Waziri
wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe.
Ummy Mwalimu akizungumza na wafanyabiashara wa eneo la Msalato lililopo
mkoani Dodoma sehemu ambayo inatumika kufanyia mnada wa nyama choma
ikiwa ni moja ya ziara zake kufatilia hali ya ugonjwa wa kipindupindu
katika maeneo mbalimbali ya nchi, akiwa ameambatana na Mkuu wa Wilaya
hiyo, Dkt. Jasmine Tiisekwa (mwenye skafu shingoni) pamoja na Afisa
Afya Mkuu wa Manispaa ya Dodoma Bw. Alek Barakena (mwenye suti nyeusi).
Na Rabi Hume, Modewjiblog
Waziri
wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe.
Ummy Mwalimu ametembelea eneo la Msalato lililopo mkoani Dodoma sehemu
ambayo inatumika kufanyia mnada wa nyama choma ikiwa ni moja ya ziara
zake kufatilia hali ya ugonjwa wa kipindupindu katika maeneo mbalimbali
ya nchi.
Baada
ya kutembelea mnada huo, Mhe. Ummy aliwataka wananchi wa eneo hilo
kutambua kuwa bado ugonjwa wa kipindupindu upo na unaendelea kusambaa
maeneo mbalimbali ya nchi hivyo ni wajibu wao kama wananchi kuweka
mazingira yao katika hali ya usafi ili kutokomeza uonjwa huo.
Aidha
ili kuzidi kuzuia kuenea kwa ugonjwa wa kipindupindu, Waziri Ummy
ameagiza kuendelea kutekelezwa kwa agizo la Mkuu wa Wilaya hiyo, Dkt.
Jasmine Tiisekwa ambaye aliagiza kusimamishwa kwa shughuli za kuuza
nyama nyoma katika eneo hilo la Msalato mpaka uongozi wa wilaya hiyo
utakapojiridhisha kuwa ugonjwa wa kipindupindu umetoweka mkoani Dodoma.
“Kipindupindu
kimesambaa sehemu nyingi nchini ikiwepo hapa Dodoma na hivyo naagiza
katazo la Mkuu wa Wilaya, Dkt Jasmine Tiisekwa liendelee kuwepo hadi
ugonjwa wa kipindupindu uishe Dodoma na niwajibu wa kila mwananchi
kuhakikisha kipindupindu kinakwisha,” alisema Waziri Mhe. Ummy.
Pamoja
na hayo pia Waziri huyo wa Afya ameutaka uongozi wa Manispaa ya Dodoma
kufanya kikao cha pamoja na wafanyabiashara hao wa nyama choma ili kuona
ni jinsi gani wanaweza kuendelea na biashara zao huku wakizingatia
kanuni za usafi wa afya na mazingira bila kusababisha kuzidi kusambaa
kwa kipindupindu.
Waziri
wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe.
Ummy Mwalimu akifafanua jambo kwa wafanyabiashara wa eneo hilo.
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu
akitoa maagizo ya wafanyabiashara hao kusitisha shughuli zao mara
moja katika eneo hilo la Msalato mpaka uongozi wa wilaya hiyo
utakapojiridhisha kuwa ugonjwa wa kipindupindu umetoweka mkoani Dodoma.
Waziri
wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe.
Ummy Mwalimu (wa pili kushoto), Mkuu wa Wilaya hiyo, Dkt. Jasmine
Tiisekwa (wa tatu kulia) na Afisa Afya Mkuu wa Manispaa ya Dodoma Bw.
Alek Barakena (kushoto) wakisikiliza hoja kutoka kwa mmoja wa
wafanyabiashara wa eneo hilo (hayupo pichani).
Waziri
wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe.
Ummy Mwalimu akisikiliza hoja kutoka kwa mmoja wa wafanyabiashara
wa eneo la Msalato lililopo mkoani Dodoma sehemu ambayo inatumika
kufanyia mnada wa nyama choma ambaye jina lake halikupatikana alipofanya
ziara ya katika eneo hilo.
No comments:
Post a Comment