Mbunge wa Monduli ,Julius Kalanga akitazama migomba iliyoharibiwa na
upepo mkali uliotokea katika kata ya mto wa mbu na kuharibu
migomba mingi katika kata ya mto wa mbu
Mbunge wa Monduli ,Julius Kalanga akitazama migomba iliyoharibiwa na upepo mkali uliotokea katika kata ya mto wa mbu na kuharibu migomba mingi katika kata ya mto wa mbu .Picha na Ferdinand Shayo
Mbunge wa Monduli ,Julius Kalanga akitazama migomba iliyoharibiwa na upepo mkali uliotokea katika kata ya mto wa mbu na kuharibu migomba mingi katika kata ya mto wa mbu .Picha na Ferdinand Shayo
Na Ferdinand Shayo wa Wazalendo 25 Blog,Arusha.
Wananchi wa
Kata ya Mto wa Mbu iliyoko wilaya ya Monduli wako hatarini kukumbwa na baa la
njaa kutokana na upepo mkali uliotokea jana majira ya saa kumi na moja jioni na
kuangusha migomba ya ndizi ambayo hutegemewa kama chakula kikuu na zao la
biashara.
Wakulima hao
walisema kuwa upepo huo mkali umeathiri mashamba makubwa ya migomba hivyo
wameiomba serikali ichukue hatua za haraka kunusuru hali ngumu ya upatikanaji
wa chakula itakayojitokeza siku zijazo.
Leyan
Ngaboli na Moses Lengine ni wakulima wa ndizi wamesema kuwa upepo huo
utasababisha kusimama kwa biashara ya ndizi kwa kiasi kikubwa kwani tayari
wakulima wameanza kupata hasara kwa kulazimika kuuza ndizi kwa bei ya chini ili
zisiharibikie mashambani.
Afisa Mtendaji wa Kata ya Mto wa Mbu
Kusumu Hassan alisema kuwa karibu kaya
na hekari zimeathiriwa na upepo huo hivyo ameiomba serikali isaidie wakulima
hao waweze kurejea katika kilimo hicho ambacho huzalisha ajira
nyingi.
Kwa upande wake Mbunge wa Monduli
Julius Kalanga aliyefanya ziara ya kuwatembelea waathirika wa upepo huo
amewataka wananchi kuchukua tahadhari huku akiahidi kushirikiana na serikali
kutafuta chakula cha msaada kutoka serikalini ili kuwasaidia wakulima hao kwa
kipindi ambacho wanaanza upya kulima mashamba yao kwani zao hilo huchukua muda
mrefu.
"Nitazungumza
na Mkuu wa Wilaya na Mkuu wa mkoa tuangalie uwezekano wa kupata chakula
cha msaada ili kunusuru kaya zilizoathirika" Alisema Kalanga
Kata ya Mto wa Mbu hutegemea kilimo
cha matunda matunda kama zao la biashara na chakula ambapo matunda mengi kutoka
kata hiyo hupelekwa katika masoko ya ndani nan je ya mkoa wa Arusha.
No comments:
Post a Comment