Michezo: Ligi Kuu ya Zanzibar KVZ na JKU Mchezo uliofanyika Uwanja wa Amaan Timu ya JKU Imeshinda 2 -0 - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Thursday, 31 December 2015

Michezo: Ligi Kuu ya Zanzibar KVZ na JKU Mchezo uliofanyika Uwanja wa Amaan Timu ya JKU Imeshinda 2 -0


Wachezaji wa Timu ya JKU wakisalimiana na Wachezaji wa Timu ya KVZ kabla ya kuaza mchezo wao wa Ligi Kuu ya Zanzibar uliofanyika Uwanja wa Amaan Zanzibar Timu ya JKU imeshinda 2--0.
Mchezo uliochezwa jioni mabao ya JKU yamefungwa katika kipindi cha kwanza na katika dakika ya 8 mshambuliaji wa Timu ya JKU Mbarouk Chande ameipatia bao timu yake katika dakika ya nane ya mchezo huo kipindi cha kwanza na Bao la ushindi la JKU limepatikana katika kipindi hicho cha kwanza katika dakika ya 35 ya mchezo huo lililofungwa na mshambuliaji wake Nassor  Mattar.
Kocha Mkuu wa Timu ya KVZ King akifuatilia mchezo huo wakati timu yake ikiwa nyuma kwa mabao 2--0 
Beki wa timu ya KVZ Juma Abdalla, akijiandaa kumzuiya mshambuliaji wa Timu ya JKU mwenye mpira Nassorv Mattar, wakati wa mchezo wao wa Ligi Kuu ya Zanzibar uliofanyika uwanja wa Amaan Zanzibar. 
Mshambuliaji wa Timu ya JKU Mbarouk Chande(kulia) akimpita beki wa Timu ya KVZ Emill Wiliam  

Mshambuliaji wa Timu ya JKU Mbarouk Chande, akimiliki mpira huku beki wa timu ya KVZ Emill William akijiandaa kumzuiya.  
Mshambuliaji wa Timu ya JKU Mohammed Abdalla akimpiga chenga golikipa wa timu ya KVZ Yakub Bakari. hatimai mpira huo na kutoka nje ya uwanja. 

Mshambuliaji wa Timu ya KVZ Masoud Abdalla mwenye jezi ya kijani akimpita mchezaji wa timu ya JKU  Mbarouk Chande. 
Imetayarishwa na OthmanMapara.Blogspot
Zanzinews.com.

No comments:

Post a Comment