Meneja wa Mradi wa Kansa ya Shingo ya Kizazi wa UMMATI, Jeremiah
Makula akizungumza wakati wa utoaji tuzo kwa wadau wa mradi wa kansa ya
Shingo ya Kizazi iliyofanywa, PSI Tanzania, Marie Stopes pamoja na
UMATI iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Kanda Kusini Mwa Afrika, Ulla Muller akizungumza
wakati wa utoaji tuzo kwa wadau wa mradi wa kansa ya Shingo ya Kizazi
iliyofanywa, PSI Tanzania, Marie Stopes pamoja na UMATI iliyofanyika leo
jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Kinga wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto, Neema Rusibamayilla akizungumza wakati wa utoaji tuzo
kwa wadau wa mradi wa kansa ya Shingo ya Kizazi iliyofanywa, PSI
Tanzania, Marie Stopes pamoja na UMATI iliyofanyika leo jijini Dar es
Salaam.
Wakurugenzi wa Mashirika yaliyokuwa na Mradi wa Kansa ya Shingo ya
Kizazi pamoja na wawakilishi wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto wakifatilia maada wakati wa mkutano wa utoaji wa
tunzo kwa wadau wa mradi iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya wadau wakifatilia maada wakati wa utoaji tunzo kwa
mashirika yaliyokuwa katika mradi wa kansa ya Shingo ya Kizazi
iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
(Picha na Chalila Kibuda wa Globu ya Jamii).
Na Chalila Kibuda ,Dar.
WADAU wa wanaoshughulika na kansa ya shingo ya kizazi kwa wanawake
ni wachache ikilinganishwa na mahitaji yaliyopo nchini kwa tatizo
hilo.
Akizungumza katika mkutano wa wadau waliokuwa wakifanya Mradi wa
Kansa ya Shingo ya Kizazi na Kinga kwa wanawake dhidi ya kansa hiyo,
Mkurugenzi wa Kinga wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee
na Watoto, Neema Rusibamayilla amesema serikali inatambua juhudi za
wadau ambao wamekuwa wakifanyia wanawake juu ya kinga ya kansa ya shingo
ya kizazi.
Amesema serikali itaendelea kushirikiana wadau mbalimbali katika
kukabili tatizo la kansa ya kizazi ikiwa ni pamoja na kutoa elimu kwa
wanawake kujitokeza kupima afya zao na inapotokea na tatizo hilo
kushughulikiwa kwa haraka.
Neema amesema serikali itaendelea kutoa ushirikiano zaidi kwa pale
inapohitajika katika kukabili tatizo la kansa ya shingo ya kizazi
kutokana na serikali peke yake haiwezi kushugulikia matatizo kwa wakati
mmoja.
Nae Mkurugenzi Mtendaji wa UMATI, Lulu Ng’wanakilala amesema kansa
ya kansa ya shingo ya kizazi inaua hivyo ni lazima wanawake kupima mara
kwa mara kabla tatizo halijawa kuwa kubwa.
Amesema wadau wanaoshughulika na kansa hiyo ni wauchache
ikilinanishwa na tatizo lilopo hasa katika maeneo ya vijijini ya kuwa na
wanawake wengi ambao hawajafikiwa kwa kupima au kupata huduma hiyo.
Kwa upande wa Mkurugenzi Mkazi wa Marie Stopes ,Anil Tambay
akiwakilisha wadau walikuwa katika mradi huo amesema mafanikio
walioyapata katika mradi huo ni kwa kusaidia wanawake uhai katika utoaji
wa tiba ya kansa ya shingo ya kizazi.
No comments:
Post a Comment