Matukio : Mbunge wa Jimbo la Lindi aendelea kutimiza Ahadi zake Jimboni kwake - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


19 Jan 2016

Matukio : Mbunge wa Jimbo la Lindi aendelea kutimiza Ahadi zake Jimboni kwake


Hassani Selemani Kaunje
Mh Hassani Selemani Kaunje ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Lindi kupitia chama cha Mapinduzi (CCM) leo hii ameweza kutekeleza ahadi yake aliyowaahidi kikundi cha wanawake wachuuzi wa samaki cha Mitwero ya kuwapatia msaada wa Majokofu mawili (2) ya kutunzia Samaki.

Akikabidhi majokofu hayo leo hii Mh. Mbunge amewataka wachuuzi hao kutunza vitu hivyo kwani ni vyagharama na vitadumu kwa muda mrefu endapo wataviweka katika mazingira mazuri. Nao wanakikundi hicho cha akinamama wachuuzi wa samaki wameweza kupongeza hatua hiyo, wamemsifia kuwa ni mtu wa kutimiza ahadi kwani ametimiza kile alicho ahidi.
Hassani Kaunje
Mh. Mbunge amekuwa mstari wa mbele kutekeleza ahadi zake kwa kipindi hiki kifupi tangu alipochaguliwa na wananchi wa jimbo la Lindi mjini kwani hivi karibuni aliweza kutoa msaada wa Matanki ya kutunzia maji katika kata ya Kineng'ene.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad