Waziri
wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa amewataka
makandarasi wanaojenga barabara za Mangaka-Mtambaswala KM 62.7 na
Mangaka-Nakapanya Km 70,5 kukamilisha ujenzi huo ifikapo Juni mwaka huu.
Amewataka
makandarasi hao kuongeza rasilimali watu na vifaa ili ujenzi huo
ukamilike kama ilivyopangwa katika mkataba wa ujenzi wake.
“Hakuna
muda utakaoongezwa nataka miradi yote miwili iwe imekamilika ifikapo
juni mwaka huu tena iwe kwenye ubora unaowiana na thamani ya
fedha,”amesema Waziri Prof. Mbarawa.
Barabara
hizo ambazo ujenzi wake kwa kiwango cha lami ulianza mwaka 2014
zitafungua fursa za kiuchumi mkoani Mtwara ikiwemo kuiunganisha Tanzania
na Msumbiji kwa lami kupitia daraja la umoja lililoko Mtambaswala.
Akizungumza
katika ziara hiyo Meneja wa Wakala wa Barabara TANROADS mkoa wa Mtwara
Eng. AISHA SALIM amesema hawata kubali maombi yoyote ya kuongeza muda wa
ujenzi wa barabara hizo ambapo ujenzi wa barabara ya Mangaka
–Mtambaswala Km 62.7 unatarajiwa kukamilika mwezi Mei na ule wa
Mangaka-Nakapanya KM 70.5 ukitarajiwa kukamilika mwezi julai mwaka huu.
Mapema
Prof. Mbarawa alikagua hali ya barabara wilayani Ruangwa,Nachingwea na
Masasi na kusisitiza kuwa ujenzi wa barabara na madaraja katika wilaya
hizo utaendelea katika kipindi kifupi baada ya Serikali kuanza kutoa
fedha kwa miradi inayotumia fedha za Mfuko wa Barabara (RFB).
Waziri
Mbarawa yuko katika ziara ya mikoa ya lindi na mtwara kukagua miradi ya
Barabara,Mawasiliano na Bandari ili kuona ufanisi uliopo katika sekta
hizo.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano,Profesa Makame Mbarawa akiweka saini
kwenye kitabu cha kumbukumbu mara alipowasili Mkoani Lindi kwa Ziara
ya Kukagua miradi inayotekelezwa na Wizara hiyo.Kulia ni ni Bi.Mariam
Mtima Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano,Profesa Makame Mbarawa akipokea
taarifa ya Ujenzi wa barabara ya Mangaka-Mtambaswala (KM 62.7), kutoka
kwa Mhandisi Mkazi Anold Msengezi (Katikati) anayesimamia ujenzi wa
barabara hiyo.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa akitoa
maelekezo juu ya Ujenzi wa barabara ya Mangaka-Mtambaswala (KM 62.7),
ambapo amemtaka Mkandarasi kukamilisha Ujenzi huo kwa wakati na ubora
unaokusudiwa.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (Wa kwanza
kulia) akipokea taarifa ya Ujenzi wa barabara ya Mangaka –Nakapanya
(KM70.5) kutoka kwa Mhandisi mkazi Dkt.Chaurasia inayojengwa na kampuni
ya Jiangxi Geo Engineering (Group) Cooperation ya China.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa akisalimiana
na wakazi wa Nakapanya alipopita kukagua bujenzi wa barabara ya
Mangaka-Mtambaswala (KM 62.5).
Sehemu ya barabara ya Mangaka –Mtambaswala (KM 62.5) ambayo Ujenzi wake unaendelea kwa kiwango cha lami.
Tingatinga
likiwa linaendela na kazi za ujenzi barabara ya Mangaka –Mtambaswala
(KM 62.5) ambayo Ujenzi wake unaendelea kwa kiwango cha lami.
No comments:
Post a Comment