Mkuu wa ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa
linalohudumia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Zulmira
Rodrigues akisoma hotuba mbele ya wageni waalikwa waliofika kwenye
uzinduzi wa Ripoti ya Mafanikio ya Mradi wa Wasichana walioacha shule
kwa sababu za Ujauzito unaofadhili Ubalozi wa Japan na kuratibiwa na
UNESCO.
(Picha zote na Geofrey Adroph wa Pamoja blog)
Kamishana wa Elimu kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi nchini
Prof, Eustella Bhalalusesa akizungumza jambo pamoja na kuwashukuru
wadau ambao ni hirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia Elimu, Sayansi
na Utamaduni (UNESCO) pamoja Ubalozi wa Japani nchini Tanzania ambao
wamefanikisha mradi huo wakati wa uzinduzi wa ripoti ya mafanikio ya
mradi wa Wasichana walioacha shule kwa sababu za Ujauzito unaofadhili
Ubalozi wa Japan na kuratibiwa na UNESCO.
Balozi wa Japani nchini Tanzania Mh. Masaharu Yoshida akisoma hotuba
yake wakati wa uzinduzi wa Ripoti ya mafanikio ya mradi wa Wasichana
walioacha shule kwa sababu za Ujauzito uliofadhiliwa Ubalozi wa Japan na
kuratibiwa na UNESCO Tanzania.
Mshauri na Mwakilishi kutoka shirika la UNFPA, Anna Holmstrom akitoa
ufafanuzi wa ripoti iliyofanyika katika mkoa wa Shinyanga juu ya wazazi
wenye umri mdogo waliopta mimba wakiwa bado shuleni.
Ofisa mipango ya Elimu wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni
(UNESCO) Tanzania, Jennifer Kotta ambaye alikuwa ni msimamizi wa mradi
akitolea ufafanuzi kuhusu mradi huo ikihusisha changamoto pamoja na
faida za mradi huo uliofanyika Mkoani Shinyanga.
Baadhi ya wageni waliofika katika uzinduzi wa Ripoti ya mafanikio ya
mradi wa Wasichana walioacha shule kwa sababu za Ujauzito unaofadhili
Ubalozi wa Japan na kuratibiwa na UNESCO.
Katibu Tawala wa mkoa Shinyanga, Bw. Abdul Rashid Dachi akizungumza jambo wakati wa uzinduzi huo wa ripoti hiyo.
Mkuu wa ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa
linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Zulmira
Rodrigues (kushoto) akitolea ufafanuzi moja ya picha zilizopigwa mkoani
Shinyanga wakati kukabidhi vyeti kwa wahitimu walionufaika na mafunzo
mbalimbali kupitia mradi huo.
Subira akitoa ushuhuda kwa jinsi alivyopata ujauzito akiwa shuleni na
alivyofanikiwa kutokana na Mradi wa Shirika la Umoja wa Mataifa
linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) chini ya ufadhili
wa Ubalozi wa Japan.
Veronika Amosy akitoa ushuhuda na kueleza changamoto zilizomkuta mara baada ya kubeba mimba akiwa shuleni.
Mkufunzi Mkazi wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima Bw. Said Kayege
kutoka mkoani Shinyanga akizungumza ni kwa namna gani wanavyotoa mafunzo
hasa kwa mabinti waliopata mimba wakiwa mashuleni na kupelekea kuacha
masomo yao.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu ya Watu wa Wazima nchini, Dk. Fidelis
Mafuniko akizungumza jambo wakati wa uzinduzi wa ripoti ya wazazi wenye
umri mdogo walio pata mimba wakiwa shuleni.
Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa
linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Zulmira
Rodrigues kwenye picha ya pamoja na wasichana waliopata mimba wakati
wako masomoni ambao ni Veronika Amos (kushoto) pamoja na Subira
(kulia).
Picha ya Pamoja
Na Mwandisi wetu
Shirika la Elimu, sayansi na utamaduni (UNESCO) lazindua Ripoti ya
wazazi wenye umri mdogo walio pata mimba wakiwa shuleni, ambapo kama
shirika waliweza kuwasaidia kwa kuwaanzishia mfumo maalumu utakao
wasaidia katika kujiendeleza kielimu kwa kushirikiana na Elimu ya watu
Wazima MOEVT.
Akiongea wakati wa uzinduzi huo mgeni rasmi Kamishna wa Elimu kutoka
Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufund (MOEVT)i nchini Prof, Eustella
Bhalalusesa amesema cha kwanza ni kuishukuru serikali ya Tanzania kwa
kuweka ushirikiano na shirika hili la UNESCO kwani ni jambo zuri hasa
ukizingatia wote wanafanya kazi zinazo endana , cha pili nikuendelea
kuungana kwa ajili ya kuweza kutoa elimu ya jinsia kwa ajili ya kuepuka
mimba za utotoni kwa wanafunzi walioko mashuleni hivyo ameipongeza
(UNESCO) kwa kutambua thamani ya watoto wa kike hasa wale walioshindwa
kuendelea na masomo kwa kuwaanzishia njia mbadala za kuweza kuwafundisha
kwa kuungana na elimu ya watu wazima kwani msingi wa watoto hao ni
Elimu.
Naye Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa
linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Zulmira
Rodrigues amesema wao kama shirika walianza kufanya mchakato wa kufanya
tafiti kwa mikoa mbalimbali na kugundua kwamba watoto wengi wa jinsi ya
kike wameweza kukatiza masomo yao kutokana na kupata mimba pindi wawapo
shuleni ndipo walipoamua kuanzisha namna ya kuweza kumkomboa mtoto wa
kike aweze kupata elimu inayoweza kumsaidia katika maisha yake kwa
kuweza kuwasiliana na Mkurugenzi wa elimu ya watu wazima MOEVT na
kuanzisha mchakato wa kuweza kuwakomboa kielimu. Vilevile Bi. Rodrigues
aliongeza kwa kusema wazazi waweze kukaa na watoto na kuwafundisha elimu
ya kijinsia na kuweza kuwatatulia shida mbalimbali walizonazo kwani
ndio hupelekea watoto kuingia katika tamaa mbalimbali hususani wakiwa
katika hatua za mabadiliko ya mwili.
Naye Balozi wa Japani nchini Tanzania Mh. Masaharu Yoshida amesema
wazazi wenye umri mdogo Tanzania ni wengi na wanauhitaji wa kupata
mafunzo ya Elimu kwa hali na mali hivyo kama ubalozi wa Japan umeamua
kuanzisha mradi wa kuwasaidia wazazi hao mradi huo ambao unaratibiwa na
(UNESCO) ulianza toka mwaka 2012 ambapo ulianzishwa na Bi.Zulmira
Rodrigues, Mr. Min Jeong Kim na Jennifer Alima-Kotta uliogharimu kiasi
dola za Kimarekani 400,653 kutoka Japanese Funds-in-Trust, Lengo kubwa
ni kutaka kumkomboa mtoto wa kike ambaye amepata au alipata ujauzito
akiwa shuleni, Pia alitoa shukrani kwa Shirika la Elimu, Sayansi na
Utamaduni (UNESCO) kwa kuweza kuwapa ushirikiano kuanzia walipoanza
mpaka hivi leo na aliweza toa wito kwa serikali ya Jamhuri ya Muungano
ya Tanzania kwa kuomba kuendelea kupambana na mimba za wanafunzi wawapo
mashuleni na kuendelea kutilia mkazo sheria zitakazo wabana watu wanao
sababisha ujauzito kwa mtoto wa kike awapo shuleni.
Aidha Ofisa Mipango ya Elimu wa Shirika la Elimu, Sayansi na
Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Jennifer Kotta msimamizi wa mradi huo
alieleza dhumuni la mradi na namna gani wameweza kufanikiwa pamoja na
changamoto zake ambapo alianza kwa kueleza kuwa mradi huo sio rasmi ndio
maana wameweza kushirikiana na elimu ya watu wazima kwani wanafunzi
wengi wa kike huwa wanapata vishawishi mbalimbali pindi wawapo mashuleni
na kuweza kuwa sababishia kuwa wazazi wadogo.
Kotta
amesema kumekuwa na mambo mengi yanayo wakumba wanafunzi wa kike wawapo
mashuleni na ndio husababisha madhara makubwa ambayo hupelekea wanafunzi
hao kuwa wazazi wenye umri mdogo na bila kutegemea kwani ni ajabu na ni
jambo la kusikitisha sana mtoto ana mlea mtoto mwenzake na kuwa na
imani kuwa ndoto zake haziwezi timia kwa kutoendelea na masomo pindi
awapo mjamzito au pindi akijifingua, ambapo aliwaomba wazazi kwani hali
iliyopo kwa sasa kwa watoto wetu si nzuri sana tukumbuke kuwahimiza
watoto kuhusu mila na desturi zetu na pia kuwa wafuatiliaji kwa nguvu
zote kwani wazazi wengu huwa wanawadharau watoto wa kike kwa kudhani
hawana msaada na ndipo yeye kama mtoto anaamua kuchukua uamuzi wake
binafsi na kukuta wanaangukia katika hali ya kuwa mzazi mwenye umri
mdogo vilevile aliweza kusisitiza kuhusu kuwalinda watoto wa kike hasa
kipindi cha mabadiliko ya mwili ambapo ndipo changamoto mbalimbali
hutokea kwa watoto hao hasa pindi wawapo mashuleni na hata mitaani.
Hata hivyo mmoja ya wazazi wadogo walioweza kuchukuliwa na kusaidiwa
na Shirika la (UNESCO) Tanzania, Chausiku Subira aliweza kutoa ushuhuda
namna gani wanavyokumbana na changamoto hizo mpaka hatimaye kuwa wazazi
katika umri mdogo wakiwa bado ni wanafunzi. "katika safari yangu ya
kimasomo mara baada ya kumaliza elimu ya msingi niliweza kuchaguliwa na
kuendelea na elimu ya pili hapo ndipo ndoto zangu zilipoishia kwa kupata
ujauzito ambao ulinipelekea kufukuzwa shule na hatimaye kurudishwa
nyumbani jambo lililokuwa gumu kwangu kwani ujauzito huo ulikuwa sio wa
kutegemea hasa ukizingatia mimi nikiwa bado mwanafunzi, nyumbani
walinifukuza na kusababisha niwe na maisha magumu nisiyo ya tarajia
nikizingatia nimepoteza shule pia hata ndugu hawanitaki lakini hiyo yote
ni kutoka na na miundombinu ya shule tunazo soma kuwa mbali na makazi
na kupelekea wanafunzi wengi kutembea kwa mguu umbali mrefu huku wakiwa
na njaa na kuingia katika vishawishi mbalimbali", alisema Subira.
Pia Subira aliweza kutoa wito kwa serikali kwa kujenga mabweni katika
shule mbalimbali na kuweza kuwatengenezea mazingira ya kuweza kurejea
mashuleni pindi wanapojifungua kwa ajili ya kuweza kutimiza ndoto walizo
kuwanazo pia kuweka sheria ambayo itakuwa inatenda haki kwa kila mmoja
kwani imekuwa ni kwa mtoto wa kike tu kufukuzwa huku aliye sababisha
ujauzito mtoto wa kiume kubaki akiendelea na masomo vilevile katika
upande wa shule kuweza kutoa mafunzo kwa watoto wa kike kuhusu elimu ya
jinsia na ninamnagani wanaweza wakajiepusha na vishawishi wanavyo
kutananavyo.
No comments:
Post a Comment