Maisha : NHIF Yatumia Mtandao wa Simu kuwasilisha taarifa za mama mjamzito na watoto wachanga - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


4 Feb 2016

Maisha : NHIF Yatumia Mtandao wa Simu kuwasilisha taarifa za mama mjamzito na watoto wachanga

 Afisa Mradi wa KFW kutoka Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF),Francis Mbwana akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo kwa watoa huduma wa Afya ya Mama na Mtoto kutoka katika vituo mbalimbali vya Afya mkoani Tanga iliyofanyika ukumbi wa mkuu wa mkoa.
 Kaimu Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Mkoani Tanga,Dinna  Mlwilo  akisisitiza jambo wakati wa ufunguzi wa mafunzo kwa watoa huduma wa Afya ya Mama na Mtoto,uliofanyika kwenye
ukumbi wa mkuu wa mkoa Tanga.

watoa huduma za afya ya mama na mtoto kutoka katika vituo mbalimbali vya afya mkoani Tanga wakati wa ufunguzi wa mafunzo kwa watoa huduma wa Afya ya Mama na Mtoto,uliofanyika kwenye ukumbi wa mkuu wa mkoa Tanga.

Na Assenga Oscar, Tanga.
MFUKO wa bima ya afya kupitia mradi wake wa KFW umeanza kutoa elimu
kwa wahudumu wa afya ya mama na mtoto namna ya   kutumia mitandao ya
simu kuwasilisha  taarifa za afya mama mjamzito na mtoto mchanga.

Hatua hiyo inalengo la kuhakikisha wanapunguza ikiwemo na kuzuia kwa
kiasi kikubwa changamoto ya vifo vya wajawazito pamoja na watoto wa
changa nchini kote.

Hayo yamebainishwa na Afisa Mradi wa KFW mkoa wa Tanga Francis Mbwana
wakati wa ufunguzi wa mafunzo kwa wahudumu wa afya ya mama na mtoto
kutoka katika vituo mbalimbali vya afya mkoani hapa.

Alisema kuwa utaratibu huo wa kutumia teknolojia ya simu katika
kusajili na kufuatilia hali za afya za mama wajawazito na watoto
zitasaidi kupata taarifa za maendeleo ya afya zao mapema tofauti na
sasa.

“Kupitia mradi huu wa KFW muda mwingi fomu za wanachama wapya zilikuwa
zinachelewa kutufikia ,huku wakati mwingine mjamzito anakuwa katika
hali ya hatari tunashindwa kumfuatilia kwa wakati lakini kupiti njia
ya simu tutaweza kufanya malipo na ufuatiliaji kwa haraka”alibainisha
Mbwana.

Aliongeza kuwa lengo la mradi ni kuhakikisha  wajawazito wote nchini
wanapata fursa ya kujiunga na huduma hiyo hususani maeneo ya vijijini
ili kuhakikisha wanapata fursa ya kufaidika na mradi huo.

Nae mmoja wa Wauguzi wa afya Ester Kimweri alisema kuwa toka KFW ianze
miaka miatau iliyopita mahudhurio ya wajawazito yamekuwa yakiongezeka
kila siku tofauti na hapo awali.

“Mpango wa KFW umesaidia wajawazito wengi kuona umuhimu wa
kujifunguali katika vituo vya afya,zahanati  na hospitali tofauti na
hapo awali mahudhurio yalikuwa ni madogo”alisema Kimweri.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad