembelea chumba cha kujifungulia cha
zahanati ya Kituo cha Makazi ya Wazee na Watu Walemavu cha Nunge,
Kigamboni,
jijini Dar es salaam alikotembelea na kusikiliza mahitaji yao pamoja na
kutoa msaada wa mchele kilo 3000, Unga kilo 3000 na Maharage Kilo 1200
ikiwa msaada wake kwa wazee na walemavu hao.
Mke
wa Rais Mama Janeth Magufuli akisalimiana kwa furaha na wakaazi wa
Kituo cha Makazi ya Wazee na Watu Walemavu cha Nunge, Kigambo ni, jijini
Dar es salaam alikotembelea na kusikiliza mahitaji yao pamoja na kutoa
msaada wa mchele kilo 3000, Unga kilo 3000 na Maharage Kilo 1200 ikiwa
msaada wake kwa wazee na walemavu hao.
Mkuu
wa wilaya ya Temeke Mhe Sophia Mjema akimkaribisha Mke wa Rais Mama
Janeth Magufuli kuhutubia wakaazi wa Kituo cha Makazi ya Wazee na Watu
Walemavu cha Nunge, Kigambo ni, jijini Dar es salaam alikotembelea na
kusikiliza mahitaji yao pamoja na kutoa msaada wa mchele kilo 3000, Unga
kilo 3000 na Maharage Kilo 1200 ikiwa msaada wake kwa wazee na walemavu
hao.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akihutubia wakaazi wa Kituo cha Makazi ya Wazee na Watu Walemavu cha Nunge,
Kigambo
ni, jijini Dar es salaam alikotembelea na kusikiliza mahitaji yao
pamoja na kutoa msaada wa mchele kilo 3000, Unga kilo 3000 na Maharage
Kilo 1200 ikiwa msaada wake kwa wazee na walemavu hao.
Mke
wa Rais Mama Janeth Magufuli akimkabidhi mchele, unga na maharage Mzee
Anthony Kingongoti Mwenyekiti wa wakaazi wa Kituo cha Makazi ya Wazee na
Watu Walemavu cha Nunge,
Kigambo
ni, jijini Dar es salaam alikotembelea na kusikiliza mahitaji yao
pamoja na kutoa msaada wa mchele kilo 3000, Unga kilo 3000 na Maharage
Kilo 1200 ikiwa msaada wake kwa wazee na walemavu hao.
Mke
wa Rais Mama Janeth Magufuli akipokea shukurani kutoka kwa Mzee Anthony
Kingongoti Mwenyekiti wakaazi wa Kituo cha Makazi ya Wazee na Watu
Walemavu cha Nunge,
Kigambo
ni, jijini Dar es salaam alikotembelea na kusikiliza mahitaji yao
pamoja na kutoa msaada wa mchele kilo 3000, Unga kilo 3000 na Maharage
Kilo 1200 ikiwa msaada wake kwa wazee na walemavu hao.
Mke
wa Rais Mama Janeth Magufuli akimshukuru Mzee Anthony Kingongoti
Mwenyekiti wakaazi wa Kituo cha Makazi ya Wazee na Watu Walemavu cha
Nunge,
Kigambo
ni, jijini Dar es salaam alikotembelea na kusikiliza mahitaji yao
pamoja na kutoa msaada wa mchele kilo 3000, Unga kilo 3000 na Maharage
Kilo 1200 ikiwa msaada wake kwa wazee na walemavu hao.
PICHA NA IKULU
Na Magreth Kinabo –MAELEZO
MKE
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mama Janeth Magufuli
ameziomba na kuzimahamasisha taasisi za Serikali na zisizo za Serikali
kushirikiana na Serikali kutatua changamoto mbalimbali zinazozikabili
Kituo cha Makazi ya Wazee na Watu Walemavu Wasiojiweza kijulikanacho kwa
jina la Nunge,viwemo vingine.
Aidha alisema vituo hivyo jumla vipo 17, katika maeneo mbalimbali nchini.
Kauli
hiyo imetolewa leo na Mama Magufuli wakati alipotembelea makazi hayo
yaliyoko Kigamboni eneo la Vijibweni jijini Dares Salaam, ambapo alisema
changamoto wanazokabiliana nazo amezisikia na na aliwaahidi kuwa
atashirikiana na wadau wote kuzitafutia majibu yake.
Mama
Magufuli alizitaja baadhi ya changamoto hizo, ni kuwa uchakavu wa
miundombinu, uhaba wa rasilimali fedha na watu, pamoja na maslahi duni
ya watoa huduma, upungufu wa vitendea kazi na huduma za jamii, pamoja na
uvamizi wa eneo la kituo.
Aidha
Mama Magufuli alimwomba Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema
kulishughulikia taizo la uvamizi wa eneo hilo na kulitafutia ufumbuzi.
“
Natumainni zawadi tuliyoileta ni ndogo na haiwezi kumaliza matatizo
yote mliyonayo. Lakini ni matumaini yangu kuwa zawadi hii inaweza kuwa
chachu ya kuhamsha hamasa ya watu na vikundi vingine kujitoa kusaidia
watu wasiojiweza. Ni imani yangu kuwa endapo watu wote tutajitoa kwa
dhati tutaweza kuwahudumia wazee na watu wasiojiweza na hivyo
kuwapunguzia makali ya maisha .
Tukumbuke ‘kutoa ni moyo na si utajiri’ na kwamba “sisi sote ni wazee na walemavu watarajiwa”.
Aliongeza kwamba ni dhahiri kuwa Serikali ina wajibu mkubwa katika
kuhudumia wazee na watu wasiojiweza. Hata hivyo Serikali pekee haiwezi
kumaliza matatizo yote yanayowakabili na wazee na watu wasiojiweza.
Hivyo basi, sote kwa pamoja tunao wajibu wa kusaidia nguvu za Serikali katika kuwahudumia watu hao.
“Na
kwa kutambua hilo , mimi na wenzangu niliombatana nao tumeamua kutoa
zawadi yetu ndogo kwenu. Zawadi hiyo inajumuisha vitu vifuatavyo mchele
kilo 3000, unga kilo 3000 na maharage kilo 1200. Kulingana na idadi yenu
niliyopewa kila mmoja atapewa kilo 25za mchele, kilo 25 za unga na kilo
10 za maharage.
“Nawaombeni
mniruhusu pia kuchukua nafasi hii kuwasilisha kwenu salamu nyingi
kutoka kwa Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania. Ameniomba niwaarifu kuwa yupo pamoja nayi na
kwamba Serikali itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali katika
kuhakikisha wazee na watu wasiojiweza wanapata huduma zote muhimu kwa
kadri ya uwezo wake,” alisisitiza Mama Magufuli.
Mama
Magufuli aliongeza kwamba wazee na watu wasiojiweza wanahitaji upendo,
kuthaminiwa nakusaidiwa.Hivyo kipimo kimojawapo cha kupima jamii
iliyostaarabika na inayoheshimu misingi ya utu ni kuangalia namna inavyo
wathamini wazee na watu wasiojiweza.
Aliupongeza
uongozi na watumishi wote wa kituo hicho na vituo vingine nchini kwa
kazi kubwa wanayoifanya licha ya kukabiliwa na changamoto kadhaa.
Kwa
upande wake Mkuu wa Wilaya ya Temeke , Sophia Mjema alimtaka kila
mwananchi kutambua kwamba bila wazee hakuna tutakachoweza kufanya hivyo
ni muhimu kuwa enzi na kuwasaidia wazee walioko majumbani na mitaani.
“
Tuwaenzi wazee na kuwasaidia pia hata wale walioko mitaani tuwashauri
warudi majumbani ili Serikali iweze kuwaorozesha kwa kuwa si vizuri
kukaa barabarani, Serikali ya Awamu ya Tano ya Rais Magufuli
itahakikisha inawajali wazee,” alisema.
Akizungumzia
kuhusu watoto wa mitaani alisemani wajibu wa wazazi kuhakikisha
wanawalea watoto wao vizuri ili wasikilimbile mitaani kwa kuwa watoto ni
taifa la kesho.
Naye Mwenyekiti wa wazee wa makazi hayo, Anthony Kikongoti
alimshukuru Mama Magufuli kwa niaba ya wenzake, kwa kuanza ziara yake ya
kwanza ya kutembelea kituo hicho ,ambapo alimwomba apeleke salamu zao
kwa baba yao ambaye ni Rais Magufuli kuwa wanasema asante.
“Huu ni mwaka wa wanyonge dini zote tumwombee kwa pamoja ili aweze kuendelea kupunguza makali ya maisha,” alisema.
Afisa
Mfawidhi wa kituo hicho, Ojuku Mgedzi alisema wanahitaji bajeti ya
kutosha ya kuendesha shughuli mbalimbali, watumishi 42 , wakiwemo
walinzi, kwa kuwa waliopo sasa ni 29 na hawatoshi.
Alisema eneo hilo lina hekari 50.8 na nusu ya eneo hilo limevamiwa.
Mgedzi alisema kituo hicho kina idadi yawakazi 112, ambapo alimkabidhi Mama Magufuli orodha ya idadi ya watu hao.
No comments:
Post a Comment