Bi.
Janet Sosthenes Mwenda (wa pili kushoto) akimkabidhi Mkurugenzi wa kituo
cha Watoto Wetu Tanzania, Bw. Evans Tegete moja ya vitu
vilivyowasilishwa kwenye kituo hicho ndoo ya sabuni ya unga. Kushoto ni
Muhamasishaji na mchangishaji fedha wa “Mentoring and Networking”, Bi.
Mary Sanga na wengine wanaoshuhudia ni watoto wa kituo hicho. (Picha
zote na Andrew Chale, Modewjiblog).
Mmiliki
na Mwendeshaji wa kipindi cha ‘Ongea na Janet’ Bi. Janet Sosthenes
Mwenda ambaye pia ni mmiliki wa programu maalum ya vipindi vya watoto
katika kutoa elimu katika televisheni kiitwacho ‘Tuwalinde Watoto Wetu’
kwa kushirikiana na marafiki zake wa kundi la “Mentoring and Networking”
kupitia mitandao ya kijamii wametoa misaada mbalimbali ya vyakula na
vinywaji kwa kituo cha Watoto Wetu Tanzania.
Akizungumza
wakati wa kutoa misaada hiyo mapema jana 17 Januari, wakati wa tukio
hilo lililofanyika kwenye kituo hicho kilichopo Kimara jijini Dar es
Salaam, Janet Mwenda ambaye aliambatana na baadhi ya marafiki zake hao
wa “Mentoring and Networking” wameweza kutoa misaada hiyo ya vyakula,
vinywaji ambavyo vitasaidia kituo hicho.
“Kwa
kuja hapa kutoa msaada huu ni kutokana na kuguswa na hali ya watoto
wanaolelewa hapa na kwingineko kote. Naamini msaada huu utasaidia watoto
wetu hapa kituoni naamini kwa hiki kidogo kitasaidia kwa siku kadhaa”
alieleza Janet Mwenda.
Janet
Mwenda ameongeza kuwa, amekuwa akifikiria zaidi kutoa misaada hivyo
kufika hapo ni kutokana na kuguswa kwake kwa muda mrefu na amekuwa pia
akitembelea kituo hicho kipindi cha nyuma hivyo kuwa miongoni mwa
wanafamilia.
Kwa
upande wake Muhamasishaji na mchangishaji fedha wa “Mentoring and
Networking”, Bi. Mary Sanga ambaye aliambatana na Janet Mwenda katika
kituo hicho ametoa wito kwa jamii kujitokeza kusaidia watoto wanaolelewa
kwenye vituo kama hivyo na kuchangia chochote walicho nacho.
Pia
amepongeza watu mbalimbali kwa kuguswa na hali ya watoto wanaolelewa
kwenye vituo hivyo ameomba waendelee kujitokeza zaidi pindi wanapoguswa
na masuala ya kusaidia jamii isiyo jiweza.
Naye
Mkurugenzi wa kituo hicho, Ndugu Evans Tegete akitoa neno la shukrani
mara baada ya kupokea msaada huo ambapo alishukuru kwa kuguswa kwa Janet
Mwenda na marafiki zake kwani hadi sasa kituo hicho hakina Mfadhili wa
kudumu zaidi wakitegemea kuendesha kituo kwa michango ya misaada ya watu
mbalimbali wanaofika kituoni hapo.
“Tunashukuru
kwa msaada huu. Kwani ni mkubwa sana na utasaidia kuendesha kwa siku
kadhaa ndani ya kituo chetu. Kituo chetu kwa sasa tuna watoto na vijana
zaidi ya 89 wakiwemo wale wanaosoma shule za Bweni na wa kutwa ambao
wapo hapa kituoni.” Alieleza Mkurugenzi huyo.
Pia
alieleza kuwa changamoto mbalimbali zinawakabili ikiwemo suala la ada za
shule kwa watoto na vijana waliochini ya kituo hicho.
Kituo
hicho kinacholea Watoto na vijana wa mitaani na wanaoishi katika
mazingira magumu kina jumla ya watoto pamoja na vijana 120 kilianzishwa
mnamo mwaka 1998 Kwa lengo la kuwasaidia watoto waliokosa malezi na
huduma mbalimbali za kijamii. Kituo hicho kinapatikana Kimara Suka
pamoja na Kijiji cha Mazizini Msata wilayani Bagamaoyo kinakabiliwa na
changamoto mbalimbali hivyo uongozi wa kituo hicho kinawaomba watu
binafsi na wafadhili mbalimbali kujitokeza kuwasaidia pindi waguswapo.
Mkurugenzi
wa kituo cha Watoto Wetu Tanzania, Bw. Evans Tegete akizungumza na
wanahabari (hawapo pichani) wakati wa utambulisho wa kituo hicho.
Bi.
Janet Sosthenes Mwenda (kushoto) akipata fursa ya kuwa na watoto
wanaolelewa kwenye kituo hocho cha Watoto Wetu Tanzania, kulia kwake ni
Mary Sanga kutoka kundi la marafiki wa “Mentoring and Networking”.
Muhamasishaji
na mchangishaji fedha wa “Mentoring and Networking”, Bi. Mary Sanga
akitoa nasaha na kushukuru wale wote walioguswa kwa kuchangia mpango
huo.
Bi. Janet Sosthenes Mwenda akipata fursa ya kuwa na watoto wanaolelewa kwenye kituo hicho cha Watoto Wetu Tanzania.
Bi.
Janet Sosthenes Mwenda akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) ambapo
ameiomba jamii kuwa na tabia ya kusaidia jamii isiyojiweza ikiwemo
watoto wanaolelewa kwenye vituo.
Binti
Cecilia Sospita anayelelewa kwenye kituo hicho cha Watoto Wetu Tanzania,
akishukuru kwa niaba ya watoto wenzake wanaolelewa kituoni hapo kwa
msaada uliowasilishwa na Bi. Janet Mwenda.
Msaada uliotolewa kusaidia kituoni hapo.
Kijana Samson Furgence akishukuru kwa niaba ya watoto wenzake wa kituo hicho.
Zoezi la utoaji wa zawadi likiendelea.
Watoto
na vijana wanaolelewa katika kituo hicho. Wengine ni wageni wa
kujitolea "Volunteer" wa kituo hicho kutoka nchini Ujerumani wakiwa
pamoja na watoto hao kituoni hapo.
Muhamasishaji na mchangishaji fedha wa “Mentoring and Networking”, Bi. Mary Sanga akitoa msaada katika tukio hilo.
Baadhi ya watoto na walezi wao wakifuatilia shughuli hiyo.
Janet Mwenda akishukuru watu mbalimbali kwa kumtia moyo katika kufanikisha shughuli hiyo.
Baadhi ya watoto hao.
Baadhi ya watoto hao.
Sala
maalum ya kuombea vitu hivyo vilivyoletwa kituoni hapo pamoja na Baraka
kwa waliofanikisha ikitolea na mmoja wa watoto wa kituo hicho.
No comments:
Post a Comment