Mkuu wa Idara ya Fedha wa Benki ya NMB, Veronica Pascal (wa pili kushoto) akipokea tuzo kwa niaba ya NMB toka kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Dk. Hamisi Mwinyimvua baada ya kuibuka washindi wa kwanza kwa kuwa na hati safi ya taarifa za fedha kwa upande wa mabenki nchini katika ukaguzi uliofanywa na Bodi ya Taifa ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu (NBAA) kwa mwaka 2014. Tuzo hizo zilitolewa jana Bunju nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam na Bodi ya Taifa ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu Tanzania. Jumla ya makampuni na taasisi 58 zilishiriki katika kinyang'anyiro hicho cha ukaguzi wa taarifa za fedha kwa hiyari. |

Wawakilishi wa Benki ya NMB, Veronica Pascal (kushoto) akipiga picha ya ukumbusho mara baada ya kupokea tuzo kwa niaba ya NMB baada ya kuibuka washindi wa kwanza kwa kuwa na hati safi ya taarifa za fedha kwa upande wa mabenki nchini katika ukaguzi uliofanywa na Bodi ya Taifa ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu (NBAA) kwa mwaka 2014. Tuzo hizo zilitolewa jana na Bodi ya Taifa ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu Tanzania.
No comments:
Post a Comment