Waziri
wa Afya, maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu
akitembelea moja ya ghala la kuhifadhia dawa iliyopo makao makuu ya
MSD,kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa MSD Laureane Bwanakunu na watatu
kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya MSD Prof.Idris Mtulia.
.............................. ..............
Waziri
wa Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu
ametembelea Makao Makuu ya Bohari ya Dawa (MSD) na kuahidi kuwa balozi
wa kuhakikisha deni la serikali linalipwa ili kuiwezesha MSD kutekeleza
majukumu yake kwa ufanisi.
Waziri
huyo ameeleza hayo baada ya Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Laurean Bwanakunu
kueleza kuwa ukosefu wa fedha na deni la serikali ni changamoto kubwa
inayoathiri utekelezaji mzuri wa majukumu ya MSD.
Mbali
na hilo, Waziri wa Afya amesema mbali na deni hilo, hata kiasi cha
fedha kinachotengwa na serikali kwaajili ya hospitali, vituo vya afya na
zahanati na kununua dawa hakitoshelezi mahitaji, hivyo lazima suala
hilo lifanyiwe kazi mapema, huku akisisitiza hata kiasi hicho kidogo
kinachopatikana kitumike vizuri.
Katika
hatua nyingine ameishauri Bohari ya Dawa kuanza utaratibu wa kununua
dawa na vifaa tiba moja kwa moja kutoka kwa wazalishaji, kuhakikisha
dawa muhimu zinapatikana wakati wote na kuiagiza MSD itangaze kwenye
vyombo vya habari dawa zote ambazo zinapelekwa vituoni, zahanati na
kwenye hospitali, ambapo Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Laurean Bwanakunu
ameeleza kuwa tayari MSD imeshaanza kubandika kwenye mbao za matangazo
za hospitali orodha ya dawa inazofikisha.
Waziri
huyo ambaye alifuatana na Katibu Mkuu wa Wizara, Dkt. Donald Mbando na
watendaji wengine pia alitembelea maghala ya kuhifadhia dawa ya MSD,
jengo la ofisi linalojengwa pamoja na kuwa na mkutano na menejimenti ya
MSD, ambapo pamoja na mambo mengine ameipongeza MSD kwa hatua iliyofikia
ya kuweka nembo ya GOT kwenye vidonge vyake ili kudhibiti upotevu wa
dawa za serikali pamoja na kuanzisha maduka ya dawa Muhimbili, na
mengine yanayotarajia kufunguliwa hivi karibuni mkoani Mbeya, Arusha na
Mwanza.
Waziri
Ummy Mwalimu alihitimisha kwa kusema kuwa ajenda yake kuu ni
upatikanaji wa dawa kwa wakati, kama rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Dkt. John Magufuli alivyoaainisha, hivyo MSD itekeleze
majukumu yake ipasavyo kwani mafanikio ya MSD ni mafanikio kwake pia.
Waziri Ummy akiuliza jambo kwa wafanyakazi wa bohari hiyo.
Waziri
huyo akiendelea na ukaguzi wa maghala hayo, kulia ni Mkurugenzi wa
Ugavi Misanga Muja na kushoto ni mwenyekiti wa Bodi ya Bohari hiyo.
Baadhi ya watumishi wakiendelea na kazi ya kuhakiki dawa kwenye moja ya ghala mojawapo.
Waziri
Ummy akielekea kwenye ujenzi wa jengo jipya linaloendelea kujengwa,
ambapo linatarajiwa kumalizika kujengwa mwezi Juni, 2016 ,Kushoto ni
Katibu mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Donnan Mmbando.
Mkurugenzi wa MSD Bwanakunu akieleza dira,malengo na majukumu ya Bohari hiyo.
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu
akiangalia dawa zilizowekwa nembo ya serikali (GoT) ambayo itasaidia
udhibiti wa upotevu wa dawa nchini.
Waziri
Ummy akimuonesha ukurasa wa ugawaji fedha za bohari Mwenyekiti wa Bodi
ya Bohari ya dawa Prof.Idris Mtuliya.(Picha zote kwa Niaba ya Wizara ya
Afya).
No comments:
Post a Comment