Baadhi ya Askari jeshi la Polisi wa kikosi usalama barabarani wakiongozwa na Msaidizi wa meneja miradi ya Tehama ndani ya Jeshi la Polisi hilo, Inspekta Bakari Mwamgugu (kushoto) wakiwafuatilia taarifa za magari ambayo madereva wake wamekwisha fanya makosa mbalimbali wakati wa zoezi la ukaguzi na ulipaji wa faini mbalimbali jijini Dar es Salaam Januari 15 2016. |
Msaidizi wa meneja miradi ya Tehama ndani ya Jeshi la Polisi Tanzania, Inspekta Bakari Mwamgugu akiweka alama ya kituo cha ukaguzi wakati mbele ya kamera maalum ya kuchukuwa taarifa za magari ambayo madereva wake wamekwisha fanya makosa mbalimbali wakati wa zoezi la ukaguzi na ulipaji wa faini mbalimbali jijini Dar es Salaam Januari 15 2016. |
Polisi wa usalama barabarani Happy Kataraia na Msaidizi wa meneja miradi ya Tehama ndani ya Jeshi la Polisi Tanzania, Insp Bakari Mwamgugu wakiweka sawa kamera ya kuchukuwa taarifa za magari ambayo madereva wake wamekwisha fanya makosa mbalimbali wakati wa zoezi la ukaguzi na ulipaji wa faini mbalimbali jijini Dar es Salaam Januari 15 2016. |
Na Mwandishi Wetu.
Kikosi cha Usalama Barabarani kimefanikiwa kuwalipisha faini madereva na
wamiliki wa vyombo vya moto hususani magari kwa asilimia 49 kwa kutumia
mfumo kutumia mfumo mpya maalum wa taarifa za kielekroniki jijini Dar
es Salaam.
Mfumo
huo unasimamia sheria za usalama barabarani kwa njia ya kieletroniki
sambamba na ukusanyaji wa tozo za makosa ya barabarani kwa njia ya
kieletroniki.
Kwa
kutumia mfumo huo jeshi la polisi limefanikiwa kuyakamata magari ambayo
yana makosa mbalimbali yakiwemo ya TRA na SUMATRA.
Pia mfumo unatambua na kuwabaini wale wote ambao hawajalipia faini za
makosa yao ya usalama barabarani Kwa kutumia kamera maalum ya
kuwabaini..
Mkaguzi
wa Polisi wa Kikosi hicho, Bakari Mwangungu alisema jana kuwa kwa
kutumia mfumo huo huduma za usalama barabarani zimeendelea kuboreshwa na
kufanikiwa kuwalipisha faini madereva na wamiliki wa magari waliokuwa
na mtindo wa kukwepa ama kuchelewa kulipia faini hizo kwa wakati kwa
mujibu wa sheria za usalama barabarani.
Zaidi
ya makosa 12,000 yamelipiwa faini kwa kutumia mfumo huo ambapo asilimia
51 hayajalipwa na zoezi la ukaguzi linaendelea kuhakikisha wale wote
wenye makosa na wanaendelea kutenda makosa ya usalama barabarani
wataendelea kuchukuliwa hatua ili kuhakikisha madereva wanaendelea kuwa
na nidhamu na kujirekebisha ili kuongeza umakini wawapo barabarani.
Alisema
wananchi wanashindwa kuelewa swala la adhabu za makosa wa wanalipia
nusu nusu na kwa kuwa mfumo autambui na hivyo kurudisha fedha kwa
mlipaji mpaka atakapolipia kiasi kamili ndipo mfumo utamtambua na
kumpatia risiti.
Inspector
Mwangungu amewatahadharisha wananchi kutokosea namba za kumbukumbu
wafanyapo malipo ili kuepuka usumbufu utakaosabishwa na kurudishwa ama
kukamilisha malipo ya faini zao.
Ameongeza
kwamba zoezi hilo ni endelevu na linasaidia kupunguza kero ya risiti
kwani kwa kutumia mfumo wanazipata moja kwa moja kwenye mtandao.
Pia
amebainisha faida za mfumo huo kuwa ni pamoja na kuongeza wigo wa
wananchi wa kutumia Tigo Pesa, Airtel Money na M-pesa ambapo
amewatahadharisha kutosubiri mpaka muda wa siku saba za faini kupita ili
kuepusha usumbufu wa kulipia faini pamoja na faini ya uchelewashaji wa
malipo.
Mfumo
huo ulizinduliwa Disemba mwaka jana na umeonesha mafamanikio makubwa kwa
kuongeza makusanyo ya malipo ya serikali pia kuwarahisishia wananchi
kuepusha usumbufu wa kupewa risiti kama zamani ambapo ilibidi
wakamilishe kwa kufiki vituo vya polisi.
No comments:
Post a Comment