Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Kigwangalla.
Na Rabi Hume, Modewjiblog
Naibu
Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee,
Dkt. Hamisi Kigwangalla ameanzisha kikosi kazi cha watu 24 ambacho
kitakuwa na kazi ya kutengeneza mpango mkakati wa kuwezesha kuboresha
Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF).
Katika
taarifa ambayo imetolewa na Dkt. Kigwangala imeeleza kuwa kazi ya
kuanzisha kikosi kazi hicho ni agizo kutoka kwa Waziri wa Wizara ya
Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu ambaye
alimtaka aanzishe kikosi hicho ili washirikiane kuanzisha mpango mkakati
wa kuwezesha kuboresha Mfuko wa Afya ya Jamii.
“Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Ally
Mwalimu alinipa kazi ya kuunda kikosi kazi maalum na kushirikiana nacho
kutengeneza mpango mkakati wa kuboresha Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF),”
alisema Dkt. Kigwangalla.
Dkt.
Kigwangalla amewataja wajumbe wa kikosi kazi hicho kuwa ni Prof.
Angwara Kiwara, Prof. Phares Mujinja, Dkt. Francis Frederick, Dkt. Heri
Marwa, Dkt. Deogratius Pisa, Dkt. Amos Kahwa, Irenei Kiria, Semkae
Kilonzo, Gemini Mtei, Dkt. Jehovaness Aikaeli na Obey Assey.
Wengine
ni Mathias Kabunduguru, Dkt. Dereck Chitama, Prof. Flora Kessy,
Florence Mwanri, Athuman Rehani, Maximillian Mapunda, Bedason Shallanda,
Daniel Ngowi, Beng' Issa, Edwin Mikongoti, Hussein Sengu, Dkt. Beatus
Leon na Dkt. Pastory Sekule.
Aidha
Dkt. Kigwangalla amewashukuru wajumbe hao kwa kukubali kufanya kazi na
Wizara ya Afya kupitia mpango mkakati wa kuwezesha kuboresha Mfuko wa
Afya ya Jamii bila malipo yoyote.
Hata
hivyo mara baada ya kuwachagua wajumbe wa kikosi kazi hicho tayari
kimependekeza mapendekezo yao jinsi ya kuboresha Mfuko wa Afya ya Jamii
ambayo ni kuipa nguvu kadi ya CHF ili itumike kwenye mfumo wa Afya mpaka
ngazi ya Hospitali za Rufaa za Mikoa na vituo vya Jirani na kupandisha
kiwango cha kuchangia CHF mpaka 30,000.
Mapendekezo
mengine ni kuweka bei za kukatisha tamaa watumiaji wa huduma za Afya
bila kadi ya Bima ya Afya ama ya CHF na kuwahamasisha waamue kujiunga
kuliko kulipa gharama za kila huduma watakayotumia, kuhamisha Mfuko wa
fedha za CHF kutoka Halmashauri na kuupeleka NHIF ngazi ya mkoa lengo
likiwa kumtenganisha mtoa huduma na mteja na kuweka 10,000 kuwa kiwango
cha chini kwa bei za huduma za afya sehemu yoyote nchini kwa mtu asiye
na kadi.
Aidha
mapendekezo yao yatatumika kama serikali itayaridhia na wao wametoa
mapendekezo hayo kutokana na kutambua kuwa Watanzania wapo tayari
kulipia huduma za afya kwa bima ilimradi wawe wanapatiwa huduma bora
ambazo zitawaridhisha.
No comments:
Post a Comment