Misa
ya kumbukumbu ya marehemu Leticia Nyerere iliyofanyika siku ya Jumamosi
January 16, 2016 katika kanisa la Mt. Edward Baltimore, Maryland na
kuhudhuriwa na ndugu, jamaa na marafiki kutok kila kona ya Marekani.
Mwili wa marehemu Leticia Nyerere unatarajia kufika Tanzania kesho
Jumanne January 19, 2016 na utaagwa Dar es Salaam na mazishi yake
yanatarajiwa kufanyika Butiana. Picha na Iska Jojo.
Wana
familia wakifuatilia misa ya kumbukumbu ya marehemu Leticia Nyerere
iliyofanyika siku ya Jumamosi January 16, 2016 katika kanisa la Mt.
Edward Baltimore, Maryland nchini Marekani. Kutoka kushoto ni Bi.
Kijogoo kutoka Arizona,,Margareth Mageni na ,Flora Mageni
Wanafamilia
wakiwemo watoto wa marehemu kutoka kushoto ni Julius Nyerere, Helena
Nyerere na Julia Nyerere kulia ni Edlaila Nyerere ambaye ni wifi wa
marehemu kutoka Atlanta jimbo la Georgia nchini Marekani wakifuatilia
misa ya kumbukumbu ya mpendwa mama yao Leticia Nyerere aliyeaga Dunia
siku ya Jumapili January 10, 2016 katika hospitali ya Jumuiya ya
Madaktari iliyopo Lanham, maryland nchini Marekani.
Balozi
wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Wilson Masilingi akitoa mkono wa pole
kwa mume wa marehemu Madaraka Nyerere kwenye misa ya kumbukumbu ya
marehemu Leticia Nyerere iliyofanyika siku ya Jumamosi January 16, 2016
katika kanisa la Mt. Edward Baltimore, Maryland na kuhudhuriwa na
ndugu, jamaa na marafiki
Balozi Wilson Masilingi akiongea machache na kutoa pole kwa wafiwa.
Bi Resty Budodi Semali rafiki wa marehemu kutoka Atlanta akiongea jambo ya jinsi alivyomfahamu marehemu.
Bhoke Nyerere kutoka Canada akisoma neno.
daktari wa familia Dr. Ndubisi akiongea jinsi alivyomfahamu marehemu.
Katibu mwenezi wa CCM DMV akielezea jinsi gani alivyomfahamu marehemu
Rais wa Jumuiya ya Watanzania DMV akitoa salamu za rambirambi kwa wafiwa na kuelezea jinsi gani alivyomfahamu marehemu.
Pius Mtalemwa mmoja wa viongozi wa Jumuiya ya Wakatoliki DMV akisema machache ya jinsi alivyomfahamu marehemu.
Watoto wa marehemu kutoka kushoto ni Julia, Julius na Helena.
Kwa picha zaidi BOFYA HAPA
No comments:
Post a Comment